Sunday, June 09, 2013

AKAMATWA KWA KUIBA STULI YA MWENGE WA UHURU...!!!

 

JIJI la Arusha limeendelea kujijengea sifa ya kuwa moja ya maeneo yenye vituko, kufuatia kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips, kata ya Sekei jijini humo, Hamad Rashid (32) kukamatwa leo akiiba kiti (stuli) kinachotumika kuwekea mwenge wa Uhuru wakati mwenge ukiwa katika mbio zake mkoani Arusha.
Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwaajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kamanda wa polisi mkoa wa  Arusha Liberatus Sabas ameithibitishia Nkoromo Blog kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.

SALAMA JABIR ATAMANI KUOLEWA NA A.Y.....!!!

  

Mtangazaji mahili wa show za TV/Radio aliyeisimamisha wima show mpya na kali inayorushwa kupitia channel 5 ‘Mkasi’ namzungumzia Salama Jabir ametupia ‘neno’ kupitia kipindi hicho kuwa huenda siku moja akaolewa na AY!

Kama uliiangalia show ya Mkasi jumatatu ama marudio yake leo (jumamosi) ambapo crew nzima ya kipindi cha mkasi chini ya C.E.O na Producer wa show Ambwene Yesaya ‘AY’ walikuwa wakieleza changamoto na mambo mbalimbali waliyokutana nayo wakati wanaanza kufanya kipindi hicho, mwishoni Salama ambae alikuwa akimuelezea AY kuwa ni msanii ambae anajivunia kufanya nae kazi kutokana na jinsi alivyomchapakazi na mtu wa kuaminika alimaliza kwa kusema “huenda ipo siku moja tutaona..!”.

Wote tunajua Salama  alivyo mtu wa utani sana, kitu kinachoongeza burudani ya ziada katika show zake, alitamka hivyo na kumgeukia AY akimuuliza, na AY mwenyewe akajikuta anacheka na kukubali.
Pengine ulikuwa ni utani tu, lakini hakuna aijuae kesho ukizingatia wote wako single!

"MNAOWANIA URAIS MSIKUBALI KUPOKEA PESA ZA HUYU MFANYABIASHARA FISADI AMBAYE NI KINARA WA MADAWA YA KULEVYA".... REGINALD MENGI


Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi ametoa ya moyoni kwa wote wenye mpango wa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka miwili ijayo.

Bwana Mengi ameyatoa maombi yake ya moyoni na kuyaweka hadharani kupitia akaunti yake ya twitter June 7, na hiki ndicho alichokiandika.

“Nawaombea Mungu wanaotaka Urais wasipokee mshiko wa mfanyabiashara fisadi mkubwa ambaye pia ni kinara wa madawa ya kulevya.”

Swali ni mfanyabiashara gani, hilo linaweza kuwa ni jiwe gizani kama yupo kweli aliyetajwa litakuwa limemfikia. 
Na  kama  kuna  msomaji  wetu  anayemjua, ANARUHUSIWA  KUMTAJA  kwenye  COMMENTS  hapo  chini

WASHINDI WA TUZO ZA MUZIKI ZA KILI ( KILIMANJARO ) 2013


KALA JEREMIAH, OMMY DIMPOZ  WATISHA KWA KUZOA TUZO TATU 

* CHALZ BABA,  , OMMY DIMPOZ  WAZOA TUZO MBILI MBILI

NEY WA MITEGO ABEBA TUZO NDANI YA SIKU YAKE YA KUZALIWA

*OMMY DIMPOZ AMSHUKURU ZITTO KABWE KWA KUFANIKISHA UTENGENEZAJI WA VIDEO YAKE YA BAADAE

* ZEMBELA ATISHA KWA USHEHERESHAJI

* SALEHE ABDALLAH YAZIPU NA KILIMANJARO BAND WABEBA TUZO ZA HESHIMA
* LADY JAY DEE ABEBA TUZO YA MSANII BORA WA KIKE


MBUNGE WA MTWARA MJINI AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA VURUGU ZA MTWARA

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo kwenda jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Advera Senso zinaeleza kuwa Murji alikamatwa jana jioni nyumbani kwake maeneo ya Shangani mjini Mtwara.

Kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja ikiwa zimepita siku tano tangu viongozi wanne wa vyama vya upinzani mkoani Mtwara, kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Juni 4, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa hao ni Katani Ahmed Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF, Hassan Uledi (35) wa NCCR Mageuzi na Hamza Licheta (51) wa TLP, wote wakazi wa Mtwara.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa baada ya polisi kumkamata mbunge huyo, walifanya upekuzi katika nyumba yake kwa saa kadhaa na baada ya kujiridhisha walikwenda kupekua na ofisi yake.


“Amekamatwa kwenye saa 11:00 jioni, hata hati ya kukamatwa kwake imeeleza kuwa anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi inayopatikana mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam,” alisema Katibu wa Mbunge huyo, Meckland Millanzi.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 9, 2013

2 b911e

3 21fb8

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...