Thursday, May 09, 2013

UWOYA AJISAFISHA KUPITIA JINA LA RAISI, SOMA ALICHOKISEMA HAPA


Irene Uwoya.

STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata. 

Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza.
“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu ningeitwa na rais wa Burundi kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo maana aliniita mwaka 2011 kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu tusingekubalika hadi na viongozi wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,” alisema Uwoya akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kuhusu madai ya wasanii kuwa na tabia chafu.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais  Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri

BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA



Mwimbaji wa Muziki wa Injili Bahati Lusako Bukuku.
MWIMBAJI wa Muziki wa Injili mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia 

Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
 
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
 
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
CHANZO CHA HABARI NI MTANDAO WA GLOBAL PUBLISHERS

KIOJA CHA MWAKA 2013...MWANAUME KWA MWANAUME WAFUMWA LAIVU GEST..Angalia PICHA

Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
Mama Salome akimpa kisago mumewe baada yakumfumania akiwa na Mwita (kushoto) anayedaiwa kuwa shoga



Breaking Newzzzzzzzz......!!! SHEIKH PONDA AHUKUMIWA MWAKA MMOJA



Hukumu ya  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda  imetolewa leo katika mahakama ya kisutu jijini dar es salaam ampapo kahukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.

HUYU NDIE KIJANA ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA


Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka. 
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo,  walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.

DIAMOND ALIWA DENDA KILAZIMA JUKWAANI..........!!!

https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/s480x480/946757_417898488307807_323015544_n.jpg

video

EEHH!!! jamani kina dada mbona mnajidhalilisha kiasi hicho!! ni pombe ulilewa au kitu gani!?? au ndio mambo ya NATAKA KULEWA hayo ukaamua ummwagie radhi mtoto wa mwenzio kilazima, au huna habari KAMA MCHUMBA WA MTU HUYO DADA!!?? mmmh!! WATOTO WA UK MMETISHA!!!
ALAFU nimesikia kuna mdada kaenda kulala na dancer wa DIAMOND akizani ni DIAMOND MWENYEWE biatchhh! yereeeuwiiiiiiii!!!!!! 
tunaendelea kuifatilia kwa ukaribu tutawaletea picha kamili sooooon!!! 


MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 09.05.2013

1 e393b

9 a92f7

4 4f896

3 7eac3

HUYU NDIYE ANAYETARAJIWA KUWA MRITHI WA MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON PALE OLD TRAFFORD


Kuna taarifa kuwa mabingwa wa England, Manchester United wameanza mazungumzo na Kocha wa Everton, David Moyes.


Man United wanataka Moyes achukue nafasi ya Alex Ferguson ambaye ametangaza kustaafu mara baada ya msimu huu kwisha.


NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013

Coat of arms of Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alitangaza nafasi za ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka 2012/2013 ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ilikuwa tarehe 10 Mei, 2013. Kwa tangazo hili Wananchi wanajulishwa kuwa muda wa kuwasilisha maombi hayo umeongezwa hadi tarehe 20 Mei, 2013.  Aidha inasisitizwa kuwa hata wahitimu wa mwaka 2012 wanapaswa kutuma maombi yao kwa sababu hakutakuwa na utaratibu wa wahitimu kupangiwa vituo vya kazi moja kwa moja.Maombi hayo yaendelee kuwasilishwa kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani iliyopo chini ya tangazohili. 

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

KAIMU KATIBU MKUU,

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM.

MBUNGE GODBLESS LEMA NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MULONGO USO KWA USO LEO ........... WAONE WALIVYOCHUNIANA


p1 6ed46


photo

Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu Katikati akiwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kushoto na Mkuu wa mkoa wa Arusha Maggesa Mulongo wakati wakikabidhi misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa bomu kwenye hospitali ya St.Elizabeth jijini Arusha Leo Asubuhi

HakiElimu YAKATAA KUFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na muungano wa asasi tano za kiraia uliowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Elizabeth Missokia.

Asasi zilizotoa tamko la pamoja huku zikipendekeza njia sahihi ya serikali kuwekeza katika elimu ni pamoja na Hakielimu yenyewe, Policy forum, Sikika, TenMet na TGNP.
Kwa niaba ya mitandao hiyo mkurugenzi huyo alisema hakukuwa na haja ya kufuta matokeo hayo na kufanya maboresho kwa kuwa sababu zilizosababisha kufeli kwa wanafunzi zinajulikana na si kama serikali inavyodai kwa sasa.

Missokia alisema kabla ya serikali kutoa uamuzi huo ilitakiwa kuweka wazi mapendekezo ya Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza matokeo hayo ili wadau wa elimu wapate fursa ya kuona sababu zilizochangia kushuka kwa ufaulu katika mitihani hiyo.

“Kwa kufuta matokeo hayo bila wadau kujua sababu na kutoa mchango wao inawaaminisha Watanzania kwamba sababu nyingine hata kama zipo ziliathiri kwa kiwango kidogo matokeo hayo na suala la upangaji wa madaraja kuonekana ni sababu kubwa zaidi kuliko nyingine,” alisema Missokia.

RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA HII HAPA.


KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo. Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya klabu zinazoshiriki michuano hiyo.



Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0 nyumbani.

DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)  

JK aaga kikosi cha kwenda DRC

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Rais Jakaya Kikwete amewaaga wapiganaji wa Tanzania wanaokwenda DR Congo kulinda amani kwa kuwadhibiti waasi wa vikundi mbalimbali kikiwamo cha M23 walioko Mashariki wa nchi hiyo.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana.Picha na Ikulu 

Kikwete alimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini humo katika hafla iliyofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni mwa mashuhuda katika hafla hiyo.
“Ninawatakia kila la kheri kwenye mapambano,” Amiri Jeshi Mkuu alimwambia kiongozi wa Batalioni ya Wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda nchini humo. Tanzania inaungana na Afrika Kusini na Malawi kufanya kuwapo kwa kikosi cha askari 3,100 huku Tanzania ikipeleka askari 850 kwa ajili ya kazi hiyo.
Vikosi vya awali vya Tanzania vimekwishatangulia nchini humo vikiongozwa na Jenerali James Mwakibolwa anayeongoza Brigedi hiyo chini ya UN, na tayari amewasili kwenye Mji wa Goma, ambao ndio Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini unaokaliwa na waasi wa M23 tangu Aprili 2012.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Monusco, vikosi vingine vya wapiganaji wa Tanzania na Afrika Kusini vitawasili wiki ijayo wakati Wanajeshi wa Malawi haijafahamika tarehe ya wao kuwasili.
Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...