Sunday, December 28, 2014

WANAWAKE WANAOCHELEWA KUBEBA UJAUZITO WAONYWA

Dk Ali Mzige
 Dk. Ali Mzige

WANAWAKE wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko kunawaweka hatarini kuja kupata watoto wenye mtindio wa ubongo.
Mbali na hilo, pia wanaume wanaotafuta watoto wakiwa katika umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60, nao wametajwa kuwa hatarini kupata watoto wa aina hiyo na wakiepuka hilo, watakosa uwezo mzuri wa akili darasani.
Taarifa ya daktari mkongwe nchini, Dk Ali Mzige aliyotoa wiki hii, amebainisha kuwa hali ya umri mkubwa wa wazazi wa kike na kiume, ndio chanzo kikubwa cha kuzaliwa kwa watoto wa aina hiyo, na siyo uchawi wala mazingaombwe.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

DK. SLAA AZIDI KUMBANA KIKWETE ACHUKUE HATUA DHIDI YA PROF. MUHONGO

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete asitumie kivuli cha mapumziko ya sikukuu kuchukua uamuzi dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo anayehusika katika kashfa ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow ya Sh306 bilioni.
Pia, amemtaka Rais Kikwete kuwaeleza ukweli Watanzania kuhusu kigogo wa Ikulu aliyenufaika na mgawo wa fedha, Sh800 milioni za akaunti hiyo zilivyotumika na mnufaikaji alikuwa nani.
Dk Slaa aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa Somangila-Kigamboni Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa kuwachagua wenyeviti sita kati ya 13 wa Ukawa wa kata hiyo yenye mitaa sita.
“Tunamtaka haraka Rais Kikwete amfukuze kazi Profesa Muhongo, asiseme anakula ‘bata’ Msoga (Kijijini kwake Bagamoyo mkoani Pwani) eti sikukuu...Tumemchagua atusimamie na kutuongoza kwa saa 24 kwenda kula Krismasi huku wagonjwa wanakufa hospitalini ni dharau kwa Watanzania,” alidai.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

UGONJWA WA TB HATARI WINGIA NCHINI


 
Moja ya Chumba cha maabara kwa ajili ya vipimo na utafiti wa ugonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto.

Wakati Taifa likikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa dawa hospitalini, aina mpya na hatari zaidi ya ugonjwa wa kifua kikuu sugu imegundulika na kuathiri mtu mmoja nchini.
Mgonjwa huyo alibainika kuwa na kifua kikuu sugu kisicho na tiba, aina ya ‘Xtreme Drug Resistant’ au XDR-TB ambayo hapo awali haikuwa ikiwaathiri Watanzania.
Huyu ni mgonjwa wa pili kubainika kuwa na aina hii hatari ya TB baada ya kesi ya kwanza kuripotiwa mwaka 2011.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa XDR-TB ni nadra sana ambapo ni nchi 77 tu duniani ikiwamo Tanzania zimeripoti tatizo moja moja, mwishoni mwa mwaka 2011.
Taarifa zilizokusanywa na WHO kutoka katika mataifa mbalimbali duniani zinahakiki kuwa kuna asilimia tisa tu ya kesi za XDR-TB. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 28, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MWENYEKITI WA CHADEMA AREJESHWA KWAO RWANDA


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani Mbogwe mkoani Geita Omari Atanas, amekamatwa na maofisa Uhamiaji wilayani hapa kurudishwa kwao nchini Rwanda baada ya kubainika sio raia wa Tanzania.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo, Aman Mwenegoha, alisema Mwenyekiti huyo alikamatwa Desemba 22, mwaka huu na maofisa Uhamiaji na kuhojiwa kwa muda na kugundulika sio raia wa Tanzania bali ni raia wa Rwanda.
Mwenegoha alisema , awali tetesi za uraia wa Atanas, zilianza wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali wa Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini, baada ya Mwenyekiti huyo kufika kijiji cha Luganga. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

RUSHWA, NGONO TATIZO MISS TANZANIA


“Kwa sasa hana uamuzi wowote mpaka pale atakapokuwa amepewa barua rasmi.” Lundenga 

Serikali imesema imeyafungia mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandaaji kukiuka taratibu na kanuni huku pia yakitajwa kukithiri kwa rushwa ya ngono na upendeleo.
Mashindano hayo yalifunguliwa mwaka 1994, yamefungiwa kwa miaka miwili baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi na washiriki.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bazara la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza alisema jana kuwa Kamati ya Miss Tanzania kupitia kampuni yake ya Lino Agency, imekiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
“Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,” alisema Mngereza.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

YANGA, AZAM MWISHO WA UBISHI LEO

Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako kutafanyika mchezo kati ya Azam na Yanga
Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

YANGA leo itakuwa mwenyeji wa Azam FC katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Timu zote zinashuka dimbani zikiwa na pointi 13 kila moja zikitofautiana kwa uwiano wa mabao.
Mechi ya leo ni ya pili kukutana kwa timu hizo msimu huu, baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyofanyika mapema Septemba na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na aliyekuwa mchezaji wao Geilson Santos ‘Jaja’ na Simon Msuva.
Katika historia ya kukutana kwao kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga wanaonekana kuwazidi Azam baada ya msimu wa mwaka 2012/2013 kuwafunga bao 1-0. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

FIFA YAMPA BEJI MWAMUZI WA SIMBA NA YANGA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akijiandaa kuusaini mpira ulioshikiliwa na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa (kulia)

MWAMUZI aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe2
Jonesia Rukyaa ni miongoni mwa waamuzi wa kike sita waliopata beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Jonesia alimudu vyema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Wengine waliopata beji hiyo ni Florentina Zablon wa Dodoma na Sophia Ismail wa Mara (Waamuzi wa kati) na Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary wa Tanga, Grace Wamala kutoka Kagera na Dalila Jaffary wa Zanzibar (Waamuzi Wasaidizi).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KIONGOZI WA AL-SHABAAB AKAMATWA

 Kundi la wapiganaji wa Al shabaab
 
Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi. Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat. Mapema mwaka huu alikosana na kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC 

WANAUME WALIOOANA WAPUNGUZIWA HUKUMU

 Wanaume waliooana Misri wapunguziwa hukumu jela
 
Mahakama moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto Nile huku wanaume wawili wakionekana wakivalishana pete na kukumbatiana.
Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja. Ushoga ni kinyume na utamaduni wa Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria. Wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri. 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...