Tuesday, May 21, 2013

GODBLESS LEMA AUMBUKA....VODACOM WADAI KWAMBA ULE UJUMBE WA VITISHO HAUKUTOKA KWA MKUU WA MKOA


BARUA  TOKA  VODACOM

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amedai kuwa uchunguzi wa awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, umetumwa na mtandao wa simu wa nje ya nchi.
Kamanda alisema katika ujumbe huo ambao Lema anadai uliandikwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kutumwa kwenye simu yake Aprili mwaka huu, uchunguzi wa polisi umeonyesha kwamba haukutumwa kupitia kampuni moja wapo ya simu za mikononi ya hapa nchini.

BABA YAKE DULLY SYKES ANASWA AKIVUTA BANGI....!!

   Baba mzazi wa mwanamuziki wa bongo flava nchini Dully Sykes, Mzee Sykes pichani kama inavyoonekana akiwa na madawa haram ya kulevya aina ya bangi mkononi huku mbegu mbegu zikiwa zimedondoka chini.-----  

Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa bongo flava nchini Dully Sykes , Mzee Sykes hivi karibuni alinaswa  akichambua bangi mikononi mwake kwa ajili ya kuivuta.

Tukio hilo la aina yake lilitokea  nyumbani kwa msanii aliyefahamika kwa jina la Shebo, na kushuhudiwa na mwandishii wetu ambae alifanikiwa kumpiga picha mzee huyo akiwa na bangi mkononi mwake.

Mzee huyo akiwa hana shaka yoyote alionekana  akichambua bangi hiyo huku mbegu zake zikidondoka chini kama mchele ( picha ya juu)

Hata hivyo mzee huyo alishindwa kuendelea na zoezi la kuitayarisha bangi hiyo kutokana na kumtilia wasi wasi mwandishi akidhani ni afande.

Prof. Jay ajiunga CHADEMA Angalia PICHA


 


Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Joseph Haule (Prof. Jay) amejiunga rasmi leo na chama cha CHADEMA.

KUTOKA JAMII FORUM, SIRI YA KIFO CHA KAMANDA BARLOW ZAVUJA. KAMANDA MUNA ATAJWA.....!!!

Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika ukurasa wa Mbele kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika gazeti kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana)

Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la
Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri zote.

Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow.

Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.

" MATOKEO YA KIDATO CHA SITA".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA


MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.


“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.


 "Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.

HII NDIO PRIVATE JET ATAKAYOKUWA AKIITUMIA MAKAMU WA RAISI WA KENYA RUTO


Full size bed ndani ya ndege hiyo
Huu ni mlango wakuingilia kwenye ndege hiyo
Breakfast and diner on board 

BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI DODOMA..... MACHANGU WA DAR WAKIMBILIA HUKO



BIASHARA ya ngono katika mji wa Dodoma imeshika kasi kubwa ambapo imebainika kuwa wateja wakubwa ni watumishi wa serikali, wanasiasa na madereva.

Uchunguzi wetu  umebaini kuwa katika biashara hiyo kuna makundi mbalimbali yanayotofautiana kwa malipo ya biashara hiyo.
Wapo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake ambao wamedai kuwa wanalazimika kufanya biashara hiyo kutokana na kubanwa na maisha, hususani katika marejesho ya mikopo wanaichukua kutoka katika taasisi mbalimbali ya kifedha.

Mmoja wa wafanyabiashara ya ngono (jina tunalo) bila kujua anaongea na nani, alieleza kuwa kwa sasa katika mji wa Dodoma kuna ushindani mkubwa wa biashara ya ngono kwani wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini hapa vimeteka soko hilo.

Alisema kutokana na ushindani huo kwa sasa kima cha chini ni sh 7,000 kwa mchepuo mmoja na sh 30,000 hadi 40,000 kwa kulala.

Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa wateja wakubwa wa ngono ni wafanyakazi wa serikali, wanasiasa (wabunge), madereva pamoja na wafanyakazi wa benki.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 21.03.2013

DSC 0043 f478a

DSC 0047 b993f

DSC 0045 6ff67

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...