Monday, July 13, 2015

NEC YATANGAZA MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo mapya.

Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.

Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba, Vwawa, Monongo, Mlimba, Pamoja na Uliambulu.

Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.

Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 13, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

POLISI WANNE WAUAWA KATIKA SHAMBULIO

Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo
Maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania.

Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam. Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.

Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Kwa mujibu na raia wanoishi karibu na kituo hicho,makabiliano ya risasi yalidumu kwa zaidi ya saa moja.
Uchunguzi unaendelea kujua nani aliyetekeleza shambulizi hilo
Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo akisema askari 4 na raia 3 wameaga dunia. Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.

Aidha amesema kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

KAMBI YA JESHI YAPOROMOKA YAUA 23

Takriban wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka.

Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka kwa vifusi vya jengo hilo.
Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali hiyo.

Picha za televisheni zilionyesha sehemu ya jengo hilo la ghorofa nne likiwa limeharibika kabisa huku wanajeshi wakishirikiana kuondosha vifusi.

Mwandishi wa BBC Moscow amesema inadhaniwa kwamba ukarabati duni uliofanyika mwaka jana ndio uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

MAN CITY YAKUBALI KUMUUZA STERLING KWA LIVERPOOL


Raheem Sterling
Klabu ya Manchester City ya Uingereza imekubaliana na wapinzani wao Liverpool dau la pauni milioni £49 kumsajili mshambulizi Raheem Sterling.
Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya. Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.

Mshambulizi huyo atakuwa mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.
Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika mwaka wa 2017. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

VAN PERSIE ATUA UTURUKI


Van Persie akipokelewa Uturuki
Mashabiki wa manchester United wengi walijua kuwa Van Persie anaondoka kuelekea Fenabashe lakini kwa mtoto mdogo mwingereza wa miaka minne Louis Diamond hakufahamu kuwa kipenzi chake Robin Van Persie anaondoka mpaka pale alipoambiwa na wazazi wake kwamba mpachika magoli Robin alikuwa tayari kuelekea uturuki. 

Hivi sasa waturuki wameanzisha kampeni ya kuchangishana pesa ili mtoto huyo ambaye video yake imesambaa mitandaoni na kutizamwa na watu wengi aletwe Uturuki kumshuhudia mchezaji huyo. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...