Thursday, December 19, 2013

BASI LA HOOD LAPATA AJALI MOROGORO LAUA...!!!

Wakazi wakishuhudia basi la kampuni ya Hood lililopinduka jioni hii maeneo ya Doma, Morogoro.
Upande wa chini wa basi la Hood
Wakazi wa eneo la Doma nje kidogo ya mji wa Morogoro wakitafakari tukio kwa huzuni
Mtu mmoja amekufa na wengine 27 kujeruhiwa baada ya basi la Hood Limited lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Arusha kupata ajali eneo la Melela Mvomero, Mkoani Morogoro. CHANZO East Africa Television (EATV)

MWEKEZAJI WA SHAMBA LA KAPUNGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

rubani wa ndege Andreas Daffee. akipongezana na wakili wake Lweikaza
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewaachia huru watuhumiwa watatu ambao ni Mwekezaji wa Shamba la Kapunga(Kapunga Rice Project) lililopo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya ambao walikuwa wakituhumiwa  kwa mashtaka matatu ambayo ni kula njama,  kumwaga sumu na kuharibu mashamba ekari 557 ya Wananchi.
 
Akisoma hukumu Mhakamani hapo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili watuhumiwa ambao ni Waldeman Veemark ambaye ni meneja wa shamba, Sergei Beacker ambaye ni Afisa Ugani wa kampuni pamoja na rubani wa ndege Andreas Daffee.
 
Mteite alidai kuwa mbali na upande wa mashtaka kuwa na mashahidi 155,ambapo kati yao mashahidi zaidi ya 20 hawakuweza kufika mahakamani huku wengine 9 wakitoa ushahidi wa uongo tofauti na mashtaka yaliyopelekwa.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 19, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


.

TAZAMA PICHA YA NDEGE ILIYOTUA KWA DHARURA KATIKA UWANJA MDOGO WA NDEGE WA ARUSHA BADALA KIA



http://jambotz8.blogspot.com/


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...