Sunday, December 28, 2014

FIFA YAMPA BEJI MWAMUZI WA SIMBA NA YANGA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akijiandaa kuusaini mpira ulioshikiliwa na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa (kulia)

MWAMUZI aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe2
Jonesia Rukyaa ni miongoni mwa waamuzi wa kike sita waliopata beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Jonesia alimudu vyema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Wengine waliopata beji hiyo ni Florentina Zablon wa Dodoma na Sophia Ismail wa Mara (Waamuzi wa kati) na Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary wa Tanga, Grace Wamala kutoka Kagera na Dalila Jaffary wa Zanzibar (Waamuzi Wasaidizi).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya kwenye mtandao wa Fifa kwa upande wa wanaume Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin Saanya wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama waamuzi wa kati.
Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Fredinand Chacha wa Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.
Tanzania imepata beji nyingi za FIFA kwa upande wa wanawake msimu mpya wa mwaka 2015 kwani haijawahi kupata beji zaidi ya nne tangu ianze kutoa waamuzi wa kike, mwaka huu 2014 haikuwa na mwamuzi wa kike wa FIFA.
Waamuzi wa kike ambao walishawahi kuwa na beji za FIFA kuanzia mwaka 2006 ni Flora Kashaija, Isabela Kapera na Judith Gamba kama waamuzi wa kati na waamuzi wasaidizi ni Zahara Mohamed, Saada Tibabimale na Mwahija Omary kutoka Zanzibar.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Habari Leo 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...