Wednesday, February 20, 2013

Dkt. Shein aongoza Wazanzibar kutoa heshima za mwisho kwa Padri Evarest Mushi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi, katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, ambapo alifika kutoa salamu ya mwisho kwa Padri huyo aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita, na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(kushoto)  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(katikati) Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.

Baadhi ya Waombolezaji wakiwa ndani ya Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar wakati wa kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel  Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Naibu Waziri wa TAMISEMI ataka watendaji wa vijiji Singida kufanya kazi ya kuandikisha wanafunzi wa madarasa ya awali na msingi.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida na baadhi ya watendaji wa sekta ya elimu. Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuinua taaluma mkoani Singida yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida. Kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa (hayupo kwenye picha). (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.
 Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani Singida.
Amesema kutokana na ukweli huo, serikali  itafanya kazi ya uandikishaji watoto wenye sifa ya kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, ni watendaji wa vijiji na kazi hiyo, itakuwa na ufanisi mkubwa kuliko kipindi cha miaka ya nyuma.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa kila mtendaji wa kijiji anapaswa kuwakilisha ripoti ya kazi ya uandikishaji wanafunzi wa shule za awali na wale wa msingi mbele ya kikao cha maendeleo ya kata (WDC)  ili kupata Baraka ya kikao hicho.
 Majaliwaa mesema ili kuipa umuhimu mkubwa elimu ya awali ni lazima kuwepo na bajeti ambazo zitaonyesha ongezeko la shule za awali.
 Katika hatuna nyingine, Naibu Waziri huyo amekumbusha kuwa kila shule ya msingi ni lazima iwe na vyumba vya kutosha vya madarasa ya awali.
Mh. Majaliwa amesema wanafunzi wa shule za awali sio walundikwe tu madarasani au wawe wa kucheza tu kipindi chote wawapo shuleni, hapana, ihakikishwe wanasoma kikamilifu ili wakianza darasa la kwanza katika shule za msingi, wawe wameiva barabara.

NDALICHAKO AISHUTUMU CLOUDS FM WAMECHANGIA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE


Joyce Ndalichako adai
Clouds FM imechangia
yaliyotokea Kidato cha
Nne!
- Adai walimpa 'Promo'
kijana aliendika matusi na
"Bongo Flavor" katika
mtihani wake wa Kidato
cha Nne Mwaka jana kwa
kumfanyia interview katika
moja ya vipindi vyake.
- Adai kuwa hatua hiyo ya
Clouds FM imechangia
uandikaji wa matusi kwa
watahaniwa wa mwaka
huu

Albino wapendekeza adhabu ya kifo kwa wanaowauwa

 Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) “Tanzania Albino Society” ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo, taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi katika nchi yao kwa amani.



 Mwenyekiti wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.
 Kabla ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni wake.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa kukatwa mkono wake wa kushoto. 

 Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo mikononi mwa polisi.
NA HAMZA TEMBA – OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
………………………………………………………………………………………………………………………………………

Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania “Tanzania Albino Society” (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.

Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.

Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. “Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.

Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.

Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.

Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri

Mtoto wa miaka 6 afariki nchini Uganda kwa kukosa hewa baada ya mama wa kambo kufungia watoto ndani na kuchoma moto nyumba.


Baba wa watoto hao Kanakulya akiwa na mmoja wa watoto zake aliyeokolewa katika janga hilo.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug)
Mtoto asiye na hatia amefariki dunia baada ya mama yake wa kambo kumfungia ndani ya nyumba pamoja na ndugu zake watatu wakiwa wamelala kisha akachoma nyumba moto.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku katika kijiji cha Namuyenje kilichopo katika wilaya ya Mukono.
Mtoto huyo Shafik Jjuuko mwenye umri wa miaka 6 alifariki kwa kukosa hewa wakati mama yake wa kambo Margaret Nampiima mwenye umri wa miaka 27 alipochoma moto nyumba waliokuwemo watoto hao huku baba yao ambaye ni dereva akiwa safarini.
Watoto wengine Sulaiman Mutebi 8, Shamim Nakimera, 9 na Hassan Geserwa ,11 waliokolewa wakiwa na majeraha yaliyosababishwa na moto huo ambao pia umeteketeza mali kadhaa.

Pinda afungua kiwanda cha kusindika mbegu za Pamba.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa  cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti  na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Morgan Nzwele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mbegu za pamba wakati alipofungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...