Friday, February 14, 2014

MAGAZETI YA LEO SIKU YA WAPENDANAO FEBRUARI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS

.

.  
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

HISTORIA FUPI YA SIKU YA WAPENDANAO AU VALENTINE'S DAY

http://jambotz8.blogspot.com/

Sikukuu ya wapendanao inasherekewa kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka.
Watu wengi wanaosherekea siku hii kwa Nchi za Afrika Mashariki ni vijana walio kati ya miaka 18 hadi 35.
Historia ya sikukuu hii inaanzia miaka mingi jijini, Roma, Italia ikiwa inahusishwa na mtakatifu Valentine au Valentinus aliyekuwa akiishi jijini humo katika karne hiyo. Wakati wa maisha ya mtakatifu Valentine Roma ilikuwa ikitawaliwa na Kaisari, Claudius II, ambaye alipata hisia wakati huo kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyekuwa na mke wala familia. 
http://jambotz8.blogspot.com/
Claudius alilifanyia kazi wazo lake na aliamua kupiga marufuku ndoa zote kwa askari wa nchi hiyo, jambo ambalo halikukubaliwa na mtakatifu, Valentinus. Hivyo Valentinus alichukua jukumu la kukaidi amri ile na kuendelea kuwafungisha ndoa kwa siri maaskari waliokuwa wakitaka kufungishwa ndoa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
 
Haikuchukua muda mrefu, taarifa zilimfikia mfalme, Claudius na alipopata habari hizo aliamuru kukamatwa na kufungwa gerezani na kisha Valentinus aliuawa kwa amri ya Kaisari. Kuna taarifa zinadai kuwa kabla ya kuuawa kwa Valentine wakati huo akiwa amefungwa, mtakatifu Valentine aliandika barua ya salamu kwa binti aliyekuwa amekwenda  kumsalimia gerezani. Na mwisho wa barua kulisomeka maneno yaliyoandikwa ‘From your Valentine’.
Tangu hapo Valentine akawa anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na siku hii ikawa inaadhimishwa duniani kote.
Baada ya kufariki kwa mtakatifu huyo ndipo wananchi wengi duniani wakaamua kuadhimisha siku hii kama sherehe ya kumkumbuka Mtakatifu Valentinus
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...