Tuesday, August 11, 2015

SHERIA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 01

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa siku zao zinahesabika kwani ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya Uhalifu wa Mitandao itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.

Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo, bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kwa watu maarufu.

“Napenda kuwatahadharisha Watanzania na watumiaji wa mitandao hii kwa ujumla kuwa sheria hii si ya kupuuzwa, kwani kwa hali ilivyo wengi watatozwa faini na watashindwa kulipa na kuishia gerezani,” alisisitiza. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

MBOWE: NAENDELEA VIZURI



Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe 


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe amesema uchovu ndiyo sababu iliyomfanya kuugua ghafla jana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, kuchukua fomu jana, Mbowe aliugua ghafla eneo la Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili ambako amelazwa hadi leo.



Hata hivyo, mwanasiasa huyo ambaye anawania ubunge katika jimbo la Hai kupitia Chadema amewahakikisha wanachama na wafuasi wa Ukawa kuwa afya yake ni njema na huenda akaruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 48.

Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminieli Aligaesha pamoja na kukiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo, hakutaka kuweka hadharani kilichokuwa kinamsumbua Mbowe. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

DK. BILALI APUUZA UVUMI WA KUIHAMA CCM

MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amekanusha taarifa za uzushi ziliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana, Katibu wa Makamu wa Rais, Zahor Mohammed Haji kwa niaba ya Dk Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina yake. Zahoro alisema, Dk Bilal yupo nchini Uingereza katika shughuli za ujenzi wa taifa na kwamba hana mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza uzushi huo wana lao jambo.

Katibu huyo amemnukuu Dk Bilal akisema; “Ndugu zangu wa CCM, na Watanzania kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwa taarifu kwamba kuna taarifa inayoenezwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook na whatsApp kuwa nitaitisha mkutano na vyombo vya habari ili kujitoa CCM.

MAGUFULI ATAKA KAMPENI ZA KISAYANSI KUPATA USHINDI WA TSUNAMI

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara nje ya ofisi ya CCM jana. Picha na Ofisi ya CCM 

Waziri wa Ujenzi na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa, kata majimbo, wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni wa tsunami,” alisema Dk Magufuli. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

LOWASSA AIPAGAWISHA DAR, CHUKUA FOMU YA URAIS NEC


MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vingine vitatu vya upinzani vinavyounda umoja unaofahamika kwa jina la Ukawa, Edward Lowassa jana alichukua fomu za kuwania rasmi nafasi hiyo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiunga Chadema hivi karibuni baada ya kushindwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, sasa ameungana na wagombea wengine kujitokeza NEC kuchukua fomu za kuwania urais.

Ametanguliwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa. Wengine ni Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, Mac-Millan Lyimo wa TLP, Hashim Rungwe wa CHAUMMA, Chifu Lutasola Yemba wa ADC na Dk Godfrey Malisa wa CCK. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 10, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...