Saturday, June 22, 2013

HATIMAE NDUGU YETU MPENDWA CHARLES HILILA AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO



 

 NYUMBA YA MILELE ALIMOLALA MWANDISHI WA HABARI KITUO CHA MATANGAZO CHA CHANELL TEN

Habari Na Steven Kanyeph
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa chaneli ten Charles hilila umezikwa leo katika makaburi ya nyumbani kwao katika kijiji cha Dumida kata ya Tinde mkoani Shinyanga nakuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji akiwemo mkuu wa mkoa wa shinyanga na viongozi wengine wa kiserikali , vyama vya siasa pamoja na viongozi wa kidini.

Mazishi hayo yametanguliwa na ibada ya misa takatifu iliofanyika katika kanisa la mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyangsa na baade kufuatiwa na ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwao na kuongozwa na padre Emmanueli Makolo akisaidiana na padri Josephati Mahalu kabla ya maziko.
katika mahubiri padre Mahalu amewaasa wanajamii kudumisha upendo na kuwakumbusha kuwa kifo kipo mahali popote hivyo wanajamii wanapaswa kumrudia Mungu na kutenda matendo mazuri yenye kuleta amani na yanayompendeza Mungu.


Hali kadhalika mkuu wa mkoa wa Shinyanga Alli Nassoro Lufunga ametoa salamu za rambirambi kutoka katika serikali ya mkoa na kuwaomba wanahabari kudumisha upendo zaidi hasa katika umojawao kwani utawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kuleta tija zaidi kwa wanajamii.
Marehemu Charles hilila amefariki juni 19 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa TB ya mifupa uliokuwa unamsumbua .
Aidha marehemu ameacha mjane na watoto watatu ,
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema mbinguni amina

*********************************************************************************


 

MEYA AZIMIA BAADA YA KUPIGWA NA POLISI

Meya wa Mji Mkuu wa Kampala nchini Uganda akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhumza za kusababisha vurugu.

Kampala, Uganda. Watu wawili wameuawa kwa risasi nchini Uganda juzi, wakiwa katika mkusanyiko kwenye eneo la soko la Kisekka.

Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, pia alizirai baada ya kupigwa na polisi hao waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.

Akiwa kitandani, Meya huyo amesema baada ya kupata kipigo hicho alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini.

“Bomu ambalo lilinifanya nipoteze fahamu lilirushwa katika gari langu na kuingia ndani,” amesema.


Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alieleza kwamba maofisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimtuhumu kwa kuchochea ghasia. 

NKAMIA AZUA VURUGU TENA BUNGENI SAFARI HII ATAKA KUMPIGA MBUNGE MWENZAKE...!!!

1625 cb219Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), kwa mara nyingine ameingia katika kashfa nzito akituhumiwa kutaka kumpiga Mbunge wa Viti Maalumu CUF, Moza Abeid ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki ambapo imeelezwa kuwa Nkamia mbali na kutaka kumpiga mbunge huyo, pia alimtolea matusi mazito ya nguoni (gazeti hili haliwezi kuandika).

Kwa mara ya kwanza mbunge huyo aliingia katika kashfa baada ya kutoa kauli bungeni kuwa hazungumzi na mbwa, bali anazungumza na mwenye mbwa kabla ya kuingia katika mzozo na wahariri na baraza la habari aliposema kuwa Jukwaa la Wahariri na Baraza la Habari ni NGOs za kutafuta fedha.

Uchunguzi wa Mwananchi ambao umethibitishwa na Nkamia mwenyewe umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni kutokana na kuzomewa kwa Nkamia katika kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Dalai Wilaya ya Chemba.

Kwa mujibu wa wabunge mashuhuda ambao waliliona tukio hilo, ilielezwa kuwa Nkamia, ambaye pia ni mwandishi wa habari, alianza kumshushia matusi Moza wakiwa ndani ya Bunge hadi walipotoka nje alimfuata na kutaka kumpiga.

MCHUNGAJI AZAA NA HAUSIGELI WA MIAKA 17 HUKO KIMARA....AVULIWA UCHUNGAJI, MKEWE AOMBA TALAKA...!!!

HAYA ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha Utakaso au Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar, Thomas Mariki anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa kuzaa na ‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.

Akizungumza nasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki, Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka 2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini mmoja hakuwa bahati.


MATESO YAANZA
Mwanamke huyo alidai amani katika ndoa yake ilipotea baada ya kujifungua mtoto wa pili (marehemu), mumewe alianza kumtuhumu kuwa alitoka nje ya ndoa na huyo mtoto hakuwa wake.

MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA..... PENZI LAKE NA DIAMOND LAKAA PABAYA...!!!

TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevujaKwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.
 
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

ANGALIA PICHA ZA BOB JUNIOR AKIPEWA KICHAPO LOCATION...!!!


Bob Junior ameshare picha hizi kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika: Kwa Dizaini hii lazima nirudi kwetu k…Aaaaah Maisha Haya Ya Bongo?,,,,COMING SOON Huu Mzigo…1 Love.


Bob Junior akiwa location kushoot video yake mpya, duuuuuuh...!!! kaaazi kweli kwelii

BOMU LA ARUSHA LAWATESA CCM, POLISI.

 
IGP SAIDI MWEMA. 
KATIBU MKUU MPYA WA CCM ABDULRAHMAN KINANA.

MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne, umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.

Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi unaon
esha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.

“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini kwetu ?.

NASSARI: WAZIRI MKUU MSTAFU EDWARD LOWASSA ANAHUSIKA KUNIPIGA.

 
Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema) Joshua Nassari akiwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), jana, baada ya kuhamishwa kutoka Arusha kwa ajili ya kupata matibabu zaidi baada ya kuumizwa kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni mkoani Arusha.Picha na Silvan Kiwale.


DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.

Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali.

Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana.

Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 22, 2013

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...