Tuesday, August 05, 2014

MJUMBE WA UKAWA ATINGA BUNGENI...!!!

Bunge  

Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni.
Baadaye alipoulizwa imekuwaje akajiandikisha ilhali uongozi wa chama chake umesema hawatashiriki, Mwatuka alijibu: “Kwa hapo ni mapema sana kuzungumzia suala hilo, nitazungumza kesho (leo) kule bungeni ukinitafuta.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ISRAEL NA HAMAS KUSIMAMISHA MAPIGANO?

Mwanajeshi wa Israel
Israel na Hamas yamekubaliana kufuata maombi ya Misri ya kusimamisha mapigano kwa siku tatu huko Gaza, kuanzia leo jumanne asubuhi.
Israel inasema kuwa itakubaliana na mpango huo bila ya masharti yoyote.
Nayo Misri inasema kuwa muafaka huo unafaa kufuatiwa na mazungumzo ya amani yenye nia ya kuboresha kabisa usalama.
Majeshi ya Israeli awali yalirejelea operesheni kali zaidi huko Gaza, baada ya kumalizika kwa makataa ya saa saba ya kukomesha mapigano. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BENKI YA DUNIA YASAIDIA EBOLA

Wahudumu wa afya katika tahadhari ya kukabiliana na Ebola
Benki ya Dunia imetangaza kutoa msaada wa hadi dola milioni mia mbili, kutoka mfuko wa dharura wa msaada, ili kuzisaidia mataifa matatu ya Afrika magharibi kukabiliana na ugonjwa hatari wa ebola.
Pesa hizo zitasaidia Liberia, Sierra Leone na Guinea, ili kuboresha vifaa vya afya ya umma na kushughulikia matatizo ya uchumi yaliyosababishwa na ugonjwa huo.
Rais wa Bank ya Dunia Jim Yong Kim amesema amehuzunishwa sana kwa jinsi Ebola unavyoendelea kuvuruga mfumo wa afya kwa nchi tatu.
Kwa mwaka huu pekee karibu watu mia nane na tisini wamekufa kutokanana Ebola katika nchi za Afrika Magharibi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAGE APATA AJARI DODOMA...!!!

adenrage
RAIS Mstaafu wa klabu ya Simba Sc  Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, amenusurika kifo na kuumia bega la Kushoto akiwa na watu wengine watatu baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya Toyota Land Cruser T 845 BQS (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la Chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini Dodoma kuanza vikao vya Bunge la Katiba leo.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime, amesema ajali hiyo imetokea jana Agost 4, 2014 na kuwa imetokea katika eneo la Njia panda ya Kigwe katika barabara ya Singida Dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge Maalum la katiba.
 Amesema Rage, ameumia katika bega la kushoto na mgongoni huku Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora, Munde Abdalla Tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 Amesema watu wengine waliokuwepo katika gari hilo ni pamoja na Mwanahamis Athumani, John Hoya ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo. Hata hivyo amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

LIGU KUU KUTANGAZA MASHINDANO MAPYA YA ULAYA KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 21

1407189839139_wps_2_Football_Chelsea_lift_the
Mabingwa: Chelsea wakishangilia kombe la vijana chini ya miaka 21 kutoka timu za ligi kuu msimu wa 2013/14 
MSIMU huu uongozi wa ligi kuu unatarajia kuzindua mashindano mapya ya kombe la ulaya kwa timu za ligi kuu nchini England chini ya miaka 21 na timu kutoka nje ya England.
Vikosi vya vijana chini ya miaka 21 kutoka timu nane (8) za juu katika msimamo wa ligi kuu Engalnd  zikiwemo klabu za Manchester City, Manchester United  na Chelsea vitashiriki pamoja na timu nane (8) kutoka nje ya England ambapo jumla ya timu itakuwa ni 16.
Hii hatua ni kutekeleza mkakati maalumu wa soka la vijana ulioanzishwa mwaka 2011 ili kuwaimarisha vijana wanaozalishwa na klabu za juu za England.
TIMU 16 ZITAKAZOSHIRIKI 
Timu za England: Chelsea, Fulham, Leicester City, Man City, Man Utd, Southampton, Sunderland, West Ham.
 
Timu za Ulaya: Celtic, Athletic Bilbao, Benfica, Borussia Monchengladbach, Schalke, FC Porto, PSV Eindhoven, Villarreal
Liverpool, walioshiriki ligi ya vijana chini ya miaka 21 msimu uliopita hawatashiriki mashindano hayo na badala yake nafasi hiyo imeenda kwa West Ham waliomaliza nafasi ya tisa katika msimamo msimu uliopita.
Mashindano hayo yataenda sambamba na ligi ya vijana chini ya miaka 21. 
Kwa sasa yatawavutia watu wengi zaidi kwasababu Sky Sports na BT Sports watarusha ‘Laivu’ mechi 10.
Waandaaji wana matumaini kuwa michuano hii itawavutia watu wengi na timu zitapata wachezaji wao wazuri ili kuwaingia katika timu za wakubwa.
Mkurugenzi wa akademi ya Schalke ,Oliver Ruhnert  alisaidia kuzalisha wachezaji wanne walioisadia Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka huu na timu yake itashiriki michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 21. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA SC HAWATASHIRIKI KOMBE LA KAGAME 2014, WAGOMA KUBADILI KIKOSI...!!!

126
TAARIFA Mpya usiku huu! Yanga hawatashiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, maarufu kwa jina la Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Agosi 8 mwaka huu,, mjini Kigali, Rwanda.
Hii imetokana na Yanga kugoma kubadili kikosi chao kama walivyotakiwa na CECAFA leo hii.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wamekomaa na kikosi B kama walivyopanga wakati CECAFA wamewataka kwenda na kikosi B.
Awali ilielezwa kuwa Yanga wanatakiwa kubadilisha kikosi hicho kufikia alfajiri ya kesho na kama haitafanya hivyo, basi timu itatolewa kwenye mashindo.
Kwa mana hiyo, mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaweza kupewa nafasi hiyo kama ilivyoelezwa awali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...