Sunday, November 24, 2013

LOWASSA AIELEZEA ILANI IJAYO YA CCM


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wakazi wa Kigamboni.
******
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewaomba wanachama wa CCM kushawishi suala la elimu bure na bora liwe ajenda ya kwanza katika Ilani ijayo ya uchaguzi ya Chama hicho.
Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kigamboni ambako alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kukabidhiwa madawati shule za msingi za kata hiyo, Mh Lowassa amesema kwa maoni yake anapendekeza suala hilo liwe ajenda ya kwanza katika Ilani ya uchaguzi ya ccm.
"Wana CCM wenzangu naomba tushawishi suala la elimu bure kwa wanafunzi wote wa shule tena elimu bora liwe la kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi" alisema Lowassa na kushangaliwa na mamia ya wananchi wa kata hiyo.
Alisema kuwa ana ndoto hiyo kuwa siku moja elimu itakuwa bure tena elimu iliyo bora, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kujenga usawa wa matabaka kwa taifa letu.
Lowassa ambaye ni miongoni mwa wana CCMinakosemekana yuko katika mbio za kuwania urais uchaguzi ujayo, alisema kuwa kutokana na hali nzuri ya uchumi hivi sasa suala hilo linawezekana.
"Wakati Mzee Mkapa anaingia alikuta madeni mengi sana Serikali yake ikafanya juhudi kulipa na kuanza kukopesheka, Rais Kikwete yeye ameunyanyua uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu na sasa hali ni nzuri kabisa, hebu sasa tuelekeze nguvu katika elimu"alisema na kuongeza iwe kipaumbele cha sasa.

RAGE AGOMA KUITISHA MKUTANO WA DHARURA - ATISHIA KUJIUZULU AMTEUA WAMBURA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI

Hatimaye mkutano wa Mwenyekiti aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage na waandishi wa habari umefanyika leo mchana kama alivyohaidi jana.

Katika mkutano huo Rage amegoma kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama kama alivyoagizwa na Rais wa shirikisho la soka nchini Bwana Jamal Maliniz mapema jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Rage amesema kwamba haoni sababu za kuitisha mkutano mkuu na endapo TFF na Malinzi wataendelea kumshinikiza kufanya hivyo basi atajiuzulu.

Katika hatua nyingine Rage amemteua mwanachama wa klabu hiyo Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba.

Pia, amemteua Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 24, 2013

.
.
.

MAMA YAKE ZITTO KABWE AELEZEA SAKATA LA MWANAYE

Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. 
Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata)

SOMA KWA MAKINI ILE TAARIFA MAALUM YA CHADEMA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU


Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama hicho ya kuwavua nyazifa Naibu Katibu Mkuu,Zitto Kabwe na  Mjumbe wa Kamati Kuu Kitila Mkumbo Katikati ni Mwanasheria wa chama hicho,Tundu Lissu na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa. PICHA | FIDELIS FELIX  
----
 TAARIFA KWA WATANZANIA JUU YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU KUWAVUA NYADHIFA ZA UONGOZI NAIBU KATIBU MKUU, MH. ZITTO ZUBERI KABWE NA WENZAKE 
 
Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA,

         Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya siku ya Jumatano ya tarehe 20 Novemba, 2013 hadi alfajiri ya leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2013 imetafakari na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali juu ya hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama chetu ambayo kwa muda mrefu imegubikwa na tuhuma kubwa na nzito dhidi ya Chama chetu na viongozi wake wakuu, yaani Mwenyekiti wa Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (MB), na Katibu Mkuu, Dk. Wilbrod Peter Slaa. Tuhuma hizi zilikuwa na malengo na athari ya kuwapaka matope na kuwachafua viongozi wakuu wa Chama na Chama chenyewe, kutengeneza mtandao wa siri ndani na nje ya Chama ambao hatimaye ungefanikisha sio tu lengo la kufanya mapinduzi nje ya utaratibu wa kikatiba wa Chama, bali pia ungekipasua Chama vipande vipande na hivyo kuua matumaini ya Watanzania juu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na kijamii katika nchi yetu kwa kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM).

          Ndugu Wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA, Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huu uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi, Bwana Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.

       Kwa mujibu wa waraka wenyewe, “Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji.” Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’ yametoka kwenye ‘Mtandao wa Ushindi’ na hayajabadilishwa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...