Friday, June 21, 2013

Mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema, Joshua Nassari Anendelea Vyema na Matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam

 Mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema, Joshua Nassari akionesha simu yake ya mkononi iliyokuwa na matukio ya tukio la kufavamiwa kwake.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema, Joshua Nassari akiwa katika hospitali ya Taifa muhimbili jijini Dar es Salaam jana akipata matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani jijini Arusha.
Mbunge wa Vunjo-TLP, Mh. Agustino Lyatonga Mrema akimjulia hali mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema, Joshua Nassari.

HII NDIO HISTORIA YA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN ALIYEFARIKI DUNIAI JUZI

Marehemu CHARLES HILILA 

Na Mwandishi Wetu Steven Kanyeph
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo cha television cha chanel ten mkoani Shinyanga, CHARLES HILILA unatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha tinde alikozaliwa.
Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada itayofanyika katika kanisa la mama mwenye huruma la ngokolo mjini shinyanga, ibada inayotarajiwa kufanyika saa nne kamili asubuhi ambayo itakwenda sambamba zoezi la kuaga mwili wa marehemu.

Taarifa kutoka familia ya marehemu HILILA zinasema kuwa baada ya ibada ya mazishi msafara utaelekea katika kijiji cha tinde kwaajiri ya mazishi. Marehemu CHARLES HILILA alizaliwa tarehe 15 mwezi wa 9 mwaka 1964 katika kijiji cha tinde mkoani shinyanga na ni mtoto wa tatu kati ya watoto wanne katika familia ya bwana na bibi BARTHOROMEO HILILA wa kijiji cha mishepo-mwamtini wilaya ya shinyanga.

SERIKALI YA MKOA WA SHINYANGA YATOA TAKWIMU YA UFAULU KWA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI

Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa
Na Steven Kanyeph
Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Bi. Eva M. Lopa ametoa takwimu ya ufaulu kwa elimu ya msingi na sekondari kwa muda wa miaka mitatu kwa mkoa wa shinyanga katika kikao cha taarifa ya elimu kwa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa uliopo mkoani Shinyanga , siku ya jana.

Akitoa takwimu hizo kwa elimu ya msingi Bi. Lopa amesema kuwa matokeo ya elimu ya msingi yamekuwa ya yakipanda mwaka hadi mwaka , na kwa mwaka 2010 yalikuwa ni asilimia 42.5 wakati mwaka 2009 yalikuwa asilimia 31.9 mwaka 2011 matokeo yalikuwa asilimia 44.2 hivyo kuwepo na ongezeko la asilimia 1.7% kwa mwaka 2009 hadi 2011 wakati mwaka 2012 wanafunzi waliofauru ni asilimia 56.1% sawa na ong ezeko la asilimia 11.9

Afisa elimu huyo ameainisha sababu zilizopelekea ongezeko la ufaulu huo kwa mwaka 2012 kwa elimu ya msingi kwa mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa viongozi wa elimu ngazi za wilaya na mkoa , ufuatiliaji wa ufundisha ji, ongezeko la walimu kutoka uwiano wa 1.74 hadi 1.54 na ongezeko la vitabu kwa wanafunzi kutoka uwiano wa f1.6 hadi 1.4

RAIS MSTAAFU WA MAREKANI GEORGE W BUSH KUTUA JIJINI DAR ES SALAAM MWEZI UJAO..!!

 
Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo watahutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake za marais katika kuinua wanawake duniani.
Taasisi ya George Bush  ndiyo imeandaa kongamano  hilo litakalofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 3.
Taarifa iliyotolewa jana na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari, ilisema kongamano hilo, litahudhuriwa pia na mke wa Rais Barack Obama wa Marekani, Michelle na  muasisi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair. 


 Wake wengine wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji),  Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.
Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake za marais  kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU UDSM APIGWA RISASI YA TUMBO USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO YOMBO..!!


Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.


AUNTY LULU..... "MAZISHI YANGU WATAJAA MASHOGA NA WATOTO TU"

MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto
 
 

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi yake.
Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.
“Unajua kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,”alisema Aunty Lulu.

WEMA SEPETU NA KAJALA MASANJA WAGEUKA "PAKA NA CHUI "....ZILE MILIONI 13 ZALETA BALAA ZITO

Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, 

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.

“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?


“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna. “Hapo ndipo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.

 “Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
 “Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.

“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.

MABONDIA WANNE WA TANZANIA WAFUNGWA JELA MIAKA 15 BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI MAURITIUS


Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.
 "Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
 
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea. "Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema

Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.

Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 21, 2013


.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...