Sunday, April 28, 2013

GARI JIPYALA MILIONI 35 ALILONUNUA NEY WA MITEGO PAMOJA NA BASTOLA HAPA

Mwaka 2013 ni mzuri kwa rapper Nay wa Mitego. Licha ya kuwa na hit single hewani, Muziki Gani aliyomshirikisha Diamond, rapper huyo amenunua ndinga mpya aina ya Mark X yenye thamani ya shilingi milioni 35. Kama hiyo haitoshi, hitmaker wa Nasema Nao, amejihami pia kwa kununua bastola.
29ddba2cae6b11e2aeda22000a1f973b_7


Nay akiwa na bastola yake
Nay akiwa na bastola yake
Nay ameshare picha hizo kwenye Instagram na Facebook ambapo miongini mwa picha za gari lake ameandika, ‘My new car. Mark X, Zic z wat I nid.” Mwaka huu Nay ametumiwa kwenye show nyingi za Airtel na Vodacom ambazo huenda zimemwingizia mkwanja wa kutosha.
23a19536ae6e11e2942122000aaa0535_7

82d44f72ae6d11e2a2ce22000a1fa411_7

a2364980ae6b11e2b9ed22000a1f8cd8_7

d07e1cfaae6b11e2b09522000a1f9363_7

dc3c1784ae6d11e28c1022000a9e08e0_7


MBUNGE LEMA AZUILIWA KUPIGA MSWAKI WALA KUNYWA CHAI AKIWA MAHABUSU...... !!

TUKIO la kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo,
 
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
 
Mbunge huyo alikamatwa kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyedai kuwa aliwachochea wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea kiongozi huyo na kupopoa gari lake kwa mawe.
 
Hata hivyo, siku moja kabla ya kukamatwa Lema aliwaonesha waandishi wa habari ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani aliyotumiwa na Mulongo akimtishia kuwa atamfungulia kesi yoyote anayoitaka.
 
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.

MSANII SIZE NANE ALILIA BIKRA YAKE HADHARANI...!!

Mwanamuziki  aliyeitikisa vilivyo Kenya kabla ya kuokoka na kuachana na muziki wa kidunia, mwanadada Size 8 sasa ameanza kufunguka katika interview kwenye vituo mbali mbali vya redio na Tv kuhusiana na maisha mapya ya kidini.

Kati ya  mambo yote ambayo Size 8 amekuwa akiyaongelea, ni moja tu ambalo amekuwa akilitilia mkazo kwa kumaanisha kuwa linamsikitisha zaidi .....Jambo hilo ni lile la kupoteza BIKRA YAKE.....
Size 8 ameziambia media kuwa  "Najutia sana kupoteza bikra yangu. Ninaamini kuwa kijana anatakiwa kujilinda na kujizuia kufanya ngono katika ujana wake wote mpaka atakapo pata kibali toka kwa Mungu."

KIONGOZI WA KANISA AZIKWA AKIWA HAI

26 46e3f
Msaidizi wa zamani wa Padri (Katekisita) katika Kigango cha Kanisa Katoliki Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa baada ya kuzikwa akiwa hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua kwa njia ya kishirikina.
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alikiri kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa lilitokea saa 9:00 mchana katika kijiji hicho cha Maweni Mkwajuni wilayani Chunya.

"Marehemu aliuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na mawe kwa tuhuma za kuhusika na uchawi na kusababisha kifo cha Peter Robert," alisema.
Kamanda Athumani alisema kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na kwamba wahusika wote wa tukio hilo wamekimbia na kuzihama nyumba zao, hivyo polisi wanaendelea na msako wa kuwatia mbaroni watuhumiwa na kwamba tayari kaburi hilo limefukuliwa jana kutenganisha maiti hizo.

WEMA AFUNGUKA INSTAGRAM BAADA YA KUSOMA MOJA YA GAZETI KWAMBA ANA BEEF NA LULU

BEYONCE AWAPIGA MKWARA WAPIGA PICHA, HIKI NDO ALICHOKISEMA

Baada ya kukerwa na picha alizopigwa wakati wa tamasha la SuperBowl ambazo anaona zilimdhalilisha, mwanamuziki Beyonce amefikia maamuzi magumu ya kuwakataa wapiga picha

Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa kwenye ukurasa wa facebook wa Umoja wa Wapiga picha za Muziki imeeleza kuwa mwanamuziki huyo haitaji tena wapiga picha katika shoo za ziara yake ya sasa ya Ulaya

Badala yake amekuwa akitoa picha rasmi zilizopigwa kutoka katika shoo na wapiga picha maalum aliowakodisha.

MAGAZETI YA LEO APRIL 28 2013 KURASA ZA MWANZO NA MWISHO

.

.
.
.

Mawaziri, wabunge CCM warushiana 'makombora'



Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jana walishambuliana huku waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali katika vikao vya bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma wakituhumiwa kukiua chama na kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kikao hicho ambacho kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilifanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

Pinda alianza kwa kuweka hoja mezani akitaka wabunge wa CCM kuchangia Sh.100,000 kila mmoja kwa ajili ya kuwezesha ushindi katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika katika kata 26 nchini.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge hao, lakini alisimama Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Khangi Lugola, akihoji kulikoni wanaosaidiwa na chama wakawa madiwani ili hali wabunge walio na kesi mahakamani wakiachwa kugharamia kila kitu wenyewe.
“Si unajua nyoka wa shaba (Lugola), ana kesi mahakamani, sasa ndiyo maana akaamua kuhoji, iweje yeye hasaidiwi na chama wakati huo huo anaambiwa akisaidie chama,” alisema mmoja wa wabunge aliyekuwa ndani ya kikao hicho.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...