Sunday, February 16, 2014

KIKWETE AWATAKA WANA-CCM KUACHA UNYONGE...!!! ASEMA UNYONGE UNA KIKOMO...!!!


03_ecd2e.jpg
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge na kusema uvumilivu una kikomo chake.
Aliyasema hayo jana wakati anafungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, kilicholenga kuweka msimamo wa chama kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ambayo inaanza kujadiliwa Jumanne wiki ijayo.
"Tuna uchaguzi mdogo, Iringa, Kalenga, tumeshapata mgombea na tumefanya hiyo kazi kwa niaba yenu kwa sababu hatukupata muda wa kuitisha Kikao cha Halmashauri Kuu, lakini mmetupatia mamlaka ya kufanya hivyo na Katiba imetupa fursa ya kufanya uteuzi kwa niaba yenu,"alisema.
CCM imemteua Godfrey Mgimwa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Dk William Mgimwa, kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu. Dk Mgimwa hadi anafariki dunia alikuwa Waziri wa Fedha.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na Chadema vikiwa vimetaja wagombea wake, Chadema kikiwa kimetangaza, Grace Tendega Mvanda.
Rais Kikwete alisema chama hicho kinashindana na vyama vingine katika uchaguzi huo mdogo.
"Tunashindana na wenzetu wagomvi, maana wao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa,"alisema Kikwete bila kutaja chama chochote cha siasa kwa jina.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

UMECHOKA KUAJIRIWA UNATAKA KUJIAJIRI?! HAYA HAPA MAMBO 8 MUHIMU YA KUZINGATIA


Kuna sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo.  
Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.
Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.
 
Mkakati ni muhimu: Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto. 
Katika kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa, teknolojia, na uchumi. 
Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MECHI KALI ZA LEO NA KESHO ZA KOMBE LA FA


http://jambotz8.blogspot.com/ 
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii itakuwa ‘mapumziko kidogo kupisha Mechi za Raundi ya Tano za FA CUP ambazo zitachezwa Jumapili na Jumatatu.
Jumapili Februari 16
16:30 Everton v Swansea
18:00 Sheff Utd v Nottm Forest
19:00 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Februari 17
2245 Brighton v Hull
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

KESI YA MOHAMMED MOSRI KUSIKILIZWA LEO

Mohammed Morsi akiwa mahakamani
Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi atafika katika mahakama moja mjini Cairo ili kusikiza mashtaka ya upelelezi na njama ya kutaka kutenda ugaidi yanayomkabili.
Bwana Morsi aling'atuliwa mamlakani na jeshi mnamo mwezi Julai na sasa anakabiliwa na mashtaka mengine matatu.
katika kesi hiyo yeye na wanachama wengine 35 wa vunguvu la Muslim Brotherhood wanatuhumiwa kwa kushirikiana na makundi ya kigeni kama vile Hamas,Walinzi wa mapinduzi nchini Iran na Hezbollah kupanga mashambulizi nchini Misri.
Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

KIONGOZI WA DHEHEBU LA SHIA AJIUZULU


Moqtada al-Sadr akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kiongozi wa Dhehebu la Shia nchini Iraq Moqtada al-Sadr ametoa taarifa akitangaza kujiuzulu kwake katika ulingo wa kisiasa.
katika tangazo ambalo halikutarajiwa na wengi na ambalo liliwekwa katika mtandao wake,Bwana Sadr amesema kuwa hatashikilia wadhfa wowote wa serikali wala kuwa na wawakilishi bungeni.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa atazifunga afisi zake zote isipokuwa zile za kutoa misaada pekee.
Bwana Sadr na wanamgambo wake wa Mahdi walipata ushawishi nchini Iraq baada ya uvamizi wa marekani nchini humo mnamo mwaka 2003.
lakini katika miaka ya hivi karibuni amepoteza umaarufu wake kufuatia mzozo kati yake na waziri mkuu nchini humo Nouri al-Maliki.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TANGAZO MUHIMU KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA




BUNGE MAALUM

TAARIFA KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA _______________________________________________

 Kufuatia wito wa Serikali kuwa Wajumbe wote wanaombwa kufika Mjini Dodoma kuanzia tarehe 16 Februari, 2014 katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar wanapenda kuwaarifu Wajumbe wote maandalizi yafuatayo: -


1.0        USAFIRI WA KUFIKA DODOMA 

Wajumbe wote wanatakiwa kujigharamia wenyewe kufika Dodoma kwa vyombo vya usafiri wa umma.  Wajumbe watarejeshewa gharama za usafiri wa kufika Dodoma kutoka maeneo wanayotoka baada ya kuwasilisha stakabadhi za gharama walizotumia kwa usafiri.


2.0        MALAZI

Utaratibu wa malazi umeandaliwa.  Hoteli zilizoteuliwa kwa malazi kwa Wajumbe kuchagua kwa kadri itakavyowapendeza zimeainishwa.  Hoteli hizo ni hizi zifuatazo: 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz   

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 16, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...