Sunday, June 23, 2013

The Finest : FA apata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee.

Mwanamuziki Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake kuna jina la Jay Dee.
 
Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.

Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.

Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
Saa nne kamili mwanamuziki Hamis Mwinjuma, Mwana FA alikanyaga ‘red carpet’ akiwa na mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi, na baada ya kuchukuliwa picha kadhaa alianza kuelekea nje ya ukumbi sehemu waliyosimama watu wakipata chakula na vinywaji, watu walizidi kufurika lakini kila aliyeingia alikuwa alwatan kidogo.

Waliendelea kuwasili mastaa na shoo inaanza Mashabiki wanaanza kuingia ukumbini saa tano kamili baada ya kupata vyakula na vinywaji nje, huku muziki wa taratibu ukipigwa na bendi ya muziki wa dansi ya Njenje. Mashabiki wanaendelea kubadilishana mawazo mpaka inapotimu saa tano na robo usiku, ambapo Mwana FA anapanda jukwaani.

Anaanza kazi kwa shoo ya aina yake baada ya kuimba hip hop live akiwa na bendi ya muziki wa dansi, kwenye shoo hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
FA alipanda jukwaani na wimbo wa Binamu akisindikizwa na wanamuziki Mandojo na Domokaya waliovalia suruali nyeusi na mashati meupe huku wakiwa wamevalia mikanda aina ya ‘suspender’, baadaye aliimba wimbo Unanijua Unaniskia na Bado Niponipo Kwanza ambao uliwapendeza mashabiki.

Alisimamisha shoo kwa muda na msanii Bernald Paul maarufu kama Benpol alipanda jukwaani na kuimba nyimbo zake tatu kwa kuziunganisha ukiwamo wa Maneno, Pete na Nikikupata na baadaye aliimba na Mwana FA wimbo wa Asubuhi aliomshirikisha Q Chief.
FA alipanda jukwaani na wanamuziki kadhaa katika vipindi tofauti akiwamo Linah Sanga ‘Linah’, Maua, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’.
Baadhi ya nyimbo alizoimba ni pamoja na Kama Zamani, Alikufa kwa Ngoma, Habari Ndio Hiyo, Leo, Mabinti, Unanitega, Yalaiti na nyingine nyingi.

HII NDIO HALI YA MSANII BARNABAS TANGU KUPOKEA TAARIFA ZA MSIBA WA MAMA YAKE



Kiukweli inasikitisha sana tangu asubuhi hajatia kitu chochote tumboni analia ananyamaza,akipewa chakula hakitaki.mungu mjalie ndugu yetu mpe nguvu aweze kumzika mama yake kwa aman na upendo.







R.i.P mamaa BARNABAS, Maziko ni leo saa 10 katika makaburi ya mburahati,kuanzia asubuhi saa 5 tutakuwa na misa maalum kwa ajili ya marehemu mama barnabas.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 23, 2013

DSC 0019 578e1

DSC 0022 d20cc
DSC 0023 43257

ASKOFU AITAKA SERIKALI KUWABANA WASIOTAKA NCHI ITAWALIKE.

RAIS Jakaya Kiwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na dini wakati alipohudhuria sherehe za miaka 25 ya Askofu wa jimbo kuu la Morogoro Telesphol Mkude wa pili kulia kwa rais katika viwanja vya shule ya ST Peter mkoani Morogoro jana.


SIKU chache baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka Serikali iachwe ifanye kazi yake katika kudhibiti vurugu zinazoibuka kila kukicha, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude naye ameitaka Serikali kuwadhibiti wote wasiotaka nchi itawalike.Askofu huyo amesema kuonya pekee hakusaidii, bali inawajibu wa kuwachukulia hatua kali ili kukomesha vitendo vinavyotishia amani nchini.Askofu Mkude aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye viwanja vya Seminari ya Mtakatifu Petro mjini hapa ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria.

RIHANNA AMPIGA SHABIKI WAKE NA KIPAZA SAUTA BAADA YA SHABAKI HUYO KUMKERA...!!!


