Monday, April 22, 2013

WANAWAKE WATANO WANASWA WAKIGAWA URODA KWA WANAUME WAWILI NDANI YA CHUMBA KIMOJA HUKO MWANANYAMALA

Kwa tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja kilichopo Mwananyamala jijini Dar.

Watu hao walinaswa katika oparesheni kabambe iliyoongozwa na Kamanda Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, OCD Wilbroad Mtafungwa pamoja na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai.


Katika zoezi hilo, polisi walivamia kambi kuu inayotajwa kusheheni wanawake wanaojiuza iliyopo Mwananyamala A ambapo ‘wauza sukari’ hao hutumia vyumba vyao kufanya ufuska huo.
Polisi hao walipofika kwenye chumba kimoja kilichopo eneo hilo, walikumbana na upinzani mkubwa wa watu waliokuwa ndani na baada ya kufanikiwa kuufungua mlango, waliwakuta wanawake watano na wanaume wawili wakiwa kimahaba.
Mbali na hao, polisi walifanikiwa kuwanasa wanawake wengine kwenye vyumba vyao na baadhi mtaani wakijiuza ambapo walipewa kibano cha hali ya juu.
Imeelezwa kuwa, wanawake hao wamekuwa na tabia ya kujiuza na wakati mwingine hukubali kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja, hali ambayo ni hatari sana.
Mkazi mmoja wa eneo hilo, Husein Juma alisema: “Kwanza tunampongeza Kamanda Mtafungwa kwa operesheni hii, wanawake hawa wamekuwa ni tatizo kwani wamekuwa wakijiuza waziwazi na kutupa ovyo kondomu.
 Naye Inspekta Swai alisema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo wakaona ni vyema kuyafanyia kazi ambapo waliwakamata zaidi ya watu 35, wanawake kwa wanaume wanaohusika.

BI KIDUDE UMEKWENDA, UMEACHA MAJANGA YA WASANII WA KIKE BONGO!, WAJUE BAADHI YAO HAPA

Kishindo cha kuondoka kwako kwenye uso wa dunia tunayoishi kinaweza kuwa kikubwa ama kidogo au hakuna kabisa kutokana na mazingira au heshima uliyojijengea katika jamii.
Fatma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na zaidi ya miaka 100. Bado jina lake linatamkwa kwenye vinywa vya wengi na linaweza kuendelea kutamkwa kwa miaka mingi zaidi.
Bi Kidude, mwanamke shujaa mzaliwa wa Visiwani Zanzibar alileta mapinduzi katika muziki asilia wa mwambao. Aliitangaza Zanzibar, Tanzania na Bara la Afrika sehemu mbalimbali duniani alipokwenda kwa ziara za kimuziki. Inaaminika alifanya kazi hiyo ya muziki, mafunzo ya unyago na biashara ya hina na wanja kwa zaidi ya miaka 90. Katika kipindi chote, Bi Kidude hakushuka kimuziki hadi pale mdomo ulipoanza kuwa mzito kutokana na uzee miaka 10 kabla ya kifo chake Aprili 17, mwaka huu baada ya kuugua maradhi ya kisukari na kongosho kwa muda mrefu.
Pia inaaminika kuwa ndiye msanii mkongwe zaidi aliyekuwa akipanda jukwaani na umri mkubwa ukilinganisha na wengine unaowajua.

Mpango wa bunge kuidhinisha Sheria ya ndoa za jinsia moja Ufaransa wazua kizazaa mjini Paris.

Siku mbili kabla ya bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria inayohalalisha ndoa za jinsia moja kumetokea maandamano ya dakika za mwisho mwisho mjini Paris.
Watu wanaopinga sheria hiyo wamekusanyika katika eneo la Montparnasse la mji mkuu katika juhudi za mwisho za kuizuia sheria hiyo, huku maandamano mengine ya kundi hasimu pia yaliandaliwa kuiunga mkono sheria hiyo.
 Zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika maandamano mengine ya kupinga ndoa za jinsia moja.
Makundi ya kutetea haki za binadamu pia yameripoti ongezeko la matusi na mashambulizi ya kimwili dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji nchini Ufaransa.
Ufaransa inatarajiwa kuwa nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za jinsia moja, kufuatia kuidhinishwa sheria hiyo nchini New Zealand wiki iliyopita.

Liewig akabidhi majina ya anaowabakiza Simba.

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikielekea ukingoni, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji watakaobaki Msimbazi.
Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo katikati ya msimu huu akichukua mikoba ya Mserbia, Milovan Cirkovic, aliyetimuliwa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga, alisema wachezaji wengi waliopendekezwa na Liewig ni vijana.
 
“Ni mapema kuzungumzia usajili katika kipindi hiki, lakini kikubwa ni kwamba kocha tayari amekabidhi orodha ya wachezaji anaowahitaji watakaoendelea kuichezea Simba katika msimu ujao.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.

TAPELI ANAYETUMIA JINA LA WAZIRI LUKUVI AMTAPELI LOWASSA IRINGA

maofisa  wa  polisi mkoa wa  Iringa
wakiweka mtego katika nje ya
 ukumbi wa St Dominic  ili kumnasa
  tapeli  huyo anayejiita ni mtoto  wa
  waziri Lukuvi  na kutapeli  watu
Tapeli  anayetapeli  watu maeneo
 mbali mbali ya Tanzania  kupitia jina
 la  waziri Lukuvi akiingizwa ktk  gari maalum leo
Tapeli  Jonathan Wiliam Lukuvi
feki akitiwa matatani askari kanzu  Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dkt
 Christina  Ishengoma ,askofu Dkt
Boaz Sollo na Waziri mkuu wa
  zamani Edward  Lowassa akimsikiliza
 tapeli huyo akimpa maneno ya kitapeli  Lowassa
Kijana  huyo Tapeli akimsomesha
waziri Lowassa ukumbini kwa
kuahidi kuchangia 100,000 huku
akimwomba  kumsaidia misaada  zaidi
Hapa akipelekwa  katika gari
 maalum Hapa akiingizwa katika
Taxi tayari  kwenda  polisi

MAGAZETI YA LEO APRILI 22, 2013

11 6fa4e
13 d676614 a60d6

LADY JAYDEE AWACHANA TENA CLOUDS..... ANADAI KWAMBA MUNGU SI "RUGE" WALA "KUSAGA"

Baada ya kipindi kirefu cha kuongea kwa mafumbo dhidi ya wamiliki wa Clouds FM kuwanyonya wanamuziki akianzia na wimbo wake waJoto Hasira, mwanamuziki Judith Wambura ameendelea kuishambulia redio hiyo na leo Jumapili ameamua kufunguka kwa kuwachana live wamiliki wa redio hiyo.

Hii ni post yake aliyoipost twitter:

Lady JayDee ‏@JideJaydee 1h Naamini kabisa kuwa Mungu sio Ruge wala Kusaga. Atanisimamia kwenye hili #Confidence
\

BABY MADAHA: NTAWACHANGANYA WANAUME KAMA DIAMOND

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema mwaka huu atawachanganya wanaume kama afanyavyo Nasibu Abdul ‘Diamond’ ili kwenda sawa.
Akifafanua kauli yake kwa paparazi wa Stori 3, Baby Madaha aliweka bayana kuwa haoni tatizo kunaswa na Mwisho Mwampamba kama ilivyoripotiwa hivi karibuni wakati huohuo anatoka kisela na mkali wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’.
“Watakoma mwaka huu, lazima niwachanganye sana, mbona wao wanatuchanganya sana kama Diamond vile anavyofanya!” alisema Baby.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...