Thursday, May 29, 2014

MUME WA FLORA MBASHA ANATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA SHEMEJI YAKE



JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.

Taarifa zilizopatikana  ndani  ya  jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014 akidai  kufanyiwa  unyama  huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili)  wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa  kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa  alitekeleza ukatili wake huo ndani ya  gari lake  hali ambayo  ilimfanya mlalamikaji kutoa  taarifa  Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.

 
Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.

Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu  makali  aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi  aende  Hospitali ya Amana  na  kugundulika  kuwa aliingiliwa  kimapenzi na kumsababishia michubuko  sehemu za  siri. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWILI WA MSANII RACHEL HAULE WAAGWA LEO JIJINI DAR

Mwili wa muigizaji wa filamu nchini Rachel Haule umeagwa leo hii katika viwanja vya Leaders na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Kinondoni. Wasanii wengi ndugu, jamaa na marafiki wamejawa katika simanzi kubwa huku Irene Uwoya akizimia pengine kwa mshituko wa kuondokewa na msanii mwenzao. Angalia picha zikionyesha matukio ya mwili wa Rachel tangu akitolewa Muhimbili, kupelekwa Sinza na Leaders..........
Irene Uwoya akiwa amezimia . Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

SHEIKH PONDA AGOMA KWENDA MAHAKAMANI

Sheikh-Ponda1_41fd8.jpg
Kiongozi wa Taasisi ya Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aligoma kufikishwa mahakamani kutoka mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Morogoro, akidai kuchoshwa kuhairishwa kwa kesi yake kila anapofikishwa mahakamani.



Pamoja na kuchelewa kufikishwa mahakamani, kesi yake iliahirishwa tena hadi Juni 10 baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo kusema kuwa jalada bado halijarudishwa kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili wa kiongozi huyo, Bathelomeo Tarimo alilalamikia hali hiyo na kutaka haki itendeke kwa mteja wake.

Akizungumza jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema kuwa kukwama kwa faili la Sheikh Ponda ni kutokana na maombi namba 25 ya mwaka 2014 yanayosubiri kusikilizwa mahakamani hadi sasa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 29, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HALIMA MDEE AMVURUGA WAZIRI TIBAIJUKA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.


Mawaziri wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS GOODLUCK ATANGAZA VITA VIKALI

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameagiza kufanywa oparesheni kali zaidi ili kudhibiti alichokiita mauaji ya kiholela yanayofanywa na magaidi.
Katika hotuba kwa taifa kuadhimisha siku ya demokrasia, rais Jonathan alitaja utekaji nyara wa zaidi ya wasichana mia mbili wa shule na kundi la Boko Harama kuwa unyama usiokubalika kamwe.
Waandishi hata hivyo wanasema kuwa haijulikani rais Jonathana anazungumzia kuchukua hatua zipi au ni oparesheni gani itafanywa kwa sababu tayari eneo hilo la Kaskazini mashariki mwa Nigeria tayari limewekwa chini ya hali ya hatari.
Rais Jonathan pia ameahidi kufanya mashauriano na upatanishi na watu watakaoweka silaha chini na kukoma kujihusisha na ugaidi.
Alipongeza jamii ya kimataifa kwa kuisaidia Nigeria kukabiliana na tatizo la ugaidi na usalama kwa jumla.
Rais Jonathan ameahidi kushughulikia swala la umasikini ambalo limechochea harakati kama za Boko Haram, lakini akasisitiza hilo litafanyika tu ikiwa ugaidi unaotendwa na Boko Haram utakomeshwa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Benki ya dunia inasema kuwa zaidi ya watu milioni miamoja na kumi na tatu wanaishi kwa umaskini katika taifa hilo linalozalisha kiwango kikubwa zaidi cha mafuta Afrika.
Rais Goodluck, ametoa fursa kwa Boko Haram ikiwa wanataka kufanya mazungumzo na serikali kama njia ya kusuluhisha matatizo yao.
Maelfu ya watu wameuawa katika miaka mitano ya harakati za kundi hilo.Mwaka huu pekee watu 2,000 wameuawa huku zaidi ya wengine 750,000 wakiachwa bila makao.

MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU MALAWI KUTANGAZWA KESHO

Hatimaye tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kesho ijumaa.
Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya juma lililopita.
Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.
Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku 30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.
Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...