Wednesday, January 14, 2015

TANZANIA KUIKABILI KENYA BEACH SOCCER

Soka la ufukweni 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) imepangiwa kucheza na Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili ya fainali za Afrika ambapo michuano hiyo itafanyika Aprili mwaka huu nchini Shelisheli.
Mwenyekiti wa Kamati ya Beach Soccer, Ahmed Idd Mgoyi amesema jijini Dar es Salaam, kuwa Tanzania itaanzia ugenini ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu nchini Kenya.
Mechi ya marudiano itafanyikaa Tanzania kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu. Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele, katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na 15 mwaka huu.
Mgoyi alisema maandalizi ya Tanzania kushiriki kwenye mashindano hayo yameanza ambapo timu ya Tanzania Bara itacheza na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata kikosi kimoja kitakachoingia kwenye michuano hiyo ya Afrika.
Benchi za ufundi la timu ya Tanzania litaongozwa na John Mwansasu wakati Msaidizi wake ni Ali Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu hiyo ni George Lucas. Wote hao walishiriki kwenye kozi ya ukocha wa beach soccer iliyoendeshwa mwaka jana nchini na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kocha Mwansasu atatangaza timu ya Tanzania Bara, Januari 19 mwaka huu, na mazoezi ya pamoja na timu ya Zanzibar yatafanyika Januari 24 na 25 mwaka huu.
Wachezaji wa timu ya Tanzania Bara watatokana na michuano ya beach soccer iliyofanyika mwaka jana ikishirikisha timu za vyuo vya elimu ya juu vya Mkoa wa Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...