Tuesday, June 03, 2014

RAIS WA MALAWI ANA MSIMAMO MKALI ZIWA NYASA



Rais wa Malawi, Peter Mutharika. PICHA|MAKTABA 

Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa Malawi.

Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.

Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpya wa kutaka kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.

Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na Tanzania ni kupoteza muda. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

'MTOTO WA BOKSI' KUZIKWA LEO, NDUGU WA BABAKE WAJITOKEZA

Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra Rashid (4) likishushwa kutoka kwenye gari ili kuingiza katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Morogoro Hospitali ya Taifa ya Muhimbi jijini Dar es Salaam. Picha na Juma Mtanda 

Ndugu wa baba wa mtoto, Nasra Mvungi (4) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jana walijitokeza wakitaka wapewe mwili wa marehemu kwa ajili ya maziko.
Baada ya kuwasili hospitalini hapo saa 1:35 asubuhi, ndugu hao wakiongozwa na baba wa mtoto huyo, Rashid Mvungi walikutana na maofisa wa ustawi wa jamii wakiongozwa na Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti wakitaka wakamzike mtoto wao kwa kufuata imani ya dini yao ya Kiislamu.
Hata hivyo, Ngungatuti alipinga hoja hiyo akisema suala la ndugu kuzika halina nafasi na kwamba mtoto atazikwa na ustawi wa jamii ambao ndiyo waliokabidhiwa mtoto huyo na polisi.
“Tutamzika kiserikali kwa kuzingatia imani ya dini yake lakini hatutawakabidhi maiti kwa namna yoyote,” Ngungatuti alisema na kuongeza kuwa wanafanya hivyo kwa kufuata misingi ya kisheria.
Akizungumzia suala hilo Mvungi alisema: “Ndugu zangu wanataka mtoto tupewe lakini kama sheria inakataza mimi sina neno ila kama ingekuwa ni matakwa yangu ningependa nipewe mwanangu nikazike mwenyewe.
Sakata hilo liliendelea mjini Morogoro ambako baada ya mwili kuwasili, watu wanne; wanawake wawili na wanaume walifika Ofisi za Ustawi wa Jamii na kujitambulisha kuwa ni bibi na wajomba wa marehemu wakitaka wapewe mwili wa mtoto huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NIGERIA YAANIKA `BUNDUKI` ZA MWISHO KOMBE LA DUNIA BRAZIL

412895_heroaKOCHA mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa hao wa soka barani Afrika wanaenda kushiriki fainaili hizo kwa mara ya tano na wamepangwa kundi moja na Argentina, Iran na Bosnia.
Wachezaji wazoefu kama Vincent Enyeama, Austin Ejide, Joseph Yobo na Elderson Echiejile waliokuwa sehemu ya kikosi cha fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini wamejumuishwa katika orodha hiyo ya mwisho. Mfungaji bora wa fainali za 29 za AFCON, Emmanuel Emenike, Godfrey Oboabona, John Obi Mikel na Victor Moses wanatarajia kucheza fainali zao za kwanza za kombe la dunia. Kikosi kizima: Walinda mlango: Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim
Walinzi: Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose, Kunle Odunlami Viungo: John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Michael Uchebo, Reuben Gabriel
Washambuliaji: Osaze Odemwingie, Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIA 130, 00 WA DRC WAFUKUZWA BRAZAVLLE

wakimbizi wa Congo wahangaika
Zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wamefukuzwa kutoka Congo Brazaville tangu mwezi Aprili. Wengi wao sasa wanaishi katika kambi za muda nchini DRC.

Serikali ya Brazzaville imesema kuwa watu hao walikuwa wahamiaji haramu lakini wengi wao wamekanusha hili wakisema kuwa wameteswa sana na polisi wa Brazaville. Umoja wa maaifa umetoa wito kwa Congo kukoma kuwafukuza watu hao. Hapo Jumatatu ujumbe kutoka pande zote mbili ulikutana mjini Kinshasa nchini DRC kujaribu kutafuta suluhisho.
Maelfu ya waliohamia kambi hizo za muda za DRC waliishi nchini Brazaville maisha yao yote na sasa wamepoteza kila kitu walichokuwa nacho. Wamedai kuwa polisi wa Brazaville waliwapiga, kuwabaka na hata kuwaua baadhi ya watu walioaminiwa kuwa raia wa DRC wakati wa msako wao.

Huu ni unyama

Upande wa DRC umelalamikia hatua hii na kusema kuwa Brazaville imekiuka haki za binadamu.
Richard Muye ni waziri wa mambo ya ndani wa DRC. Ameambia BBC, '' Mbona sasa wanawafukuza tena kwa wingi hivi bila kujali haki zao? Wanawatesa watu wote, wake waume na hata watoto.''

Brazaville yajitetea

Lakini waziri mwenzake kutoka upande wa Brazaville Raymond Zéphirin Mboulou amekanusha kuwafukuza wakongomani 130,000. Amesisitiza kuwa ni 2000 pekee waliofukuzwa kwa lazima nchini humo, na hiyo pia ni kwasababu walikuwa wahalifu.
"Walifanya uhalifu wa kuchukiza. Wizi, ubakaji ukahaba na mengine. Wameharibu mitaa yetu. Na hawakaribishwi hapa tena kwasababu hao wahamiaji ndio wanaowahangaisha raia wetu usiku na mchana."
Waziri huyo ameongeza kuwa wale wengine 128,000 walioondoka walifanya hivyo kwa hiari yao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

NIGERIA YAKOMESHA 'BRING BACK OUR GIRLS'


Polisi wazuia maandamano Nigeria
Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
Maandamano yamekuwa yakiandaliwa kila siku kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kuishinikiza serikali kutia bidii zaidi katika juhudi za kuwakomboa wasichana hao. Polisi wanasema maandamano hayo yanamepigwa marufuku kwa kuwa yanazua hatari kwa wenyeji.

Aibu kwa serikali

Kampeini ya 'Bring back our Girls, au warudisheni wasichana wetu,'' ambayo imekuwa ikifanywa nchini Nigeria na hata nje ya Nchi hiyo imeleta aibu kubwa sana kwa serikali ya Nigeria.
Waandamanaji wamekuwa wakikutana hadharani wakiishinikiza serikali hiyo kukoma kuzungumza tu katika vyombo vya habari na badala yake waongeze jitihada na kuhakikisha wasichana hao wamekombolewa.

Makosa sio ya serikali

Lakini wiki iliyopita, kundi tofauti lilianzisha kampeini sambamba, na hata kuvuruga ile ilyokuwa ikiendelea ambapo wanadai kuwa hasira zinastahili kuelekezewa hao watekaji nyara na wala sio serikali ya Nigeria.
Kundi hili linatumia nembo 'Release Our Girls Boko Haram'. Wameongeza jina Boko Haram kwa kusudi hapo mwisho. Polisi sasa wanasema kuwa maandamano haya yanatishia usalama kwa wananchi wa Abuja.
Lakini waandamanaji wanaoendesha kampeini ya 'Bring Back our Girls' sasa wanaona kama hili ni jaribio la serikali kuwanyamazisha na wamewasilisha ombi mahakamani kutaka kutolewe agizo la kuvunja amri hiyo ili waruhusiwe kufanya maandamano yao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...