Tuesday, April 09, 2013

SKENDO YA ASKOFU PENGO KUUZA MADAWA YA KULEVYA YAITIKISA KANISA KATOLIKI............!!!

 

SKENDO kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, anafanya biashara ya madawa ya kulevya, ilitikisa kisha ikapoa, ila sasa Uwazi lipo kwenye nafasi nzuri ya kupasua jipu.


Januari mwaka jana, Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kutamka hadharani kuwa anaambiwa anauza ‘unga’, kipindi hichohicho, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ambaye alisema wanafanya kazi kisayansi.
“Kama jina la Pengo tunalo kwamba anauza madawa ya kulevya au hatuna, siwezi kutamka kwa sasa, hatutaki kupindisha ushahidi au kuvuruga upelelezi wetu,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, hivi karibuni, Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa vigogo wa jeshi la polisi nchini, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, akasema kuwa suala la Pengo lina utata ila siyo zito.
“Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya,” alisema kigogo huyo.
Aliongeza: “Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya.”...

RAILA ODINGA ASUSIA ZOEZI LA KUPISHWA KWA RAIS WA KENYA NA KUKIMBILIA AFRIKA KUSINI


 Wako kwenye mbuga za wanyama Afrika Kusini wanakula bata ....ni Raila Odinga na wenzake wawili akiwemo Kalonzo Musyoka.
Taarifa kuhusu kina Odinga na wagombea wenza kwenda Afrika Kusini zimetokea @FORA_2013 page ya Organisation inayomsupport Odinga aliekua mgombea Urais kwenye Uchaguzi wa Kenya ambao Uhuru Kenyatta ndio katangazwa mshindi na anaapishwa leo.

Inadaiwa Raila Odinga na wagombea wenza wameamua kukwepa kuwepo kwenye kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kuamua kwenda Afrika Kusini .

HILI NDILO POZI LA LULU LA MITEGO KATIKA SIKU YA KUMUENZI KANUMBA


 Hii ndo picha ya kimitego imewekwa kwenye instagram na Lulu kwenye siku ya kumuenzi marehemu Kanumba  ikiwa  ni  masaa  machache  tu  baada  ya  kutoka  katika  kaburi  la  marehemu Kanumba.....

HII PICHA YA UHURU KENYATTA ENZI ZA UTOTO AKIWA NA BABA YAKE MZEE JOMO.

.Mzee Jomo Kenyatta akiwa na mwanae Uhuru Kenyatta enzi hizo akiwa mdogo ambapo leo ndio ameapishwa kuwa Rais wa Kenya. (imetoka Nation Media Kenya)

MAMA KANUMBA AMSAMEHE LULU YALIYOTOKEA AMWACHIA MUNGU


Mama wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa upande wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia mungu

Akizungumza katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo humkumbuka mwanaye

Alisema kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto kwake, mume, rafiki, kaka  alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na alimfanya kuwa karibu kwake na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo imemfanya kuwa mpweke mpaka leo

SOMA WABUNGE TZ WALIVYOKULA MSOTO JESHINI


Kutoka kushoto: Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid.
WABUNGE katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), walipata msoto wa nguvu.

Tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kwamba wabunge hao wangepewa mafunzo kwa kubembelezwa kutokana na nafasi zao, walikutana na msoto wa nguvu mwanzo hadi mwisho.

HILI NDIO JUMBA LA MILIONI 500 ZA KENYA SERIKALI ALILOMZAWADIWA RAIS MWAI KIBAKI.

..
Wakati Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa leo kuiongoza nchi hiyo, nimeipata ripoti ya kituo cha TV cha NTV inayoonyesha jumba lililojengwa na Serikali ya Kenya kwa ajili ya kumzawadia Rais Kibaki anaestaafu.
Ripoti ya NTV imeamplfy kwamba kuna uwezekano Rais huyo akaja kuishi kwenye nyumba hii iliyopo Mweiga Nyeri nchini humo japo pia kuna taarifa nyingine zinaamplfy kwamba Rais huyo hapendelei maisha ya kijijini, zaidi anapenda mjini.
Mwai Kibaki mwenye umri wa miaka 81, anamiliki nyumba tatu za kifahari kwenye jiji la Nairobi na ana nyumba moja nyumbani kwao alikowahi kuwa mbunge.
..Na Millard Ayo

ADHABU YA VIBOKO KURUDISHWA KWA WANAFUNZI KURUDISHWA MASHULENI

Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.


