Wednesday, July 03, 2013

MJUKUU WA MANDELA AFIKISHWA MAHAKAMANI....!!!

Jamaa za familia ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, wamewasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya mjukuu wa Mandela,Mandla Mandela.
Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na sheria
Mwendesha mashtaka wa umma, kisha ataamua ikiwa amshtaki Mandla au la.
Inahusisha maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita.
Katika kesi nyingine, jamaa kumi na sita wa familia ya Mandela, wanataka kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki iliakhirishwa hapo jana kuanza kusikilizwa leo.
Wiki jana, mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa kutoka nyumbani kwa Mandla katika kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa kilomiya 22.
Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 3, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0015 775bb


DSC 0012 90b4b

SIFA ZA GARI YA OBAMA INAWEZA KWENDA 97KM TU KWA SAA AT MAXIMUM ..... YA JK IPO JUU KWA SPEED

 
Walioona msafara wa obama wataona namna msafara ulipita kwa speed ya kawaida sana tofauti na ile speed tuliyozoea anapopita JK, our president normally huwa ana cruise at an average of 120kmh.

Ile speed ikanifanya nitafute habari zaidi, niliyoyaona yamenishangaza, kumbe
Maximum speed ya limo ya obama ni 60mph tu, sawasawa na kilimita kama 97 kwa saa. hii gari haina ujanja wa kwenda hata 100km kwa saa, hata boda boda inaweza kwenda speed kuliko hii gari

  1. ina uzito unaokadiria kukaribia tani 9
  2. matumizi ya mafuta ni 8mpg, kwa lugha ingine inahitahi lita 35.31 ili kutembea kilomita 100, hii ni sawa na lita 1 kwa kila kilomita 2.8
  3. vioo vyote havifunguki isipokua pale kwa dereva kwa mbele. gari iko 100% sealed
  4. Vioo vya dirishani vina thickness ya inchi 5 wakati milango ni nchi 8.
  5. kutokana na unene wa madirisha na milango, obama hawezi kusikia chochote kinachoendelea nnje, spika zimewekwa ili kunasa sauti za nje
  6. gari ina night vision kamera zinazomuwezesha dereva kuendesha usiku bila hata kuwasha taa

OBAMA AAHIDI KUJA TENA NA KUPITA MITAANI ILI WATU WAMUONE...!!!

Kana kwamba alisikia kilio cha wakazi wa Dar es Salaam waliokuwa na shauku ya kumwona lakini ikashindikana, Rais Barack Obama wa Marekani amewaomba radhi kwa hali hiyo.
Akizungumza juzi wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa ajili yake na ujumbe wake na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam, Obama alisema akirudi nchini siku zijazo, atapita mitaani akiwa katika gari la wazi.


"Niliona wananchi walivyojitokeza kwa wingi kutupokea barabarani, nilifarijika sana lakini hawakuweza kutuona vizuri kwani tulikuwa ndani ya gari maalumu-The Beast.

"Miaka ya sitini Rais John Kennedy alipokuja hapa, alipita na gari la wazi mitaani wananchi wakamwona, naomba radhi nikija tena nitaonekana," alisema Obama.

Watu wengi waliozungumza na vyombo vya habari walionesha dhahiri kiu ya kutaka kumwona Rais huyo wa kwanza mweusi wa Marekani, lakini wakaishia kuona gari lake ambalo hata hivyo, lilipita kwa kasi barabarani kwenda Ikulu na kurudi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA DAUD MWANGOSI WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA...!!!

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mufindi imetupilia mbali mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Hamad Yusuph na wenzake 42.

Kiongozi huyo pamoja na wenzake walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu likiwemo la kufanya mkutano bila kibali pamoja na kuharibu mali ambazo ni kofia za pikipiki (helmenti) 2 za polisi katika tukio lililosababisha kuuawa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daudi Mangosi katika kijiji cha Nyololo wailayani Mufindi.

Kutokana na tuhuma hizo Chadema iliweka pingamizi za kutaka kesi hiyo ifutwe kwa kuwa ilifunguliwa kinyume cha sheria.

Wakili wa Chadema Lugaziya akisaidiana na mwanasheria wa Chadema Luka Sinkala Mwenda waliweka pingamizi kuwa aliyetoa amri ya kusitisha mkutano na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari huyo ni kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda ambapo aliingilia kazi ya OCD wa Mufindi kwa kuwa hakupaswa kutoa amri hiyo, kwamba wakati amri ya kusitisha mkutano ilitolewa wakati hakukukuwa na vurugu na polisi walipiga mabomu wakati watu wanatawanyika.

Pingamizi zingine ni kwamba aliyetoa amri ya kutawanya mkutano hakuwa na cheo chochote.Wakati Chadema ikizuiliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Bububu Zanzibar walikuwa na mkutano wa kampeni za uchaguzi..

STOKE CITY YAKAMILISHA DILI YA KUMSAJILI MARC MUNIESA KUTOKA BARCELONA

 
Marc Muniesa, Beki wa timu ya Barcelona aliyesaini mkataba wa kuichezea Stoke City Msimu ujao

Aliyekuwa beki wa Timu ya Barcelona ya Uhispania Marc Muniesa kijana wa Miaka 29 amekamilisha Usajili wake wa kuicheza timu yake mpya ya Stoke City ya Uingereza.

Marc Muniesa alikuwa ni moja wa memba wa kikosi cha Hispania chini ya Miaka 21 kilichoshinda Katika ligi ya Ubingwa wa ulaya chini ya Miaka 21.

Marc Muniesa, alisema " anafurahi kujiunga na timu ya Stoke City na atajitahidi kadri ya uwezo wake katika kuhakikisha timu yake hiyo mpya ya Stoke anailetea Ushindi"

Aliongezea kwa kusema Hakuwa na uamuzi mgumu katika kuamua kujiunga na timu hiyo ya Uingereza ya Stoke City na nimekuja uingereza jana kwaajili ya kukutana na watu wa klabu hii ya Stoke City na kuangalia Uwanja wa Mazoezi na kuona unavutia

MACHANGUDOA WALALAMIKIA UJUO WA OBAMA WASEMA AFADHALI UJIO WA BUSH:

Rais Barack Obama wa Marekani

Polisi wa Kimarekani waliokuwa mwiba mkali kwa ulinzi wa Obama

Machangudoa wakiwinda wazungu maeneo ya Oysterbay Karibu na Ubalozi wa Merikani

Machangudoa wakiwa kazini

Na Livingstone Mkoi

Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida wakina dada maarufu wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao maarufu kwa majina ya machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kilichodaiwa haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa.

Wakiongea Xdeejayz kwenye baadhi ya sehemu wanazopatikana wakina dada hao walisema kuwa” Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana lakini patutu kwani watu wake tuliokuwa tumewategemea kuwanasa walikuwa busy na usalama pia kukaa kipindi kifupi kumechangia sisi kukosa mapato" Walisema wakina dada hao waliokutwa maeneo ya Coco Beack

Aidha machungudoa hao waliongeza kusema kuwa kipindi cha Bush ambae alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Busha kwani walifanikiwa kuwanasa watu wake na kufanya nao biashara kwa bei nzuri.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...