Thursday, January 02, 2014

MWANAJESHI AUA VIJANA WAWILI KWA BASTOLA

Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), ambaye jina lake limehifadhiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kuwaua kwa kuwapiga risasi vijana wawili na kisha kuwajeruhi vibaya wengine wawili walipokuwa katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya. Tukio hilo lilitokea majira ya saa sita na robo usiku wa kuamkia jana, katika eneo la Pugu Kinyamwezi, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi (pichani) alisema tukio hilo lilitokea baada kundi la vijana waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kuzingira gari la mwanajeshi huyo aliyekuwa akielekea nyumbani kwake Pugu Kinyamwezi, akitokea katikati ya Jiji kwa shughuli zake.
Alisema mwanajeshi huyo alikuwa na gari aina ya Toyota Rava 4 na baada ya kufika katika eneo hilo alizingirwa na kundi la vijana hao waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya na ndipo aliamua kutoa bastola yake na kufyatua risasi ambapo iliwapata vijana hao na kufa papo hapo na kujeruhi wengine.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

RAY C AFUNGUKA KUHUSU JACK CLIF... ASEMA WACHA AFE TU TENA ANYONGWE KABISA...!!!


Kutokana na maswahibu makubwa yaliyompata Ray C juu ya madawa ya kulevya, ameshindwa kujizuia kutokusema ya moyoni mwake juu ya mwanadada Jack Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China. Kafunguka maneno mengi sana na alionyesha ni jinsi gani alivyokuwa hamuonei huruma mwanadada Jack mpaka kuamua kutamka bora anyongwe tu. 

Soma alichokisema hapa
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 02, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA ULIVYO SASA MARA BAADA YA MECHI ZA JANA

 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

LOWASAA ATANGAZA KUANZA RASMI SAFARI YA NDOTO ZAKE...!!!

lowassa 9c1c5
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Akizungumza katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.
Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.
"Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu,'' alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe kanisani.
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

HII NDIO HISTORIA NZITO NA FUPI YA MAREHEMU DK. MGIMWA...!!!

 Historia fupi ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kuzaliwa: Januari 20, 1950 Kalenga Iringa.
Elimu:
1961 -1965 Shule ya Msingi Wasa
1966 - 1967 Shule ya Msingi Tosa
1968 - 1969 Tosamaganga Sekondari

1970-1971 Seminari ya Mafinga
1975 - 1984 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) - Postgraduate in Finance
1989 - 1991 IDM Mzumbe (MBA - Finance)

Ajira
1981 - 2000 - NBC Ltd (Mhasibu, Mhadhiri, Mkurugenzi, Mkurugenzi Mkuu)
2000 - 2010 - Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania Mwanza (Mkuu wa Chuo)
2010 - 2013 - Mbunge, Kalenga (CCM)

Waziri wa Fedha,Dkt. William Mgimwa (pichani) alifariki Dunia Januari 1, 2014 katika Hospitali ya Mediclinic Kloff,alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...