Thursday, June 26, 2014

WALIOVUNJA 'MOCHWARI' WAPATA DHAMANA

Watu sita kati ya 12 wanaotuhumiwa kwa uchochezi na kuvunja chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kaigara wilayani hapa, jana wamepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama.
Mwendesha mashtaka wa polisi, Cleophace Waane Maatu aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Georgina Angelo, Triphory Joseph, Georgia Triphory, Shafii Abdul, Venanti Benard na Shamim Yusuph.
Aliiambia mahakama kuwa mnamo Juni 16, mwaka huu watuhumiwa hao walifanya uchochezi na kuvunja chumba cha maiti cha kituo hicho na baadaye kutoa mwili wa binti aliyedaiwa kufariki na kunyofolewa viungo vya mwili.
Maatu alisema mtuhumiwa wa kwanza ni shangazi wa marehemu, Georgina Angelo aliyekuwa ametoroka na kukamatwa na polisi kwa kuhusika na uchochezi kwenye mazishi ya binti huyo katika Kijiji cha Bukono wilayani hapa.
Alisema Triphory Joseph na mkewe Georgia ambao ni wazazi wa binti aliyefariki akifanya kazi za ndani mkoani Arusha na Georgina Angelo wanatuhumiwa kwa uchochezi wa kuvunja mochwari ya kituo hicho.
Alisema katika vurugu hizo, pia siku hiyo saa 11:00 jioni walivamia shamba la Valentina Maxmilian na kukatakata migomba pamoja na mazao mengineyo kisha kuchoma nyumba mbili, vitu vyote vikiwa na thamani ya Sh20 milioni.
Watuhumiwa wengine sita hawakutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena Julai 10, mwaka huu.
Kesi hiyo imevuta hisia za wengi kufuatia kifo cha binti huyo kuzua sintofahamu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...