Thursday, June 26, 2014

UBABE BUNGENI, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NUSURA AMPIGE KAFULILA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto) akizuliwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutomfuata Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila baada ya kupandwa na hasira kufuatia mbunge huyo kumtuhumu kwa kumuita mwizi kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Kwa ufupi
“Profesa Muhongo aliliambia Bunge kuwa Serikali ililipa fedha hizo ili kuondokana na kesi hiyo lakini ninazo nyaraka za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuteua kampuni mbili za uwakili kwenda kuiwakilisha katika kesi nchini Uingereza,” alisema Kafulila.


Kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema jana angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. 

Sakata hilo lilitokea jana asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni. Jaji Werema alichukia baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili na mwanasheria huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JUNI 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MSEKWA ATOBOA SIRI YA CCM KUNG'ANG'ANIA SERKALI MBILI...!!!


Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa akikusanya baadhi ya vitabu alivyoviandika  alipokuwa akifanya mahojiano na wahariri wa gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. 

Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa ametoboa siri ya chama hicho kung’ang’ania Muungano serikali mbili akisema hiyo ndiyo sera yake pekee iliyopitishwa na wanachama wake wote kwa kura ya maoni.
Msekwa alieleza hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam.
Msekwa ambaye katika habari iliyochapishwa na gazeti hili jana alieleza kuwa binafsi, hana tatizo na suala la idadi ya Serikali katika Muungano, alisema kamwe hawezi kukishauri chama chake kukubaliana na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya muundo wa serikali tatu.
“Siwezi kuishauri CCM kukubali serikali tatu. Hili la Serikali mbili ni sera ya CCM, siyo tu sera ya kawaida, bali hii ni sera pekee iliyopitishwa na wanachama wote kwa kura ya maoni,” alisema Msekwa ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge.
Alisema tofauti na sera hiyo ya serikali mbili, sera nyingine za chama hicho huanzia katika ngazi ya Kamati Kuu, kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WALIOVUNJA 'MOCHWARI' WAPATA DHAMANA

Watu sita kati ya 12 wanaotuhumiwa kwa uchochezi na kuvunja chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kaigara wilayani hapa, jana wamepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama.
Mwendesha mashtaka wa polisi, Cleophace Waane Maatu aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Georgina Angelo, Triphory Joseph, Georgia Triphory, Shafii Abdul, Venanti Benard na Shamim Yusuph.
Aliiambia mahakama kuwa mnamo Juni 16, mwaka huu watuhumiwa hao walifanya uchochezi na kuvunja chumba cha maiti cha kituo hicho na baadaye kutoa mwili wa binti aliyedaiwa kufariki na kunyofolewa viungo vya mwili.
Maatu alisema mtuhumiwa wa kwanza ni shangazi wa marehemu, Georgina Angelo aliyekuwa ametoroka na kukamatwa na polisi kwa kuhusika na uchochezi kwenye mazishi ya binti huyo katika Kijiji cha Bukono wilayani hapa.
Alisema Triphory Joseph na mkewe Georgia ambao ni wazazi wa binti aliyefariki akifanya kazi za ndani mkoani Arusha na Georgina Angelo wanatuhumiwa kwa uchochezi wa kuvunja mochwari ya kituo hicho.
Alisema katika vurugu hizo, pia siku hiyo saa 11:00 jioni walivamia shamba la Valentina Maxmilian na kukatakata migomba pamoja na mazao mengineyo kisha kuchoma nyumba mbili, vitu vyote vikiwa na thamani ya Sh20 milioni.
Watuhumiwa wengine sita hawakutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena Julai 10, mwaka huu.
Kesi hiyo imevuta hisia za wengi kufuatia kifo cha binti huyo kuzua sintofahamu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MLIPUKO WAUA WATU 21 NA KUJERUHI 50 NIGERIA



Moto ukiteketea kulikolipuka bomu nje ya kituo cha biashara Abuja, Nigeria.

Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.

Taswira ya majonzi na kilio ilitanda katika mji wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine kuishia mauti.

Bomu hilo lililipuka mbele ya kituo kikubwa cha biashara, kinachotembelewa na watu wengi.

Walioshuhudia walisema sehemu za miili ya wanadamu zilitapakaa kila mahali sakafuni.

Magari yalichomeka kabisa na vioo katika madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu kuvunjika vyote. Watu waliokuwa na hofu walielekea kwenye mahospitali yaliyo karibu ambapo walishuhudia magari ya wagonjwa yakisongamana kila mahali yakiwaleta wagonjwa na miili ya waliokufa.

John Tobi Wojioa aliwasili mahali hapo muda mfupi baadaye akimtafuta jamaa wake. Alitaja alichoona kama mafuriko ya damu:

"Kulikuwepo magari ya wagonjwa wa shirika la FRCS (federal Road Safery Corps) na ya mashirika mengine yaliyokuwa yakiingia na kuondoka yakibeba miili ya waathirika. Kwenye barabara alama za damu za nyayo za wanadamu zilionekana kila mahali," alisema Bwana Wojioa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...