Monday, September 02, 2013

FAMILIA: AFRIKA KUSINI YAKATALIA RIPOTI KIFO CHA NGWEA.....!!!


TAKRIBANI miezi miwili tangu alipofariki dunia mfalme wa freestyle wa Hiphop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ bado familia inalalama kuwa haijapokea ripoti ya kifo cha kijana wao.


Mama mzazi wa Ngwea, Denisia Mangweha (kulia) akiwa na aliyekuwa mchumba wa mwanaye aitwaye Misheily.
Habari za kiuchunguzi kutoka ndani ya familia zimeeleza kuwa ukiachilia mbali cheti cha kifo cha Ngwea walichopewa siku kadhaa baada ya mazishi ya mtoto wao, hawajawahi kuelezwa kwa kina juu ya kile kilichomsababishia mauti au hata mwenendo wa kesi au uchunguzi wa tukio hilo.
Ilidaiwa kuwa mara kadhaa familia hiyo ilikutana katika vikao vya ndani na kukubaliana kulifuatilia suala hilo katika Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar. Huko walikumbana na vizingiti kwa maelezo imekataliwa kutolewa nchini humo.
Ilisemekana kuwa ndugu hao walipokwenda mara ya mwisho ubalozini hapo waliambiwa waandike barua ya kuomba kujua kinachoendelea ikiwa ni pamoja na ishu ya kama kuna kesi katika tukio hilo.


Habari nyingine zilidai kuwa huenda ripoti hiyo ilikwama sehemu au uchunguzi haujakamilika.

GEORGE BUSH ATANGAZA KIFO CHA MANDELA....!!!


Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amejikuta ‘akiingia chaka’ kwa kutangaza ‘kifo’ cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambaye bado yuko hai.
 
Kosa hilo limetokea jana asubuhi (September 1) kwa bahati mbaya baada ya msemaji wa rais huyo wa 41 wa Marekani kujichanganya kwa kutosoma vizuri habari inayomhusu Mandela kupitia Washington Post hivyo kumfanya Bush aandike ujumbe huu,

“Barbara and I mourn the passing of one of the greatest believers in freedom we have had the privilege to know. As President, I watched in wonder as Nelson Mandela had the remarkable capacity to forgive his jailers following 26 years of wrongful imprisonment — setting a powerful example of redemption and grace for us all. 
He was a man of tremendous moral courage, who changed the course of history in his country. Barbara and I had great respect for President Mandela, and send our condolences to his family and countrymen.”

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 2, 2013

DSC 0522 e0f47
DSC 0523 52ecd
DSC 0524 0ca06

NIMEPEWA MAJINA YA WABUNGE WAUZA DAWA ZA KULEVYA: WAMO CCM, CHADEMA

Khamisi_Kigwangala_e74fd.jpg
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Hata hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja. Miongoni mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam.

"Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk. Kingwangallah. 

Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo kwa kuwataja majina vigogo wanaojihusisha na dawa za kulevya na kwamba bado anasubiri kujibiwa. Dk. Kigwangallah amekabidhiwa majina hayo siku chache tu baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), William Lukuvi, kulieleza Bunge kuwa kama serikali itaamua kutaja wanaojihusisha na biashara hiyo hakuna atakayesalimika ndani ya bunge kwa sababu pia wamo wabunge wanaotajwa.

MZEE MANDELA ATOKA HOSPITALI


nelson-mandela ba73e
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95), jana aliondolewa hospitali na kurejeshwa nyumbani ambako ataendelea na matibabu ya maradhi ya mapafu. Hata hivyo, taarifa ya Serikali ya Afrika Kusini imesema uamuzi huo hauna maana kwamba Mandela amepata nafuu kwa vile hali yake bado ni mbaya na wakati mwingine hudorora zaidi.
 

Taarifa hiyo imeongeza timu ya madaktari wa Mandela inaamini ataendelea kupata matibabu katika makazi yake mjini Houghton kwa kiwango sawa na anayopata akiwa hospitalini mjini Pretoria.

Tangazo hilo limekuja siku moja tu baada ya maofisa wa serikali kukanusha ripoti kuwa shujaa huyo wa taifa hilo, alisharuhusiwa.
Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel aliyekuwa amelazwa hospitali tangu Juni 8, mwaka huu anaheshimiwa duniani kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi wa wazungu wachache na kuhubiri upatanisho na maridhiano na jamii za weupe pamoja na kufungwa miaka 27 jela.

"Timu ya madaktari imetuhakikishia kuwa Mandela atapokea matibabu kwa sawa na anachopata hospitalini mjini Pretoria atakapokuwa katika makazi yake ya Houghton," taarifa ya Ofisi ya Rais ilisema.
"Lakini ikibidi, atarejeshwa hospitali," taarifa hiyo ilisema na kuongeza kwamba inamtakia Mandela afya njema.

DAUDI MWANGOSI ATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUUWAWA KWAKE MKOANI IRINGA.


Ndugu zangu,

HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu.

Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa,Daud Mwangosi kuawa.

Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile  itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja  kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi.


Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu,  nilisitisha mazoezi yale ya watoto. Nikawapa taarifa zile.  Nilipowaambia kuwa nimepata taarifa sasa hivi kuwa mwandishi wa habari ameuawa Mafinga, mtoto mmoja akaniangalia na kuniuliza; “ Kwanini?”

Ndiyo, swali la mtoto yule ndilo umma wa Watanzania unapaswa uendelee kujiuliza hata leo; KWA NINI?


Mwandishi wa habari ni mjumbe katika jamii. Anapokuwa akifanya kazi yake hapaswi kuwa na hofu ya kudhuriwa kwa kukusudia na waliopata mafunzo ya  kutumia silaha.  Ndivyo ilivyo kwa watumishi wa Msalaba Mwekundu, wanapokuwa kazini kwenye maeneo hata ya vita.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...