Saturday, April 20, 2013

Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf akamatwa akijiandaa kugombea ubunge.


Polisi nchini Pakistan wamemtia mbaroni rais wa zamani wa nchi hiyo Jenerali Mstaafu Pervez Musharraf.
Musharraf amekamatwa leo nyumbani kwake mjini Islamabad na kufikishwa mahakamani.
Kiongozi huyo alirejea Pakistan mwezi uliopita, akitarajia kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwezi ujao, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minne.
Hata hivyo ombi lake lilikataliwa na maafisa wa uchaguzi, kwa misingi  kwamba anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yanayohusiana na  kipindi chake cha utawala.
Hapo Jana mahakama mjini Islamabad iliamuru Musharraf akamatwe.

ROSE NDAUKA AWATEGA MADENTI WA DSJ, HIKI NDO ALICHOKIFANYA

STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.

Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

ANAYEMWEZESHA WEMA SEPETU KIMKWANJA AJULIKANA,

Lile fumbo ambalo limekua likiumza vichwa vya wadakuzi wingi wakijiuliza Wema anawezeshwa na nani sasa limepatiwa majibu. Kwa mujibu wa wadaku waliobobea wametamba kunyaka fulu data za mnyange huyo ambae aliwaacha watu midomo wazi baada ya kumlipia msanii mwenzake mamilioni ya shilingi na kumuepusha kwenda Segerea. Wadau hao wa udaku wamekataa kumtaja boss huyo ambae ni milionea tena ni mtoto wa mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania miaka ya nyuma."Unajua bwana Wema sasa hivi kaingia kwa tajiri asieishiwa huyu jamaa ana pesa kama mchanga, tena Wema akitulia mbona atafanya vitu vikubwa hadi watu washangae kwasababu jamaa huyo anampenda sana" Akiongea kuhusu karibu wake na huyo tajiri wa Wema mtoa data huyo alisema yeye ni rafiki wakaribu sana na bosi huyo na hapendi watu wajue ishu hizo hivyo akimtaja milionea huyo atajua yeye ndie aliyevujisha siri zake
From: zeddylicious

VIROBA TISHIO JIPYA LA SARATANI YA KOO KWA WANAUME


Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya saratani katika Kitengo cha Patholojia, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Henry Mwakyoma na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa wameeleza hayo jijini Dar es Salaam. 

Walisema kuwa ingawa bado hakuna visababishi kamili vya saratani hiyo, asilimia 90 ya wagonjwa wa saratani ya koo wamekuwa na historia ya uvutaji sigara, unywaji pombe kali kama viroba na kula aina za vyakula vilivyochomwa
ikiwamo nyama na samaki, ulaji pilipili, ndimu, ‘chilisosi’ na unywaji wa vitu vya moto kupita kiasi. 

“Ongezeko ni kubwa, asilimia 90 ya wagonjwa tuliowapokea hapa wana historia ya kutumia vilevi vikali, sigara, pilipili kwa wingi na aina nyingine na vitu vinavyosababisha saratani hii,” anasema Dk Kahesa.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 20.04.2013

.
.
.

Fid Q Atoa Mauzo RBT Ya Wimbo Wake Mpya Kuweka Kumbukumbu Ya Marehemu Bi. Kidude ...

Kuna uthubutu wa kusema kuwa hili inawezekana kuwa ni wazo zuri na jema kabisa ambalo toka mwaka uanze umewahi kulisikia ...
Rapper kutoka MWANZA CITY, Fid Q amependekeza kujengwa kwa kumbukumbu itakayomuenzi ambayo pia itatumika kusaidia waliokuwa karibu na marehemu Bi. Kidude aliyefariki na kuzikwa jana huko visiwani Unguja ...
Akiongea katika radio interview na kipindi cha XXLkinnachoongozwa na BDozen,Fid Q amependekeza kufanyika kwa jambo hilo hata kwa harambee itakayochangisha fedha za kufanikisha kitu hicho ...

Kwa kuanzia, Fid Q ambae alipata nafasi ya kurekodi wimbo pamoja na marehemu,"JUHUDI ZA WASIOJIWEZA" uliokuwa kwenye album yake ya Propagandaametoa mauzo yote ya miito ya simu, yaani Ring Back Tones [RBT]yatakayouzwa kwa wananchi na wapenzi wa muziki katika kusaidia ujenzi wa museum hiyo ...

Fid Q "Sitachukua hata thumni ..."

Hiki ni kitu cha kujivunia kuwa na mwanamuziki kama huyu ambae naweza kusema anauona umuhimu wa wanamuziki wakubwa hapa nchini, Bi. Kidude amekuwa mwanamuziki wa Taarabu aliyefanya vizuri sana na kuitangaza nchi hii ...
Mimi na wewe, tuanze kwa kushiriki kwenye hili ... BIG UP Fareed !!!
R.I.P Bi. Fatuma binti Baraka a.k.a Bi. Kidude

DARASA LA SABA KUJIUNGA VYUO VIKUU




Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo
Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.


Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”

Wanaotumia laini za simu zisizosajiliwa kutozwa Sh500,000 au kufungwa

Ni kauli ya TCRA ikinukuu sheria ya mawasiliano. Lengo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Profesa  John Nkoma, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Kampuni za Simu kuhusu usajili wa laini za simu Dar es Salaam jana.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.

‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano   mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.

“Katika vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na Aprili 11 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na uvunjifu wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika  jamii.

Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu  ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia 93 na asilimia 7 hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki inatakiwa kuondoka haraka..

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...