Wednesday, May 13, 2015

RAIS NKURUNZIZA APINDULIWA...!!!

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi
Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
 
Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu

JACQUELINE WOLPER: ANAETOKA NA NAY WA MITEGO AMESHAJULIKANA

Jacqueline Wolper

Muigizaji wa filamu zabkibongo, Jacqueline Wolper amewaweka njiapanda mashabiki wake kwa kaul yake kuwa msichana aliye katika uhusiano wa kimapenzi na msanii wa bongo flava Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' amekwishafahamika tofauti na alivyokuwa akihisiwa yeye.

 "Watu hawana dogo, ukiwa na ukaribu na mtu unaambiwa ni mpenzi wako, Nay hakuwahi kuwa mpenzi wangu kwa kuwa ni zaidi ya rafiki kwangu, ila watu wasio waelewa ndiyo waliokuwa wakivumisha kuwa tuna uhusiano kwa maslahi yao, lakini sasa ukweli umejulikana kama mnavyoona na mnavyosikia Nay ni wa nani" alieleza Jacqueline bila kuweka wazi ni nani anatoka na mwana hip hop huyo.

 Wolper aliongeza kuwa taarifa hizo ziliposanbaa alipata tabu ambapo alitumia muda mwingi kutolea maelezo kwa watu wake wa karibu.




BARCELONA YATINGA FAINALI

Messi, Suarez na Neymar wakishangilia bao

Miamba ya soka Hispania, Barcelona wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 waliyokusanya katika mikondo yote miwili waliyokutana katika hatua ya nusu fainali.
 Katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo ambao ulipigwa katika dimba la Allinza Arena, Bayern walipaswa kushinda bao nne bila ili wapate tiketi ya kusonga mbele.
 Lakini mpaka kipyenga kinapulizwa the Bavarian 3,Barcelona wakajipatia mabao mawili.
 Leo usiku kutakuwa na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus katika dimba la Banabeu.

NGASSA ASAINI KUCHEZA AFRIKA KUSINI

Mrisho Ngassa

 Mshambuliaji hodari wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa amemwaga wino wa kuichezea timu ya Free State Stars ya ligi kuu Afrika Kusini kwa miaka minne.

 Ngassa ameripotiwa kufurahia mkataba huo mnono na kuanza maisha yake mapya baada ya kucheza nyumbani kwa miaka kadhaa.

"Nataka kuitumia fursa hii kutangaza soka la Tanzania na nitajituma ili kufanya vizuri zaidi" alisema mchezaji huyo.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii Ngassa ameonekana akiwa na kocha wa timu hiyo mara baada ya kusaini mkataba.


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...