Thursday, May 22, 2014

UNYAMA: MTOTO AFICHWA KWENYE BOKSI NA KUFUNGIWA NDANI KWA MIAKA MINNE...!!!


Rashid Mvungi  akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa. Picha na Hamida Shariff 

Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai mwaka jana.

Morogoro. Mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro juzi alishushiwa kipigo na wananchi kutokana na kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne.

Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya majirani zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa. Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.

Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 22, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NGASSA, SAMATTA KUGOMBEA TUZO MOJA

 Mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa pamoja na Mbwana Samatta wa TP Mazembe, wanaumana katika kuwania tuzo za mwanamichezo anayependwa zaidi na watu zinazoendeshwa na Kampuni ya Bongo 5 Media Group kupitia tovuti yake ya bongo5.com.
Wengine wanaowania tuzo katika kipengele hicho ni Ramadhan Singano (Simba SC), Juma Kaseja (Yanga) na bondia Francis Cheka.
Inaonekana kuwa Ngasa na Samatta watakuwa na ushindani mkubwa zaidi hasa ikizingatiwa kuwa wachezaji wote wana mashabiki wengi na pia kila mmoja anacheza mchezo unaopendwa na wengi.
Akizungumzia tuzo hizo, mhariri mkuu wa bongo5.com, Fredrick Bundala, alisema watu wengi walijitokeza kupigia kura kuchagua watu wanawataka kushinda tuzo mbalimbali.
Bundala alivitaja vipengele vingine na majina ya waliopendekezwa kuwa ni pamoja na Nisher, Adam Juma, Nick Dizzo, Mecky Kaloka, Jerry Mushala wanaowania tuzo ya Mwongozaji Bora wa Video za wasanii.
Video Bora kwa Wanaume ni My Number ya Diamond, Jikubali ya Ben Pol, Mirror ya Baby, Love Me ya Izzo Bizness, Barnaba na Shaa, Muziki Gani ya Nay wa Mitego na Diamond.
Alisema wanaowania Tuzo ya Video ya Mwanamuziki wa Kike ni Amani ya Moyo ya Feza Kessy, Closer ya Vanessa Mdee, Sugua Gaga ya Shaa, Yahaya ya Lady Jaydee, Nakomaa na Jiji ya Shilole.
Bundala alifafanua kuwa wananchi wanatakiwa kuchagua jina moja kutoka katika majina matano ya kila kipengele kilichotajwa.
“Wiki moja baada ya majina ya washiriki watano kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele,” alisema Bundala.
Aliwataka Watanzania kuwapigia kura wale wanaowapenda kwa kutuma ujumbe mfupi na baadaye kufuata maelekezo rahisi ya kupiga kura pia kupitia tovuti www.tuzozetu.com. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

YAYA AITIA KIWEWE MANCHESTER CITY

Yaya Toure amekoleza moto kwenye sakata lake kutaka kuihama Manchester City akisema hajui hadi sasa atakapokwenda kucheza msimu ujao.
Wakala wa mchezaji huyo, Dimitri Seluk alibainisha kuwa Yaya anaweza kuondoka kwa sababu anadhani kwamba amekuwa akichukuliwa kama mtu asiyeheshimika na wamiliki wa klabu hiyo.
Hivyo kwa sasa, Toure ambaye ana miaka 31, hajaamua hatima yake kuhusu klabu atakayochezea msimu ujao.
Alipoulizwa kama anaweza kuichezea klabu nyingine msimu ujao, alijibu: “Ndio. Hatujui katika soka nini kitatokea. Kamwe hatuwezi kujua hilo.”
Katika mahojiano maalumu na mtandao wa BE IN SPORTS, nyota huyo wa timu ya taifa ya Ivory Coast alisema: “Kwa sababu ya msimu mzuri niliokuwanao klabu ya Man City, kila mtu ananizungumzia na kila kitu kiko wazi.
“Wakala wangu Dimitri, siku zote amekuwa akizungumza na watu kwa simu na anajua cha kufanya kwa sababu siku zote nimekuwa nikimuamini sana.
“Hatujui kesho itakuwaje, lakini kwa sasa akili yangu iko katika Kombe la Dunia na baada ya kumalizika kwake tutajua nini kimetokea.”
Toure alisaini mkataba mpya wa miaka minne kuichezezea City Aprili mwaka jana.
Hata hivyo, majaaliwa yake yamebaki kuwa na mashaka kutokana na wakala wake kuwalaumu wamiliki wa City kwa kutoonyesha heshima kwa kiungo huyo alipotimiza miaka 31. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WAZIRI AJIUA BAADA YA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI

Shughuli ya kuhesabu Kura Malawi
Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...