Tuesday, May 13, 2014

TAZAMA VIDEO YA JAY Z AKIPIGWA NA SHEMEJI YAKE MBELE YA MKEWE BEYONCE

Screen Shot 2014-05-12 at 11.40.31 PM 
Ni video kamili ikionyesha kilichotokea kwenye lifti ambapo rapper Jay Z anaonekana akipigwa na shemeji yake ambae ni Solange kwa muda usiopungua dakika 2 kwa kutumia pochi na mateke na baada ya hapo wakatoka nje ya lift.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, haya yalitokea wiki iliyopita kwenye After Party ya Met Gala ndani ya Standard Hotel, NYC na ndani ya video inaonesha Jay Z, Beyonce na Solange wakiingia katika Lifti halafu Solange anaanza kumuwakia Jay z kabla ya kuanza kumvamia wakati huo Beyonce akiwa pembeni tu ametulia na wala haingilii.

Bodyguard aliekuemo katika lifti hiyo alianza kumzuia Solange lakini alifanikiwa kuponyoka kama mara tatu hivi na kuendelea kumpiga Jay Z pia kuna muda Solange alirusha teke na Jay Z akazuia lakini hakurudisha kwa aina yeyote ile, sio kwamba alishindwa kumpiga ili alifanya maamuzi ya kuwa mstaarabu tu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAREKANI KUTAFUTA MATEKA NIGERIA

Marekani kusaidia kuwasaka wasichana waliotekwa na Boko Haram
Marekani imesema inapeleka vifaa vya uchunguzi nchini Nigeria kusaidia katika juhudi za kuwatafuta wasichana wanaozuiliwa na kundi la Boko Haram.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shule moja Kusini mwa eneo la Borno mwezi mmoja uliopita.
Msemaji wa Rais Obama Jay Carney amesema kikosi cha maafisa 30 kiko nchini Nigeria tayari kushiriki juhudi hizo.
Amesema msaada huo wa Marekani kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi na pia kutoka idara ya uchunguzi ya FBI. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Hatua hiyo imechukuliwa wakati baadhi ya Jamaa za wasichana waliotekwa nyara wakielezea majonzi baada ya kutazama kanda ya video iliyotolewa na kundi hilo.
Marekani kusaidia kuwasaka wasichana waliotekwa na Boko Haram
Baadhi wameiambia BBC kuwa kanda hiyo imewapa matumaini lakini wameshangaa kuona wasichana hao ambao wengi ni Wakristu wamevalia mavazi ya Kiislam.

Akizungumza kwa uchungu nduguye mmoja wa wasicha waliotekwa ameiambia BBC ni heri kanda hiyo ingeonyesha maiti za wasichana hao kwa kuwa hiyo ingeondoa wasiwasi unaoendelea kukithiri na kuumiza mioyo ya wengi.
Kwenye kanda hiyo ya video kiongozi wa Boko Haram , Abubakar Shekau anasikika akiambia serikali ya Nigeria yuko tayari kubadilishana baadhi ya wasichana hao na wafuasi wake waliofungwa jela.
Hatahivyo wizara ya mambo ya ndani ya Nigeria imetupilia mbali pendekezo hilo.
Seneta Ali Ndume kutoka eneo ambapo wasichana hao walitekwa nyara anaisihi serikali kulegeza msimamo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 13, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

mg 2
mg 1
13 
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE


mg1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo.
Utangulizi
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini.Ugonjwa huu umethibitishwabaada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es Salaam kupelekwa kwenye maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huuni 400 na Vifo 3. Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 ya idadi ya wagonjwa waliogundulika mkoani Dar es salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na 4-Ilala) na idadi ya wagonjwa waliopo wodini mpaka sasa ni 13.
Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa
mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013,wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
Homa ya Dengue
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.
Dengue in ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5 hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali. Homa ya Dengue imeshatokea katika nchi zipatazo 34 barani Afrika.
Hapa Afrika Dengue ni ugonjwa unaojulikana kwa kiwango kidogo sana. Licha ya kwamba milipuko ya kwanza imetokea tangu mwanzoni wa karne ya 19. Matukio ya Ugonjwa huu yameongezeka Afrika tangu miaka ya 1980, matukio mengi yakitokea nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Msumbiji, Somalia, Kenya, Komoro, Djibouti na Tanzania. Ikumbukwe kuwa jina “Dengue” linatokana na neno “Dinga” la kiswahili linalolomaanisha ugonjwa unaotakana na pepo yaani Kudinga pepo. Mabaharia wa Kispanish walipokuja kwenye pwani ya Afrika Mashariki walirudi kwao na kuuita “Dengue”.

MCHWA WAVAMIA IKULU...!!!

Mchwa wavamia ikulu ya Paraguay
Mchwa wamevamia makaazi rasmi ya rais wa Paraguay na kutishia udhabiti wa jengo hilo.
Watalamu wa maswala ya ujenzi wameonya kwamba huenda Rais huyo akapoteza makaazi yake iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa kuwaangamiza mchwa.
Kwa mujibu wa wanasayasi wa kibiolojia mchwa ni mdudu mwenye bidii sana na kamwe hachoki kutekeleza majukumu yake.
Na ni kutokana na hilo ndipo wahenga katika juhudi za kutoa motisha kwa yeyote yule anayetaka kufanikiwa maishani wakasema ''lazima awe na bidii ya mchwa''.
Msemo huu umedhihirika nchini Paraguay baada ya habari kwamba mchwa wamevamia makaazi rasmi ya Rais Horacio Cartes.
Wataalam wa maswala ya ujenzi wanasema mchwa hao wameharibu sakafu na sehemu zilizojengwa kwa mbao.
Wahandisi hao wameonya kuwa huenda sehemu moja ya jengo hilo likaanguka iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
Wamependekeza Rais huyo ahamishwe kutoka jengo hilo ili wataalam waweze kupambana na wadudu hao wenye bidii na ukarabati uweze kufanyiwa jengo hilo.
Ni dhahiri kuwa wageni hao waharibifu sasa wanatishia starehe na itifaki ya Rais Horacio Cartes. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...