Tuesday, May 27, 2014

BAJETI YA MWAKYEMBE YATIKISA BUNGE, YAPITA...!!!

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/15 bungeni Dodoma, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi      

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana usiku alikuwa katika wakati mgumu wakati Bunge lilipoketi kama Kamati ya Matumizi, kiasi cha kutishia bajeti ya wizara yake kukwama. Hata hivyo, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 yalipitishwa.
Wabunge wa vyama vyote walimbana Dk Mwakyembe na kutoa shilingi karibu katika kila kifungu wakihoji mambo mbalimbali hasa juu ya mgogoro wa umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), usafiri wa majini hususan usalama wa meli ya Mv Victoria.
Sakata la Uda
Sakata hilo la Uda lilisababisha mvutano baina ya Naibu Spika, Job Ndugai na Dk Mwakyembe ambaye alilalamikia mjadala wa Uda kuruhusiwa katika hotuba ya wizara yake. Hata hivyo, Ndugai alipangua hoja hiyo akisema mbali na kwamba Uda inagusa wizara nyingi, lakini ni suala linalohusu uchukuzi hivyo ilikuwa sahihi kujadiliwa katika mjadala huo.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla ndiye aliyeibua suala hilo kwa kuhoji sababu ya Serikali kutoa taarifa zinazokanganya kuhusu Uda, hali kamati anayoiongoza ilishakaa na pande zote husika wakiwamo wataalamu na kuwa na hitimisho kwamba Kampuni ya Simon Group Ltd ni waendeshaji halali wa shirika hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

'OCEAN ROAD WAMENISUSA, NAHAMIA TIBA ZA JADI'


Majengo ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba.

Mgonjwa wa saratani ya titi aliyepewa dawa feki za mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) amejikuta katika wakati mgumu baada ya wahudumu wa hospitali hiyo ya Serikali kumtelekeza alipokwenda kupata tiba.

Mgonjwa huyo, Pendo Shoo ambaye anahofu kwamba saratani imempata katika titi lake la pili, anasema hatakwenda tena katika hospitali hiyo na badala yake ameamua kusaka tiba kwa waganga wa tiba asilia.

Hivi karibuni gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mtumishi wa OCRI, Almasi Matola alivyomtibu Pendo kwa dawa feki baada ya kumtoza kiasi cha Sh1.34 milioni kinyume na taratibu za tiba katika hospitali hiyo.

Almasi akizungumza na gazeti hili wiki mbili zilizopita, alikiri kuwekewa fedha katika akaunti yake ambazo ni zaidi ya Sh300,000, lakini akakanusha kwamba fedha hizo ni kama ujira wa kumpa mgonjwa huyo dawa.

Kwa mujibu wa taratibu za OCRI, wagonjwa wanaokwenda hospitali hapo kwa rufaa kutoka hospitali nyingine hawapaswi kutozwa fedha zozote kwa ajili ya matibabu. Pendo alipata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba mwaka jana.

Alibaini kuwa alipewa dawa feki baada ya kutokupata nafuu yoyote wiki kadhaa tangu alipoanza kupewa tiba na baada ya kuripoti tukio hilo kwa madaktari walimwanzishia upya tiba husika. Wiki moja tu baada ya kuchapishwa habari hizo, mgonjwa huyo alifika OCRI kuendelea na matibabu lakini alijikuta katika mazingira magumu kiasi cha kuondoka bila kupewa huduma. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NI TIMU NANE TU ZIMETWAA KOMBE LA DUNIA

Vijana wa Brazil  

London, England. Kwa kipindin cha miaka 83, fainali za Kombe la Dunia zimefanyika mara 19, lakini hadi sasa ni timu nane tu ambazo zimeshatwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.
Fainali hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1930 nchini Uruguay na zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka minne, isipokuwa mwaka 1942 na 1946 kutokana na Vita Kuu ya dunia .
Brazil inaongoza kwa kutwaa Kombe la Dunia baada ya kutwaa taji hilo mara tano. Brazil ilitwaa taji hilo nchini Sweden mwaka 1958, nchini Chile (1962), Mexico (1970), Marekani (1994) na Korea/Japan (2002). Brazil pia ndiyo nchi pekee iliyoshiriki fainali zote za Kombe la Dunia tangu zilipoanzishwa mwaka 1930 na imefunga jumla ya 210 katika fainali 19.
Italia imetwaa ubingwa huo mara nne. Ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ilipoandaa mwaka 1934, baadaye nchini Ufaransa (1938), Hispania (1982) na Ujerumani (2006). Italia imeshiriki fainali hizo mara 17 na kufunga mabao 126. Kati ya 1950 na 1990, Ujerumani Magharibi (sasa Ujerumani) ilitwaa ubingwa mara tatu. Ilitwaa ubingwa nchini Uswisi 1954, na baadaye ilipoandaa fainali hizo mwaka 1974 na nchini Italia (1990). Kati ya 1930 mpaka 2010 Ujerumani imeshiriki fainali hizo mara 17 na imefunga mabao 206.
Mwaka 1978, Argentina ilikuwa ni taifa la tano kutwaa ubingwa wa dunia. Ilitwaa tena ubingwa wa dunia mwaka 1986. Tangu 1930 mpaka 2010, Argentina imeshiriki fainali hizo mara 15 na kufunga mabao 123.
Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kutwaa kombe hilo wakati ilipoandaa fainali hizo 1930. ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pilimwaka 1950 nchini Brazil. Uruguay imeshiriki Fainali za Kombe la Dunia mara 13 na kufunga mabao 76. Ufaransa imetwaa ubingwa wa dunia mara moja mwaka 1998 walipokuwa wenyeji. Ufaransa imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 13.
Pamoja na utajiri wa vipaji na kuwa na klabu bora, Hispania ilisubiri hadi mwaka 2010 kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza na ndio mabingwa watetezi. Hispania imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 88.England iliandaa na kutwaa ubingwa mwaka 1966. Imeshiriki mara 13 na kufunga mabao 77. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 27, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

JESHI NIGERIA 'TUNAJUA WALIPO WASICHANA'

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linajua wanakozuiliwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara majuma sita yaliyopita lakini likasema haliwezi kutumia nguvu kuwakomboa.
Afisa wa cheo cha juu jeshini - Mkuu wa Jeshi Alex Badeh - aliwambia waandamanaji jijini Abuja kuwa hangeweza kufichua waliko wasichana hao lakini akaahidi kuwa wanajeshi watawarejesha nyumbani wasichana hao.
"Habari nzuri kwa wasichana ni kuwa tunafahamu waliko lakini hatuwezi kuwambia. Hatuwezi kuja na kuwambia siri za kijeshi hapa," mkuu wa wanahewa Alex Badeh aliwambia waandamanaji jijini Abuja.
Alisema anaamini kuwa watawarudisha wasichana hao nyumbani hivi karibuni lakini akaeleza masikitiko yake kwa kile alichosema watu kutoka nje ya nchi wanaochochea ghasia na maandamano.
Bwana Badeh alisisitiza kuw kutumia nguvu kujaribu kuwakomboa wasichana hao ni hatari.
"Wapiganaji hawa wanataka kupigana na kwa hivyo wasichana watakuwa hatarini ikiwa kutatokea mkabiliano makali kati ya wapiganaji hao na jeshi la Nigeria," Alex Badeh alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

MISRI WAMCHAGUA RAIS MPYA

Mabango yanayotangaza uwaniaji wa aliyekuwa Mkuu wa jeshi la Misri, Abdel Fatah al-Sisi, kama Rais
Raia wa Misri wanapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama.
Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .
Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.
Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Chanzo: BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...