Friday, March 11, 2016

HATIMAE MAGUFULI AWAPA SAFARI YA NJE MAWAZIRI WAWILI

Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.

Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.

Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MBOWE: NAWALETEA KATIBU MKUU MAKINI

mbowe.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa. 

Akizungumza mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.

Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 11, 2016

20160311_043412 20160311_043507 20160311_043525 
Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MAREKANI YAMFILISI MTANZANIA MUUZA UNGA

SHKUBA
SERIKALI ya Marekani juzi ilitangaza kutaifisha mali za bilionea Mtanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu Shikuba pamoja na mtandao wake wa kimataifa wa biashara ya dawa za kulevya.
Shikuba ambaye ni mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, anamiliki msururu wa biashara kama vile maduka ya kubadili fedha (bureau de change), kampuni za ulinzi, majumba na utitiri wa magari ya kifahari.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani kupitia ofisi yake ya Udhibiti wa Mali Haramu za Raia wa Kigeni (OFAC), Shikuba na taasisi yake wameangukia katika sheria za nchi hiyo za kudhibiti mapapa wa unga wa kigeni (Kingpin Act).

Mbali ya sababu za kisheria, Marekani imesema bilionea huyo amekuwa akitumia faida haramu kutokana na biashara zake chafu kuhonga maofisa wa Serikali ya Tanzania ili asikamatwe na kushtakiwa. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAMU

Marco Rubio na Donald Trump katika mjadala
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani.

Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani.

''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.

Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao.

''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za magaidi ziangamizwe. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

SIMBA YARUDI KILELENI YAINYUKA NDANDA 3-0

Pg 32
TIMU ya soka ya Simba jana ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuinyuka Ndanda FC mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo ya ushindi wa jana yameiwezesha Simba kufikisha pointi 51 na kuwashusha mahasimu wao wa jadi Yanga hadi nafasi ya pili, wakiwa wamejikusanyia pointi 50 huku Azam FC wakibaki nafasi tatu na pointi 47.

Simba wamerejea kileleni kwa kuwazidi mahasimu wao Yanga kwa pointi moja, lakini Wanajangwani hao wapo nyuma kwa mchezo mmoja kutokana na kushuka dimbani mara 21 huku wapinzani wao wakicheza mara 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...