Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Amal alimuo9mba rafiki yake kumpelekea mumewe anayepigana nchini Syria pauni 15,800
Mwanamke
mmoja nchini Uingereza aliyeshitakiwa kwa kumfadhili mumewe aliyejiunga
na vita nchini Syria, amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.
Amal
El-Wahabi, mwenye umri wa miaka 28, alijaribu kumhadaa rafiki yake
kumbebea pauni 15,800 hadi nchini Uturuki ambako mumewe angeweza
kuzichukulia. Jaji aliyetoa uamuzi katika kesi hiyo, Nicholas
Hilliard, alimwambia El Wahabai kuwa alifahamu vyema kwamba mumewe Aine
Davis alikuwa anapigana nchini Syria na kwa hivyo alikuwa anamsaidia
katika harakati zake. Davis, ambaye alikuwa mlanguzi wa dawa za
kulevya pamoja na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha, aliondoka
Uingereza mwaka 2013 kwenda Syria kupigana na kundi la Isis. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Mafuta yaliyovuija yaliathiri mazingira na kusababisha watu kuapoteza kazi.
Mawakili
wanaoiwakilisha jamii ya watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira
anasema wakuu wa kampuni ya mafuta ya Shell walijulishwa mapema kuhusu
kuchakaa kwa mabomba yake ya mafuta.
Hii ilikuwa kabla ya kutokea
kwa visa vya kumwagika mafuta mara mbili hivyo kuchafua pakubwa eneo
hilo Lagoniland Kusini mwa Nigeria mwaka 2008. Shell inakana kwamba ilikuwa na taariifa kuwa mabomba hayo yalihatarisha usalama. Shell
inadai mabomba hayo yalipasuliwa na wezi wa mafuta lakini mawakili hao
wamejibu kwamba mabomba hayo yalikwa duni na yalimwaga mafuta hata
kwenye ziwa la eneo hilo ambako sasa uvuvi haufanyiki tena. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz