Thursday, June 20, 2013

MAMA LANGA.... "NINGEKUWEPO TANZANIA MWANANGU ASINGEKUFA HARAKA"


MAMA wa marehemu Langa Kileo, Vanessa Kimei amefungua kinywa chake na kusema kifo ni mipango ya Mungu lakini kama angekuwepo nyumbani kwake Mikocheni, Dar, mwanaye asingekufa haraka kiasi hicho.Akizungumza na Amani hivi karibuni, Mama Langa alisema wakati mwanaye alipoanza kuugua hadi kupatwa na umauti Juni 13, mwaka huu, yeye alikuwa safarini nchini Marekani kumuona mwanaye mwingine aliyekuwa amejifungua.
“Wakati mwanangu ameanza kuumwa sikuwepo, nilikuwa safarini Marekani nilikoenda kumuona mwanangu wa kike aliyekuwa amejifungua, kwa mila za kwetu ni lazima mama kwenda kumuogesha mtoto lakini ningekuwepo mwanangu asingeondoka jamani,’’ alisema mama Langa.
Akifafanua kauli yake, mama huyo alibainisha kuwa kipindi alipokuwa akiishi na mwanaye kabla hajasafiri, mara nyingi alikuwa akimhudumia alipokuwa akiumwa hivyo hata katika ugonjwa uliosababisha mauti yake basi angeweza kumtibu yeye mwenyewe.
Alisema kuwa wakati mwingine alikuwa akimuwekea hadi dripu za dawa akiwa pale nyumbani na kunusuru maisha ya mwanaye lakini ghafla kifo kimetokea wakati yeye hayupo.


“Nilikuwa namuwekea dripu za dawa mwanangu hapahapa nyumbani, alikuwa anaugua kwa muda na kisha anarudi katika hali ya kawaida,” alisema kwa uchungu mama Langa.
Hata hivyo baadhi ya waombolezaji waliokuwepo msibani walimsihi mama huyo kukubaliana na mipango ya Mungu kwamba kila mwanadamu lazima atakufa, hali iliyompa faraja na kumfanya anyamaze.
Marehemu Langa aliyefariki baada ya kusumbuliwa na kile kilichoelezwa kuwa ni ugonjwa wa malaria kali na homa ya uti wa mgongo, alizikwa Jumatatu iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.

MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN AFARIKI DUNIA




Na Steven Kanyeph.
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel Ten CHARLES HILILA amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospital ya Mkoa wa Shinyanga.

Marehemu Charles Hilila alilazwa katika hospital ya mkoa tarehe kumi mwezi june mwaka huu akisumbuliwa na maradhi ya TB ya mifupa ambapo tarehe kumi na sita mwezi huu alihamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi mpaka mauti yalipomchukua .


Kwa mujibu wa mke wa marehemu amesema kuwa mazishi yatafanyika katika kijiji cha Jomu Tinde mahali alipozaliwa marehemu yakitanguliwa na misa takatifu ya mazishi itakayofanyika katika kanisa kuu la mama mwenye huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.

Marehemu Hilila ameacha mjane mmoja na watoto watatu, wakike mmoja na wakiume wawili.

Marehemu Hilila enzi za uhai wake alifanya kazi katika kituo cha televisheni cha chanel Ten lakini aliwahi kufanya kazi katika kituo cha matangazo cha radio Faraja. Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.

MSIKILIZE MBUNGE ALLY KEISSY WA NKASI ANAYEWAVUNJA MBAVU WABUNGE

Stori ya kwanza ni ya Mbunge wa Nkasi Ally Keissy June 18 2013 bwana alivunja rekodi ya kuwa mbunge aliechekesha watu wengi wakiwemo wabunge bungeni, sio tu kwa sababu ya kutoa vichekesho lakini pia ni kwa namna alivyokua akieleza mambo pamoja na kuikosoa Serikali.
.
Mbunge wa Nkasi Ally Mohamed Keissy.


Anakwambia ‘Twende Kigoma, Mwanza, Tabora, Mpanda, Shinyanga tuwaulize watu mnataka reli au viwanja vya ndege… mtashangaa wenyewe, vipaumbele gani mnapeleka viwanja vya ndege? mtu gani wa Tabora anapanda ndege kama sio Mbunge, DC na Mkuu wa mkoa… ? ni Treni…… hawataki viwanja vya ndege, viwanja vya ndege baadae…. 

kwanza ndege zenyewe zikwapi? mna ndege nyie???? mabilioni ya hela mnajenga viwanja vya ndege… ndege hatuna, wapanda ndege ni nyie wenyewe Wabunge na Mawaziri… jamani tutulie tuweke vipaumbele ambavyo vinaweza kusaidia Wananchi na uchumi wa nchi,  mtapakia mizigo, madebe mawese kwenye ndege? migebuka kwenye ndege? acheni mambo ya kurukiakurukia ndege zenyewe hamna”

WABUNGE WA CHADEMA WASIMULIA MATESO WALIYOYAPATA RUMANDE...!!!

Wabunge wanne wa Chadema, ambao waliachiwa na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande baada ya kukamatwa juzi. Vigogo hao; Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti maalumu), walikamatwa juzi baada ya wao na wafuasi wa chama hicho kutawanywa kwa mabomu ya machozi na polisi kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.Wabunge hao waliachiwa baada ya kujidhamini wenyewe huku watu wengine 65 waliokamatwa pamoja nao wakiachiwa baada ya kudhaminiwa.
 Wote wanatakiwa kuripoti kwenye kituo hicho Julai 22, mwaka huu na wataelezwa hatma ya suala hilo.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi lake linaendelea kuwasaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na kuwaonya kuwa wanatakiwa kujisalimisha mara moja.Chagonja alisema Mbowe na Lema wanatafutwa kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali katika viwanja hivyo vya Soweto walipokuwa wakitaka kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki dunia baada ya kuumizwa kutokana na mlipuko wa bomu, Jumamosi iliyopita.
Pia aliwaamuru Mbowe na Lema kuwasilisha mara moja ushahidi wa kuwahusisha polisi na shambulio la bomu na kama hawana imani na Polisi, basi wawasilishe ushahidi wao kwa Rais Jakaya Kikwete.

MAGAZETI YALEO ALHAMISI JUNI 20, 2013


.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...