Tuesday, March 27, 2018

MAAJABU: JENEZA LAKUTWA NJE YA GETI LA NYUMBA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nelson Edson mkazi wa eneo la Nsalaga Uyole Jiji la Mbeya amestaajabu baada ya kuamka na kukuta jeneza nje ya geti la nyumba yake lililowekwa na watu wasiojulikana.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa mtaa huo Paulo Ngonde amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia siku ya leo March 27, 2018 ambapo alipigiwa simu na mjumbe wa mtaa huo juu ya uwepo wa tukio la jeneza kukutwa nje ya nyumba ya Nelson Edson.
Aidha Mwenyekiti Ngonde ameongeza kuwa katika mtaa wake kumekuwa na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na matukio ya utupaji watoto lakini hili la kukutwa kwa jeneza nyumbani kwa mtu ni la kwanza.

WATU WANNE WAKAMATWA WAKIHUJUMU MIUNDOBINU YA TANESCO MKOANI MBEYA

Meneja wa TANESCO Mbeya akiongea na waandishi wa habari pembeni ni Kamanda wa polisi mkoani Mbeya DCP Mohammed Mpinga.

 Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuwakamata watu wanne kwa tuhuma za kuingilia miundombinu ya shirika la umeme nchini (TANESCO).

Akiongea na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi mkoani humo DCP Mohammed Mpinga amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na maafisa wa Tanesco march 23, mwaka huu walifanya Oparesheni katika maeneo ya vijiji vya Isebe na Isajilo vilivyopo Wilaya ya Rungwe kufuatia taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanaingilia miundombinu ya Tanesco katika vijiji vyao pamoja na kufanya wizi wa nguzo za umeme na kuwaunganishia umeme wakazi wa maeneo hayo kinyume cha sheria. 
Watuhumiwa wa uhujumu miundombinu ya TANESCO wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.


Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Idd Hamis Mwambusye Mkazi wa Bagamoyo, Benard Kibondi Mkazi wa Kikota, Thobias Wilfred, Mkazi wa Iponjola, Eng. Geofrey Msunga Mkazi wa Mbeya.

Kamanda Mpinga amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa majumbani kwao walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme ikiwa ni pamoja na Mita za umeme 27, nyanya za umeme mkubwa na ndogo, nguzo 57 za umeme ambazo walikuwa zikitumika kuwaunganishia umeme wananchi pamoja na vifaa vingine.

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Pia ameelez kuwa jeshi hilo litaendelea na msako mkali kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na uhujumu wa miundombinu ya Shirika la Umeme  TANESCO katika maeneo mbalimbali.

MKUU WA MKOA APIGA MARUFUKU KUPIGA YOWE

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amepiga marufuku utaratibu wa wananchi wa vijiji vitatu vya Remng’orori, Mikomarilo na Sirorisimba vilivyoko katika wilaya za Bunda, Serengeti na Butiama vinavyogambania mipaka ya wilaya zao, kupiga yowe pale inapotokea kuwapo na jambo la hatari.
Marufuku hiyo imekwenda sambamba na katazo la kuzuia shughuli zozote zikiwamo za kilimo eneo linalogombaniwa, kutotumiwa na pande zote hadi hapo Serikali itakapoamua vinginevyo, ikiwa ni njia pekee ya kuzuia athari zitakazoweza kutokea.
Malima amewataka wananchi wa vijiji hivyo kutoa taarifa Jeshi la Polisi pale linapotokea jambo la kiuhalifu au linalohatarisha usalama wao, kuliko kujichukulia sheria mkononi na kusababisha uvunjifu wa amani.

MBOWE NA VIGOGO WENGINE WA CHADEMA WASWEKWA RUMANDE

Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wamefutiwa dhamana na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mbowe, viongozi wengien ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Viongozi hao wameripoti kituoni hapo leo Jumanne Machi 27, saa tatu asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kuitikia wito wa polisi ambao wamekuwa wakiwahoji kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali Februari 16, mwaka huu.
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredrick Kihwelo wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi ya viongozi walikuwa wanakaidi kuripoti polisi kila wanapotakiwa kufanya hivyo huku Msigwa akiongezwa katika orodha ya viongozi hao baada ya kuhojiwa jana na kupewa dhamana ambayo pia leo imefutwa.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 27, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


      
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MABALOZI WA URUSI WAFUKUZWA KATIKA NCHI MBALIMBALI

Australia imekuwa nchi ya karibuni kufukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.
Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.
Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia. Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.

URENO YA CRISTIANO RONALDO WAPIGWA 3-0 NA UHOLANZI

Cristiano Ronaldo
Haki miliki ya ja

Mabingwa wa Ulaya Ureno walipokezwa kichapo cha kushangaza na Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi.
Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel waliwaweka Waholanzi 2-0 mbele.

Beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ambaye majuzi alitawazwa nahodha mpya wa timu hiyo, alifunga la tatu.

BRAZIL KULIPIZA KICHAPO CHA 7-1 AU KUAIBISHWA TENA?!

Brazil full-back MarceloHaki miliki ya pichaJambo tz
Mkufunzi wa Brazil Tite amesema timu yake bado inatatizwa na "mizimu" ya kipigo cha 7-1 ambacho walipokezwa na Ujerumani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne iliyopita.
Mataifa hayo mawili yatakutana tena mara ya kwanza Jumanne mjini Berlin tangu Brazil walipoaibishwa kwao nyumbani wakati wa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
"Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...