MWIMBAJI nyota wa muziki wa R&B, Robyn Rihanna Fenty, anayefahamika zaidi kwa jina  la Rihanna, amenaswa na kamera akimpiga shabiki ‘mic’ usoni alipokuwa akifanya shoo huko Birmingham, Uingereza Jumatatu iliyopita.

Rihanna alifanya tukio hilo la kushtua alipojichanganya kwenye umati wa mashabiki, huku akiimba kwenye shoo hiyo ambayo ni sehemu ya ziara yake ya dunia inayojulikana kama ‘Diamond World Tour’ akiitangaza albamu yake ya saba ya ‘Unapologetic’ iliyotoka mwaka jana.

Ilidaiwa kuwa Rihanna mwenye umri wa miaka 25 alishindwa kudhibiti hasira zake baada ya shabiki huyo asiyefahamika kumng’ang’ania mkono wake.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliandika kwenye ukurusa wake wa Twitter: "Rihanna amempiga mtu mmoja na mic yake katika ajali haha oops."

Na Rihanna alijibu akisema kuwa alikusudia kumpiga shabiki huyo kwa sababu alikuwa akimzuia.

TAMASHA LA KILI MUSIC AWARDS NDANI YA UWANJA WA JAMHURI DODOMA.....OMMY DIMPOZ APIGWA CHUPA NA MASHABIKI JUKWAANI..!!

Ommy dimpoz arushiwa chupa na mawe jukwaaani dodoma na kushindwa kufanya show ya kilimanjaro muzik award dodoma. Wadau wa dom wasema kamwe msanii yoyote atakaye mdisi msanii wa dodoma awatamkubari kufanya show dom na watamshusha jukwaani kama walivyo fanya leo

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.




 Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.

 

POLISI 7 WAFUNGWA JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA MAUAJI HUKO KIGOMA

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela askari saba wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambao walikuwa wakishtakiwa kwa mauaji.

Akitoa hukumu yake katika kikao cha Mahakama Kuu kilichokuwa kikifanyika mkoani Kigoma Jaji wa mahakama hiyo, Sam Mpaya Rumanyika alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi mbalimbali Mahakama hiyo imewatia hatiani askari hao kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012 washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kumuua Festo Stephano, mkulima wa kijiji cha Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu mkoani hapa katika tukio lililotokea Agosti 6, mwaka 2011.

Askari hao waliohukumiwa ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo Swahib, D/C Charles, D/C Shamsi, D/C Jerry na D/C Amrani ambao kwa pamoja walikana shitaka lao katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012.
Akitoa utetezi kabla ya hukumu hiyo wakili wa washitakiwa, Method Kabuguzi aliiomba Mahakama kuwafutia shitaka washitakiwa hao na kuwaachia huru kwani wote bado vijana na wameoa hivi karibuni.
Sambamba na hilo Kabuguzi alisema kuwa askari hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakitekeleza jukumu lao la ulinzi wa taifa ambapo walimkamata mtuhumiwa wa kutumia silaha na ndipo kifo kikatokea wakati wakitekeleza majukumu yao.

Source: http://www.wavuti.com

AMANDA APIMA NGOMA, PRESHA YAPANDA YASHUKA

Stori:Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta akipandwa na kushukwa na presha  mara baada ya kwenda hospitali kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi.Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni, jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari, alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha ikampanda baadaye ikashuka.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Amanda na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo bila hiyana alitiririka:
“Ile ilikuwa ni mara ya tatu kupima ngoma yaani wakati nikisubiri majibu, presha ilipanda ghafla mpaka daktari akawa na wakati mgumu wa kunipa majibu.



“Nilienda kuchukua majibu na sikutaka kuyaangalia, nilimpelekea daktari ambaye aliniambia niko safi yaani sikuamini nilitoka nikiwa naongea peke yangu, nilikuwa sijiamini si unajua tena ujana ni maji ya moto sasa presha ,” alisema Amanda.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...