Wednesday, August 21, 2013

ALHAJ MWINYI NA MZEE MKAPA WAWASILI ZIMBABWE KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MUGABE

Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Harare, Zimbabwe, kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 22, 2013
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katioka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 22, 2013.PICHA NA IKULU

MADIWANI BUKOBA: TUKO TAYARI KUHAMIA CHADEMA....!!!

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofukuzwa katika Manispaa ya Bukoba, wamesema wako tayari kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kama chama chao kitaendelea na msimamo wa kuwafukuza. Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, mmoja wa madiwani hao (jina na kata yake tumevihifadhi), alisema wako tayari kuhamia Chadema muda wowote kama hawatarudishiwa uanachama wao.

Alisema, madiwani wote waliofukuzwa wana msimamo mmoja, ambapo wanasubiri vikao vya Kamati Kuu ya CC ili wajue hatima yao, lakini vikishindwa kuwarudisha kwenye chama, watahamia Chadema ili kuendeleza harakati zao walizozianzisha.

Alisema, wanachokifanya wao ni kutetea maslahi ya taifa na wananchi waliowapigia kura na si kulinda biashara za watu binafsi, hata kama wanaungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM.

Msimamo huo wa madiwani umekuja siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuwakaribisha madiwani hao katika chama chake na kusema wako tayari kuwafundisha siasa za mageuzi.

GODBLESS LEMA AUGUA GHAFLA, KESI YAKE YAHAIRISHWA




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha jana imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kutokana na mbunge huyo kuwa mgonjwa.

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Hawa Mguruta, anayesikiliza shauri hilo kuwa Lema anaumwa na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya AICC tangu Agosti 14 hadi 19, mwaka huu aliporuhusiwa kutoka hospitali, hivyo ametakiwa apumzike kwa muda wa siku 10 kuanzia Agosti 19, mwaka huu.

Wakili Kimomogoro aliomba shauri hilo liahirishwe hadi siku nyingine, ombi lililokubaliwa na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1 na 2 mwaka huu, ambapo mashahidi tisa wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

DIAMOND NAE ATAJWA SAKATA LA UNGA....!!!



*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange

KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.

 
Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.

PONDA AIGHARIMU SERIKALI MILIONI 10...!!!


*Usafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
 
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.

 
MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .

Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.

Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.

TSVANGIRAI ATUHUMIWA KUDHARA MAHAKAMA...!!!

Morgan-Tsvangirai_da35d.jpg

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu amesema waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya yanajiri wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
P.T

Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njiya huru na haki. Mugabe alipata asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba kikisema hakikua imani ya kupata haki.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 21, 2013

DSC 0001 5fba2
DSC 0002 b5ca6

RAIS DKT SHEIN AFANYA MABADILIKO YA MAWIZARA ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.

Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya MzeeMarekebisho ya muundo na shughuli katika baadhi ya Wizara ni kama ifuatavyo.

ANGALIA VIDEO YA RAIS KAGAME APOPOLEWA KWA MAWE UINGEREZA


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...