Wednesday, February 26, 2014

HIKI NDICHO KINACHOENDELEA MSIBANI KWA DADA YAKE LADY JAY DEE...!!!

Msanii mkongwa wa Bongo Flava Lady Jay Dee amefiwa na dada yake Aitwaye Lucy Lameck Isambwa Mbibo
Lady Jay Dee Ameshare Taarifa Hizo za msiba wa dada yake kupitia mitandao yake ya kijamii

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

SERIKALI YATANGAZA TAREHE YA USAILI KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI ZA KILIMO NA MIFUGO

Serikali inapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi kwa tangazo la tarehe 27 Novemba, 2013 wa kada za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Udereva kuwa usaili utaanza tarehe 4 Machi, 2014 takriban katika mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea kwa lengo la kufahamu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini.
Amesema usaili huo unaoanza tarehe 4 Machi katika mikoa takribani yote nchini utahusisha jumla ya wasailiwa 6,087 wa fani za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na udereva kwa kada ambazo sio za Maofisa. Amefafanua kuwa vigezo vya kupanga mikoa ya usaili vimetokana na anwani ambazo waombaji waliwasilisha katika barua zao za maombi husika ya kazi.
Daudi alibainisha kuwa kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa kama anwani yake inavyoonyesha katika tangazo kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, isipokuwa kwa waombaji wa mkoa wa Katavi wao wataenda kufanyia usaili mkoa wa Rukwa na waombaji waliotumia anwani za mkoa wa Singida wao watafanyia usaili mkoa wa Manyara kutokana na sababu zisizozuilika.
Aliongeza kuwa kwa mwombaji ambae hatazingatia anwani, siku na muda aliopangiwa na kuamua kwenda mkoa mwingine tofauti na utaratibu uliopangwa ajue wazi hatasailiwa kwa kuwa ratiba na idadi ya majopo ilishapangwa kwa kila mkoa na haitabadilishwa ili kuweza kurahisisha kazi hiyo kukamilika  kwa ufanisi.

ANGAALIA PICHA ZA MECHI YA JANA KATI YA OLYMPIACOS NA MAN UTD WALIOCHAPWA 2 BILA MAJIBU

Celebration: Alejandro Dominguez (centre) wheels away after scoring the opener in Greece
Celebration: Alejandro Dominguez (centre) wheels away after scoring the opener in Greece
Arrival: Joel Campbell slides on his knees in celebration of his goal just after half-time
Arrival: Joel Campbell slides on his knees in celebration of his goal just after half-time
Outstretched: David De Gea is well beaten by Campbell's shot in the 55th minute to deflate United
Outstretched: David De Gea is well beaten by Campbell's shot in the 55th minute to deflate United
Flat out: Robin van Persie lies on the floor after missing United's best chance of the game late on
Flat out: Robin van Persie lies on the floor after missing United's best chance of the game late on. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

PBF_8384-w480-h580
PBF_8385-w480-h580 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI...!!!

daktari_553f2.jpg
Askari akimwongoza mtuhumiwa Mustafa Kitano, anayedaiwa kutoa huduma za utabibu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinyume na utaratibu,Picha na Michael Jamson
Dar es Salaam. Maofisa Usalama wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamemkamata mtu anayedaiwa kutoa huduma kwa wagonjwa kinyume cha utaratiba na kwamba, amekuwa akiwatapeli wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminieli Eligaesha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mustafa Kitano na kwamba, amekuwa akitumia majina ya Dk Nyirabu na Koba, alikamatwa wakati akimsaidia mgonjwa mmoja.
Eligeisha alisema Februari 22 mwaka huu walipata taarifa kutoka kwa Hussein Haji kuwa, kuna daktari anaitwa Koba alitaka kumtapeli Sh200,000 ili amtafutie kazi ya udereva kwenye tawi la MNH lililopo Kahama Shinyanga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

OPERESHENI DHIDI YA WAASI WA UGANDA ADF

UGANDA_98bb6.jpg
Waasi wa Uganda ADF.
Operesheni zinaendelea katika wilaya ya Beni, jeshi la serikali limetangaza kuwa, operesheni hizo, zimelipelekea jeshi hilo kuyakomboa maeneo kadhaa, toka mikononi mwa waasi.
Operesheni dhidi ya waasi wa Uganda ADF wanaojihifadhi katika misitu
ya wilaya ya Beni mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiwa zinaendelea,huku wanajeshi wakiwa wamepelekwa katika eneo hilo, raia wa mji na wilaya za Beni wameanza kulalamikia usalama wao,kutokana na jinsi wanavyo nyanyaswa na wanajeshi wa serikali. Ili kukomesha vitendo vya unyanyasi wa raia, jeshi la Congo limelivalia njuga suala hilo.
Mwandishi wetu John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Beni. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo, dw.de.com/swahili.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...