Wednesday, August 06, 2014

BINTI ALIYEGOGWA KWA BAHATI MBAYA NA MTOTO WA RAIS OBAMA ATOA KALI YA MWAKA...!!!

Mtoto wa kike wa rais wa  Marekani, Maria Obama mwenye umri wa miaka 16 alimgonga kwa bahati mbaya msichana aliyefahamika kwa jina la Bridget Truskey walipokuwa katika tamasha kubwa la muziki la Lollapalooza nchini Marekani. 
Msichana huyo amewashangaza watu baada ya kuonesha kufurahishwa sana na tukio hilo  kutokana na umaarufu wa Maria Obama.
Truskey ametweet sentensi kadhaa kuonesha furaha yake huku maelezo yakionesha kuwa haamini kilichotokea.
“I got (accidentally) kicked by Malia Obama today at Lollapalooza. No lie. Malia. Obama. It was awesome. #lollapalooza.”  Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA: BUNGE LITAPOTEZA FEDHA NYINGI ZA WANANCHI...!!!

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa vikao vyake mjini Dodoma jana. 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kuendelea vikao vya Bunge Maalumu la Katiba bila kuwapo maridhiano baina ya pande zinazovutana na upande mmoja ukibaki nje ya Bunge, ni sawa na kutumia vibaya fedha za Watanzania.
Amesema kauli kwamba akidi ya wajumbe wa Bunge hilo imetimia na vikao vinaweza kuendelea haiwezi kuzaa Katiba itakayokubaliwa na wananchi wote na ni tofauti na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyoeleza katika sehemu ya kufanya uamuzi.
Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema, “Kama uwezekano wa kukutana upo, kwa nini Bunge liendelee kutumia fedha wakati mnajua kuwa mwisho hamtafikia uamuzi? Jambo la msingi ni kujitahidi kuafikiana na Bunge liwe na wajumbe wote.”
Kauli ya Warioba imeungwa mkono na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba wakati akichangia hoja ya mabadiliko ya kanuni ya Bunge hilo kwa kulitaka bunge hilo kujitathimini iwapo baada ya mjadala litaweza kufikia uamuzi, ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha za walipakodi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PINDA: TUNGEJUA TUNGEAMUA AINA YA MUUNGANO KWANZA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda PICHA|MAKTABA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema kama Serikali ingejua, ingeanza kwa kura za maoni ya wananchi kuamua aina ya muungano wanaoutaka, kabla ya kuendelea na mchakato wa Katiba.
“Tungejua kama hali ya aina hii itajitokeza, basi tungeanza na kura ya maoni, tungewauliza wananchi kama wanautaka muungano na kama ndiyo, basi uwe wa aina gani au serikali ngapi, mtu angesema moja, mbili, tatu na kadhalika,” alisema Pinda jana kwenye Viwanja vya Bunge mjini hapa.
Pinda alikuwa akijibu swali kuhusu hatima ya Bunge Maalumu kutokana na wajumbe wa Bunge hilo ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao hivyo wakishinikiza kile walichokiita kujadiliwa kwa rasimu iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na siyo vinginevyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA SC WAIBUKA NA KUIPA MAKAVU ‘LAIVU’ CECAFA, WASEMA INALICHIMBIA SOKA KABURI


benomarcio

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza” alisema Beno. 
Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”

FRANK LAMPARD ANAWEZA KUFIKIA REKODI YA KUCHEZA MECHI 1,000 AKIWA MANCHESTER CITY

_76387466_frank_lampard_chelsea_getty
FRANK James Lampard, mwenye miaka 36, mpaka sasa amecheza mechi 973 kwa klabu na nchi yake katika maisha ya soka.
Anahitaji mechi 27 tu kufika digiti nne na kitu hicho anaweza kufanya kupitia michuano ya ligi kuu soka nchini England baada ya kujiunga na Manchester City kwa mkopo kutoka klabu ya New York City mwezi huu.
Kiungo huyo mkongwe ataitumikia Man City mpaka mwezi Januari mwakani ambapo ataende NYCFC kujiandaa na michuano ya ligi kuu nchini Marekani.
Atakuwepo kwa michezo 23 ya ligi kuu, mechi sita za ligi ya mabingwa, ataanza kombe la Capital One na FA na mechi ya Ngao ya Hisani itakayopigwa siku ya jumapili.
Lampard ambaye bado hajastaafu soka la kimataifa, ana nafasi kubwa ya kuongeza mechi zake 106 alizocheza kwa timu ya taifa baada ya kurudi ligi kuu.
Lampard ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwa taifa lake. Pia alicheza England B na alicheza mara 19 katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 19.
Kiungo huyo alicheza mechi 187 akiwa na Westaham, klabu yake ya kwanza na alicheza mechi 11 akiwa kwa mkopo Swansea kabla ya kwenda kucheza mechi 649 katika miaka 13 aliyocheza Chelsea, na kujiweka katika nafasi ya tatu ya kucheza mechi nyingi klabuni hapo nyuma ya Peter Bonetti na mchezaji anayeshikilia rekodi Ron Harris.
Mchezaji wa mwisho wa England kufikisha mechi 1,000 katika timu ya wakubwa alikuwa kocha msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs ambapo alifikisha idadi hiyo mwaka 2013 kwenye mechi za ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid.
Kocha wa sasa wa Fleetwood, Graham Alexander, ambaye aliichezea Scunthorpe United, Luton Town, Preston North End na Burnley alifikisha mechi 1,00 mwezi aprili 2011.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...