Tuesday, July 23, 2013

MASELA WAUWANA KWA MARUNGU KISA DEMU WA KISUMKUMA...!!!


Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.

Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.


Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.


Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya. 


Source: Watemi

MAGAZETI YA LEO JULY 23, 2013


DSC 0061 f2b62
DSC 0062 6a196

KIKWETE AWATAKA UMOJA WA MATAIFA KURUHUSU SILAA KATIKA OPERATIONI ZAO



Rais Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu askari waliouwawa huko Darfur wakitekeleza majukumu ya umoja wa mataifa ya kulinda amani.


Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa Tanzania waliokuwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya UN na Afrika (Unamid) ambao waliuawa na kundi linalodaiwa la wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na Serikali ya Sudan inayoongozwa na Rais Omar al-Bashir.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).
“Lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya vijana wetu ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini watu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezesha wafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao?
“Moja kwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na watu wote walioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. UN ifanyie marekebisho sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu za kujihami ili kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza.”

GODBLESS LEMA AFYATUA KOMBORA LINGINE....!!!




CHAMA cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami kwa vijana wao maarufu kama Red brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka huu.

Akitangaza tarehe hiyo jana wakati wa mkutano wa chama hicho uliofanyika Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini, kiongozi wa ulinzi wa chama hicho kanda ya Nyanda za juu kusini Lucas Mwampiki, alisema kuwa ameamua kuweka wazi adhima hiyo ili serikali isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa kuwazuia.

‘’Polisi msisumbuke kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa nane mwaka huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.

TAIFA STARS KUIFUATA UGANDA 'THE CRANES' JUMATANO, KUKIPIGA JUMAMOSI

 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.

HAWA NDIO ASKARI WALIOKUFA DARFUR WAKILINDA AMANI - MUNGU ZILAZE ROHO ZAO PEMA PEPONI AMINA


 MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...