Ligi kuu ya England imeendelea kwa mechi mbili ambapo..Arsenal imeibamiza Man City ,Huku Westham Ikiibamiza Hull City bao 3-0
Nayo
Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ikiwa imeng'oa nanga hapo
jana kwa Gabon Kuilaza Burkina faso bao 2-0 Huku Pierre Emerick
Aubemeyang aking'ara vilivyo.Nao wenyeji Equitorial Guinea wakishikwa
shati na Congo Brazaville kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Ligi
kuu ya England ambapo Jumapili zimechezwa mechi mbili ,Katika mechi ya
awali Westham United iliibamiza Hull City bao 3-0 mabao yaliyotiwa
kambani na Andy Carrol katika dakika ya 49,Amalfitano katika dakika ya
69 na Stewart Downing aliyehitiisha ushindi huo mnono wa Westham katika
ya 72 akimalizia pasi murua ya kiungo Mcameroun aliyeko kwenye Fomu
Alexandre Song.
Kwa matokeo hayo Westham imefikisha Point 36
wakiwa nafasi ya 7,wakiwa pointi moja mbele ya Liverpool wenye pointi 35
walioko nafasi ya 8,huku timu hizo zikitaraji kukutana katika mechi
ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.