Monday, October 06, 2014

LEMBELI: CCM ILINIHUJUMU UCHAGUZI 2010

Mbunge wa Kahama, James Lembeli akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi.

Mbunge wa Kahama, James Lembeli amemtuhumu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuph Makamba kwamba alikuwa nyuma ya mpango mahususi wa kumhujumu ili akose ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Lembeli, mmoja wa wabunge walio mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi, alisema mpango huo ulitekelezwa kwa kueneza taarifa za kuanzisha jimbo la Ushetu ambalo alitakiwa agombee badala ya Kahama, lakini baadaye msamaria mwema alimpa taarifa kwamba jimbo hilo ni halipo.
Lembeli katika mahojiano yake maalumu na gazeti hili mjini Dodoma alisema alipewa taarifa hizo saa chache kabla ya muda wa mwisho wa kurudisha fomu za kugombea ubunge na kwamba tukio hilo lilimfanya afute fomu yake ya kugombea mara mbili.
“Ulikuwa ni uhuni na ufisadi wa hali ya juu kisiasa,” alisema mwanahabari huyo wa zamani katika mahojiano hayo maalumu yaliyofanyika mjini Dodoma mapema wiki iliyopita. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POLISI WACHANA BANGO LA WALIMU LINALOHOJI POSHO YA BUNGE MAALUMU


Wafanyakazi wakiwa na bango wakiingia kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam palipofanyia maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, jana.

Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, jana yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.

Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu.

Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi usawa uko wapi, posho ya mjumbe wa Bunge la Katiba kwa siku shilingi laki tatu, mshahara wa mwalimu shilingi 370 kwa mwezi. No big results without big salary (Hakuna matokeo makubwa bila mshahara mkubwa)”.

Ujumbe huo ulikuwa ukifanya rejea ya viwango vya malipo ya Sh300,000 kwa siku ambazo walikuwa wakilipwa wajumbe wa Bunge Maalumu zikiwa ni Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS KENYATTA TAYARI KWENDA ICC

Rais Kenyatta anasema anajiamini na kwamba anajua hana hatia katika tuhuma zinazomkabili
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.
Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.
Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.
Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.
Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.
Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.
Takriban wabunge miamoja wanajiandaa kuambatana na Kenyatta Hague katika ishara yao ya kumuunga mkono. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JESHI LA SOMALIA NA AU WADHIBITI BARAWE

Wanajeshi wa Somalia
Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na vikosi vya Muungano wa Afrika kwa sasa wamechukua udhibiti wa mji wa Barawe ambayo ni ngome ya mwisho ya wanamgambo wa al-Shabab.
Wanajeshi hao waliingia mji wa Barawe ulio kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumatatu baada ya kuuzingira tangu siku ya Jumapili.
Sauti za risasi zilisikika mapema Jumatau wakati wanajeshi walikuwa wakiingia mji huo. Ripoti zinasema kuwa kwa sasa mji huo umetulia na magari ya kijeshi kwa sasa yanapiga doria.
Mji wa Barawe haujakuwa chini ya serikali kwa miaka 23 na umekuwa chini ya udhibiti wa al Shabab kwa miaka sita iliyopita.
Gavana na maafisa wa kijeshi waliwahutubia wenyeji leo ambapo walitoa wito wa kuwepo kwa utulivu wakisema kuwa nyakati za al-Shabab zimekwisha.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay alipongeza jeshi hilo la pamoja na kusema kuwa sasa Somalia ina mazuri siku za usoni.
Kutwaliwa kwa mji huo ni pigo kwa kundi la al-Shabab lililo na uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.
Al Shabab wamekuwa wakiutumia mji huo kupitisha silaha na chakula na pia kama kituo cha biashara ya makaa.
Muungano wa Afrika pia unasema kuwa al-Shabab waliutumia mji wa Barawe kupanga mashambulizi yao dhidi ya mji mkuu Mogadishu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

JULES BIANCHI APATA AJALI

Jules Bianchi
Katika Mashindano ya mbio za magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules Bianchi, yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika mashindano ya Japan Grand Prix. Madaktari wa upasuaji wanaendelea kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu wakati alipofikishwa hospitalini hapo.Bianchi alipoteza uelekeo wa gari lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa.Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton alitangazwa mshindi katika mashindano hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA INAVYOSHINDA BILA WASHAMBULIAJI KUFUNGA MABAO

IMG_2927
Yanga SC ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro baada ya kulala kwa mabao 2-0, lakini timu hiyo imemudu kupandisha kiwango chake cha kujituma, umakini na nidhamu na kufunga mabao manne katika michezo miwili iliyopita ukiwemo ushindi wa siku ya Jumapili dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu katika ligi kuu baada ya kuichapa, Tanzania Prisons ya Mbeya kwa mabao 2-1 wiki moja iliyopita, na jana wakaifunga JKT Ruvu inayofundishwa na mchezaji/kocha wao wa zamani Fred Minziro kwa ushindi kama.
Michezo yote hiyo ilifanyika katika uwanja wa Taifa hivyo kufanya mabingwa hao wa zamani kusogea hadi katika nafasi ya Tatu nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja, na pointi Tatu nyuma ya vinara Mtibwa ambao walishinda kwa mara ya Tatu msimu huu katika uwanja wa nyumbani. Mtibwa imekusanya pointi tisa baada ya kuzishinda Yanga, Ndanda FC na JKT Mgambo.JAJA
Hakuna mshambulizi aliyefunga bao hadi sasa katika dakika 270 katika kikosi hicho cha mkufunzi, Mbrazil, Marcio Maximo. Baada ya viungo, Andre Coutinho na Saimon Msuva kufunga katika ushindi dhidi ya Prisons, mlinzi Kelvin Yondan alifunga moja ya mabao mazuri hadi sasa katika ligi kuu wakati alipomnyang’anya mpira mshambulizi, Iddi Mbaga na kuanzisha ‘ move’ aliyopanda nayo hadi alipokutana na pasi ya mwisho kutoka kwa Haruna Niyonzima. Kelvin alipiga kiufundi mpira akiwa ndani ya eneo la hatari na kuupeleka pembeni kabisa ya ‘ angle’ na kumuacha golikipa, Jackson Chove akishindwa la kufanya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA MDOGO MDOGO, MTIBWA KILELENI

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la pili walilopata katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 2-1.

Yanga imeendelea kutoa dozi Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa 2-1 JKT Ruvu katika mechi iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa huku Mtibwa Sugar ikiichapa Mgambo Shooting 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Hii ni mechi ya pili kwa Yanga kushinda katika Ligi Kuu kwani iliichapa Tanzania Prisons 2-1, lakini katika mechi yake ya ufunguzi wa msimu huu ilichapwa 2-0 na Mtibwa hivyo kuanza safari yake ya kusogea katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kwa mwendo mdogo mdogo.
Katika mechi ya jana, hadi mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa kwa shuti kali na beki Kelvin Yondani dakika ya 35 akiunganisha pasi safi ya Haruna Niyonzima.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Niyonzima kwa mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni dakika ya 73 huku bao la JKT Ruvu likifungwa dakika ya 90 kwa shuti kali na Jabir Aziz akiwa nje ya 18. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...