Sunday, October 12, 2014

MJUMBE WA NCCR AWATESA VIGOGO...!!!


“Kutokana na alichofanyiwa kwa kupigiwa kura bila huku akiwa hajafanya hivyo tumemwandikia barua IGP tukimwomba amwekee ulinzi (Hamis) kwani kwa siasa za Pemba (anakoishi Hamis) wanaweza kumdhuru.” PICHA|MAKTABA 

Siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi- Zanzibar, Haji Ambar Hamis kutoa tuhuma za ‘kupigishwa’ kura ya kupitisha Katiba inayopendekezwa bila ridhaa yake, uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba umethibitisha kuwapo kwa dosari hizo.
“Sikuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye kupitisha katiba hiyo. Ukweli ni kwamba nimeumia sana na hadi sasa sielewi hatma ya maisha yangu na usalama wa familia yangu kwa ujumla” alisema Hamis alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Akizungumzia tuhuma hizo za Hamis, Naibu Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Dk Thomas Kashililah alisema: “Kwa taarifa zetu hakupiga kura siku zote tatu za zoezi hilo. Jina lake katika orodha ya wapiga kura lilikuwa namba 63 na hakupiga kura.”
Alisema hata hivyo wakati wa kuondoa majina ya Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wale ambao hawakushiriki jina lake lilisahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NYARANDU: HAKUNA TEMBO ALIYEUAWA SELOUS HIVI KARIBUNI


Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu. PICHA|MAKTABA 

Serikali imesema vita vya kupambana na ujangili vinaonyesha mafanikio katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita na hakuna taarifa za kuuawa kwa tembo katika Pori la Akiba la Selous.

Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu alisema jana wakati akiaga wanafunzi zaidi ya 100 kutoka China na Tanzania Makao Makuu ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) waliokwenda kutembelea pori hilo kubwa kuliko yote barani Afrika kupata mafunzo ya uhifadhi.

Alisema baada ya serikali kuvalia njuga suala la ujangili wananchi wameelimika na sasa wamekuwa wakitoa taarifa za majangili ambazo zimesaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na ujangili.

“Baada ya Rais Jakaya Kikwete kukerwa na kukithiri kwa majangili tulianza mapambano na taarifa nilizonazo hadi hivi sasa kwa kipindi cha miezi mitatu hakuna tembo hata mmoja aliyekutwa ameuawa,”alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POSHO ZA BUNGE ZAIBUA MAPYA


Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta. PICHA|MAKTABA

Siku chache baada ya Bunge la Maalumu la Katiba kumaliza muda wake, matumizi ya fedha zilizobaki kwenye Bunge hilo yameibua mvutano baada ya kuwapo taarifa kuwa fedha hizo ziliisha, huku Wizara ya Fedha ikieleza kuwa bado zipo.
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 12, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI ‘ YACHAPWA’ KWA MARA YA KWANZA NA POLAND

Poland imeifunga UJerumani kwa mara ya kwanza na kukwea juu ya kilele katika kundi la Nne kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016 nchini Ufaransa. Mabingwa wa dunia , Ujerumani ilikuwa na rekodi ya kucheza mara 18 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya majirani zao, Poland ambao walipata mabao yote mawili katika kipindi cha pili.
Mshambulizi kinda wa klabu ya Ajax Amsterdam, Arkadiusz Milik, 20 alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 51, na dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Sebastian Mila aliwahakikishia wenyeji ushindi baada ya kufunga bao la pili katika mchezo huo uliopigwa jijini, Warsaw.
Mabingwa hao wa sasa wa dunia, walifungwa mara ya mwisho na Jamhuri ya Czech, Oktoba, 2007 katika michezo ya kufuzu. Ujerumani ilicheza michezo 33 ya kufuzu pasipo kupoteza. Kipa wa Ujerumani, Manuer Neur aliokoa mabao manne ya wazi katika mchezo ambao walishambuliwa sana. Poland iliyokuwa na mshambulizi wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ilipiga jumla ya mashuti 19, huku mashuti 12 yakilenga bao.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alikwenda Poland huku baaddi ya wachezaji wake muhimu wakikosekana. Ujerumani ilibanwa hasa na walimudu kufanya mashambulizi machache . Walipiga mashuti saba tu ambayo yote yalilenga lango lakini nyota wa mchezo huo, golikipa, Wojciech Szczesny alikuwa imara, kipa huyo wa klabu ya Arsenal aliokoa mara 14. Tomas Mueller, Andre Schurrle na Mario Gotze walishindwa kufunga kwa muda wote waliokuwa uwanjani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UFARANSA YAICHAPA URENO NA C.RONALDO AKIWEMO

Mshambulizi Karimu Benzema alifunga bao la mapema na akatengeneza lingine kwa kiungo Paul Pogba katika kipindi cha pili na kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ureno. RicaRrdo Quaresma alitokea benchi katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Luis Nani katika dakika ya 68, alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika tisa baada ya kuingia uwanjamni .
Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa fainali zijazo za Ulaya waliifunga Ureno ambayo ilikuwa na mshambulizi wake mahiri na mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo katika mchezo uliofanyika jijini Paris. Ronaldo alipiga mashuti manne katika mchezo huo lakini ni shuti moja tu ambalo lilikuwa na uhai. Timu zote zilicheza mchezo wa kufanana, Ufaransa walipiga mashuti 12 sawa na waliyopiga Ureno, lakini wageni walifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ambayo yalimsumbua golikipa, Steven Mandanda.
Eliaguim Mangala, RAfaer Varane, Patrice Evra na Bacary SAgna walianza katika safu ya ulinzi na wanne hao hawakuwekwa majaribuni na kikosi kilichopoteza makali cha Ureno. Ronaldo alitoka uwanjani dakika ya 76 akimpisha Jose Mario alianza sambamba Danny na Nani katika safu ya mbele lakini watatu hao hawakuwa tishio kwa Ufaransa ambao walicheza jumla ya faulo 15 katika mchezo huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SITI MTEMVU NDIYE REDD'S MISS TANZANIA 2014

Miss Tanzania 2014, Siti Abass Zuberi Mtemvu akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililoshirikisha warembo 30 na kufanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Siti Mtemvu ametwaa taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Happyness Watimanywa.

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.

Redd's Miss Tanzania aliemaliza muda wake, Happiness Watimanywa akimpisha crown, Redd's Miss Tanzania wa sasa, Sitti Mtemvu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz




Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM LAWAACHIA MATEKA 27

boko haram
Rais wa Cameroon amesema kuwa mateka 27 wakiwemo raia 10 wa Uchina wameachiliwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.
Raia hao wa China walitekwa nyara mwezi mei wakati kampuni moja ya China ilipovamiwa karibu na mpaka wa Nigeria.
Wengine walioachiliwa ni pamoja na mke wa naibu waziri mkuu nchini Cameroon aliyetekwa nyara mwezi Julai.
Haijulikani iwapo fidia ililipwa.
Boko haramu wameeneza mashambulizi kutoka nchini Nigeria kwenda kaskazini magharibi mwa Cameroon. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...