Friday, December 19, 2014

HII NDIO LIST YA WASANII 10 WA NIGERIA WALIOVNJA REKODI YA KUTAFUTWA KUPITIA GOOGLE

davido
Mwaka unaisha, kwenye ule mfululizo wa rekodi mbalimbali za mwaka 2014 bado kuna nyingine nyingi millardayo.com itakuwa ikikupatia. Tumezisikia rekodi nyingi za nje ya Afrika, sasa hivi moja ya jitihada ninazozifanya ni kukusanya zile rekodi za Afrika na kukuletea mtu wangu.
Davido ni mmoja ya mastaa ambao tukiuzungumzia muziki wa Afrika Magharibi, jina lake ni moja ya majina ambayo yameng’aa sana kwa mwaka 2014. Mtandao wa Google umemtaja Davido kwamba ni staa namba moja kwa kwa wanamuziki wa Nigeria aliyetafutwa zaidi mwaka 2014 kwenye mtandao.
Kwenye list hiyo Phyno ameshika namba mbili na nafasi ya tatu kushikwa na the Marvin’s Queen, Tiwa Savage. List kamili hii hapa....

 1. Davido
2. Phyno
3. Tiwa Savage
4. Don Jazzy
5. Timaya
6. Ice Prince
7. Olamide
8. Sean Tizzle
9. Lil’ Kesh
10. Burna Boy


 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 19, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

DSC07327

DSC07328
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KENYATTA ASAINI SHERIA KALI YA USALAMA

Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

HILI NDILO GARI LINALOWEZA KUJIENDESHA KWA KUTUMIA SAA

Kampuni ya BMW imezindua kifaa ambacho kinawezesha gari lako kujiegesha lenyewe.
 

Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.
Lakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.
Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.

Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia saa ya mkononi ambayo inabonyezwa na dereva.
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.

WENGER AIOGOPA LIVERPOOL KUFUATIA KIPIGO

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger asema kuwa anaogopa kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya timu yake wakati wa mechi kati ya LIverpool na Arsenal msimu uliopita.
 
Kocha wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba anaogopa kichapo cha 5-1 alichokipata wakati timu yake ilipochuana na Liverpool msimu uliopita, lakini akaongeza kuwa hatarajii kichapo kama hicho wakati timu hizo mbili zitakapokutana siku ya jumapili.
Arsenal ilikuwa imefungwa mabao 4-0 kufikia dakika ya 20 wakati wa mechi hiyo iliochezwa Anfield huku Liverpool ikiongozwa na mshambuliaji hatari ambaye ameihama kilabu hiyo Luis Suarez.Mechi hiyo ilikamilika ikiwa 5-1 dhidi ya Arsenal.
Lakini meneja huyo wa Arsenal anaamini mengi yamebadilika katika kipindi cha miezi 10,ikiwemo kuondoka kwa Suarez na jeraha la mshambuliaji Daniel Sturridge na mafanikio yake ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka Barcelona mbele ya Breanda Rodgers.
 
Liverpool washerehekea ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Anfield msimu uliopita.
Wenger alisema;Liverpool ilifunga zaidi ya mabao 100 mwaka uliopita.
Walikuwa wazuri sana katika safu ya mashambulizi,lakini msimu huu wamefunga mabao 19 pekee,hawana tena moto wa kufunga mabao waliokuwa nao.
Walianza kwa mori siku hiyo na sisi tulishindwa kujibu mashambulizi yao.
Kila mechi unayoshindwa inakua kovu katika moyo milele.Lakini tuna kumbukumbu nzuri katika uwanja wa liverpool.
Tulishinda mechi nyingi sana katika uwanja huo,lakini utakumbuka kwamba juma moja baadaye tuliweza kuishinda timu hiyo hiyo tulipocheza nayo nyumbani katika kombe la FA.' Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

FIFA SASA KUCHAPISHA RIPOTI YA GARCIA

 Aliyekuwa mchunguzi wa kamati ya maadili katika shirikisho la soka FIFA. 
 
Maafisa wakuu wa shirikisho la FIFA wamekubaliana kuchapisha ripoti yote kuhusu uchunguzi wa madai ya ufisadi uliotokea wakati wa kutolewa kwa kandarasi za kombe la dunia kwa mataifa ya Urusi mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
Wamekubaliana kutoa kurasa 430 za uchunguzi wa Michael Garcia baada ya kufanya mkutano kufuatia pendekezo la mkuu wa kufuata maagizo Domenica Scala.
Ripoti hiyo itawekwa wazi baada ya uchunguzi unaondelea kuhusu watu watano kukamilika na inatarajiwa kufanyiwa uhariri ili kuficha majina ya mashahidi.
Hatua hiyo ya kuichapisha ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera baada ya FIFA kukataa shinikizo kutoka kwa Garcia mwenyewe na wengine kutoa ripoti hiyo.
Garcia alijiuzulu siku ya Jumatano baada ya ombi lake la kupinga ripoti fupi ya uchunguzi wake iliotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maadili katika shirikisho hilo Hans-Joachim Eckert kukataliwa.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...