Tuesday, April 16, 2013

ANGALIA RIHANA ALIPOFANYA SHEREHE YA UCHI AKIWA BARBADOS SEHEMU ALIYOZALIWA, AIBU....!!





DIAMOND AMTOLEA NJE WEMA NA KUMPAMBANISHA NA PENNY AMREKODI NA KUSAMBAZA CLIP

 
 Clip iliyosambaa inayomuhusisha Wema Diamond na Penny imefika ndani ya blog yako, clip ambayo inaonekana kurecodiwa kwa maksudi na Diamond pale alipopigiwa simu na Wema Sepetu jana usiku. Inasemekana Wema alimpigia simu Diamond usiku, lakini baada ya Diamond kupokea alimtaka kuacha drama na kumsisitizia kuwa sasa hivi anampenda Penny.
maongezi yako hivi 
Diamond: mi sikufanyii drama na wala sitaki drama yoyote, am inlove with penny we unajua hilo right?
Wema: yeah your inlove with Penny and i i ... 
Diamond: sipendi kwasababu sipendezewi kwasababu mwisho wa siku itakuja kutuletea matatizo drama, nakujua kitu kidogo hukawi kukifanya kikubwa mji mzima na nini na nini sitaki.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA UDHIBITI WA HUDUMA ZA KIUCHUMI BARA LA AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa kimataiafa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akiwahutubia.

HUYU NDIYE MBUNGE ALIYEMWAMBIA SUGU 'SIONGEI NA MBWA NAONGEA NA MWENYE MBWA........!!

Mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea huko Dodoma na wabunge wameendelea kujadili bajeti ya ofisi ya waziri Mkuu katika kikao cha 5.
Siku hizi watu wengi wamezoea kusikia malumbano ama vijembe wanavyotoleana
wabunge wetu, licha ya kuwa vinakuwa sehemu ndogo tu na wanaendelea na hoja za kutusaidia watanzania, lakini bunge limekuwa tofauti sana hasa kwa kuzingatia matumizi ya lugha na hata tafsiri ya lugha hizo.

Leo asubuhi mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma Suleiman Nkamia alimwambia mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa “kumbuka siongei na mbwa naongea na mwenye Mbwa”. Sentensi hii ilitamkwa na mbunge huyo baada ya kusikia sauti ya Sugu akijaribu kukataa kile alichokuwa anachangia bila kufuata utaratibu wa kunyoosha mkono ama kumuomba naibu spika, na ndipo alipomuomba kuwa na heshima kwanza kwa kumtaja kwa jina la ‘Sugu'

PENNY: "NIMEMSAMEHE DIAMOND INGAWA ALINISALITI KWA UWOYA....KWA SASA TUMEYAMALIZA"


Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni  staa huyo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.....
 
Magazeti ya udaku nchini yaliandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako  walienda kufanya yao.
DIAMOND3
Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu amezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.

Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha  taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.

“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema Jokate.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE APRIL 16, 2013

.
.
.
.

Kutoa Taarifa za Siri Katika Mawasiliano ya Elektroniki ni Kosa la Jinai.

Jana na leo, Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu, wahusika wa namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo hili ni Kosa la Jinai. Mfano; tamko la Chadema lililotolewa na Ndugu Mabare Marando Mjini Dar es Salaam tarehe 14/04/2013.
Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;
“Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii”. Aidha, “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...