 
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo  

“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.


Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”


Aliyalaumu mashirika yasiyo ya kiserikali na haki za binadamu ambayo yamekuwa yakipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo shuleni na kusababisha kushuka kwa nidhamu kwa kiasi kikubwa.

Uhuru Kenyatta kuapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Kenya.

Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, anaapishwa rasmi leo huku marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakitazamia kuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kwenye sherehe hizo.



Uhuru na mgombea mwenza wake, William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka jana kwa zaidi ya kura milioni 6.13 na hivyo kumshinda mpinzani wake Rail Odinga, aliyepata kura milioni 5.3 .


Uchaguzi huo ulifuatiwa ule wa Desemba mwaka wa 2007 uliomalizika kwa ghasia za kikabila na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine kupoteza makazi.
Kuhusu sherehe, maofisa wa Serikali ya Kenya, walisema zinatazamiwa kuhudhuriwa na viongozi kadhaa barani Afrika na kwamba baadhi yao walianza kuwasili nchini humo tangu jana.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameambatana na maofisa kadhaa wa Serikali yake.Wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.


Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu kuhusu kuhudhuria kwa kiongozi huyo wa Sudan anayetakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayomtuhumu kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu katika Jimbo la Darfur.

Ziara ya Jay Z na Beyonce nchini Cuba yazua utata kwa baadhi ya wanasiasa nchini Marekani.


Wanasiasa wawili wa bunge la Kongres la Chama cha Republican nchini Marekani wamehoji iwapo ziara ya wanamuziki maarufu wa nchi hiyo mume na mke Jay Z na Beyonce nchini Cuba ilikuwa na kibali cha serikali.
Mastaa hao wamepigwa picha kadhaa wakiwa mjini Havana wakisalimiana na mashabiki wao, wakitoka kupata msosi na kutembelea sehemu kadhaa za mji huo wakati wakisherehekea miaka mitano ya ndoa yao.

Hata hivyo vikwazo vya kibiashara vya Marekani vinazuia wamerekani kuitembelea Cuba kwa sababu za kiutalii pekee na anayetaka kusafiri lazima aombe kibali maalum.
Wanasiasa hao Ileana Ros-Lehtinen na Mario Diaz-Balart wametuma barua kwa Idara ya hazina ya Marekani wakiulizia ni aina gani ya kibali walichopewa wanamuziki hao kuitembelea nchi hiyo.

Wamesema vikwazo vya kuitembelea nchi hiyo viliwekwa kwa sababu marekani iliiorodhesha serikali ya Cuba kama taifa linalounga mkono ugaidi na kudai kuwa nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa kawaida sababu za muhimu zinazoweza kumruhusi raia wa Marekani kwenda Cuba ni pamoja na matibabu, kusoma, sababu za kidini, huduma za kijamii na sababi nyingine za kibinadamu.

Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv apatikana.


Masoud Said (38), mkazi wa Mbeya akifurahia kitita cha Tshs 10,000,000 alizozawadiwa na DStv kwenye campaign ya DStv Rewards. Kila wiki, DStv wamekuwa wakitoa Tshs 5,000,000 kwenye droo maalum kwa wateja wake wanaofanya malipo kabla ya akaunti zao kukatika. Kushoto ni Meneja wa Fedha wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Francis Senguji na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu.
Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv  Masoud Said akiwa ameshikilia mabulungutu ya fedha zake.

Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare

POLISI WADAIWA KUMFANYIA UNYAMA KADA WA CHADEMA
HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.
Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 09.04.2013

.
.
.

MFANYABIASHARA WA KIHINDI AUAWA NA KUPORWA MIL 100, SALENDER BRIDGE

Majambazi yamempiga risasi mfanyabiashara wa Kihindi na kumuua papo hapo na kumpora shilingi milioni 100 eneo la Salender Bridge, Upanga Dar es Salaam jana jioni .
Kwa mujibu wa walioshuhudia sakata hilo, wanasema mtoto wa kike wa marehemu pia alipigwa risasi ya paja, lakini akafanikiwa kuendesha gari lao huku akiwa na mwili wa marehemu babake hadi Hospitali ya Regency.
Hivi sasa msichana huyo shupavu, anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo...
Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kadri tutakavyokuwa tunazipata..

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...