Tuesday, November 04, 2014

UNAFAHAMU MADHARA YA KUFANYA KAZI USIKU...???


kufanya kazi usiku huathiri uwezo wa akili kufanya kazi haraka
Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la Occupational and Environmental Medicine kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.
Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo wamekuwa wakilala usingizi wa mang'amung'amu.
Moja ya madhara yatokanayo na kufanya kazi usiku ni kuongezeka uzito kupita kiasi
Wataalam hawa wameiambia BBC kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya Saratani na uzito mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara ya kiakili pia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...