Friday, July 25, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


1_ba461.jpg
2_a3788.jpg
3_25f32.jpg 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TIBA, KINGA YA UKIMWI VYANUKIA

Watafiti wakitoa sampuli za damu kutoka kwa sokwe mtu katika utafiti wa Ukimwi huko Gabon. Picha ya Mtandao 

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.
“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABAKI YA NDEGE ALGERIA YAONEKANA

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali. Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa. Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. 
Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
 "Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa. Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua" Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...