Tuesday, August 13, 2013

NDAUKA AANZA KUNG'AA ANGA ZA MUZIKI.....!!!

MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo ya aina yake ya nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG, katika tamasha la sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa single inayoenda kwa jina la  'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.


 
 Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na kazi ya filamu ambayo ameizoea.

Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.

"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema Ndauka.

TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI )


Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.

 
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.

 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
 

-Bongo5

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AUGUST 13, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

MWINGEREZA ADAKWA NA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SH 118,314,900

 (Picha na maktaba)

RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.

Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.

Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.

Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.

CRDB YAKABIDHI WODI YA WAZAZI NA VIFAA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA META-MBEYA


 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki. 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...