Tuesday, December 31, 2013

JAMAA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR LEO NA KUGOMA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAISI KIKWETE

 Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 31, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

MAAJABU YA MWAKA: MUME AUZA KABURI LA MKEWE...!!!


Hii ndiyo kali ya kufungia mwaka katika zote zilizotokea mwaka 2013! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar, anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe, Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.

MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao wanapingana na tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya marehemu mama yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.
 “Kiukweli alichokifanya baba siyo sawa. Haiwezekani auze eneo ambalo lipo kaburi la mama yetu. Mbaya zaidi hadi sisi watoto wa kutuzaa yeye mwenyewe anatutishia maisha.

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii

Monday, December 30, 2013

BONGO MOVIE KAMA KAWADA YAO SAFARI HII WAMFANYIA WASTARA, MWEEEEEEE...!!!

DUA maalum ya kumbukumbu na kumuombea aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ imezua minong’ono mingi kufuatia wasanii wengi wanaounda Kundi la Bongo Movie kudaiwa kumfanyia mbaya mkewe, Wastara Juma kwa kutohudhuria. Dua hiyo ya ilifanyika Jumamosi iliyopita nyumbani kwa marehemu Tabata-Bima, Dar na kumalizikia kaburini kwake Kisutu. Katika tukio hilo, wadau mbalimbali wa filamu na burudani, walionekana kushangazwa na kitendo cha wasanii wengi wa Bongo Movie kutokuwepo licha ya marehemu Sajuki kushirikiana nao kwa karibu enzi za uhai wake. Aidha, wengine walifika mbali kwa kuhoji kulikoni wafanye hivyo, maswali ambayo yalimuongezea uchungu mkubwa Wastara aliyekuwa akibubujikwa machozi mara kwa mara. Kwa upande wake, Wastara alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli hiyo na kuwaombea kwa Mungu wote waliojitokeza kumuunga mkono kwenye dua hiyo. “Nawashukuru wote waliojitokeza, wamenifariji sana,” alisema Wastara kwa simanzi.
Wasanii wa filamu waliohudhuria dua hiyo, ni pamoja na Denis Sweya ‘Dino’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Flora Mvungi, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na Suleiman Bin Sinan ‘Bond’.  
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ alipotafutwa, simu iliita bila kupokelewa.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, 2012 na katika kutimiza mwaka mmoja kaburini misa nyingine itafanyika nyumbani kwa wazazi wake mkoani Songea Januari 2, 2014.
Na GPL
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

WABUNGE 15 KUKATWA MISHAHARA KWA KOSA LA KUCHUKUA POSHO ZA SAFARI BILA KUSAFIRI...!!!

Katibu wa Bunge  Dk. Thomas Kashililah akiwa ofisini kwake jana wakati wa mahojiano na mwandishi wa gazeti hili. Picha na Kelvin Matandiko  
********
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa habari hii, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.
Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.
Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

MAALIM SEIF: "WAZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI"

maalim1 1e311
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Wazanzibar wanaisubiri kwa hamu Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona kama imezingatia masilahi na matakwa yao katika kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.
Msimamo huo ameutoa kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, Mkoa wa Kalazini Unguja na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Aidha, katika mkutano huo, kwa mara ya kwanza Waziri wa zamani wa SMZ na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mansoor Yussuf Himid alihutubia tangu avuliwe uanachama wa CCM kutokana na madai ya kwenda kinyume na sera, maadili na nidhamu ya chama hicho.
Katika maelezo yake, Maalim Seif alisema wanachodai Wazanzibar
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
Alisema Zanzibar ilikuwa taifa huru lililoungana na Tanganyika kwa ridhaa na siyo mateka wa Tanganyika, hivyo wanayo sababu ya kujitegemea.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

JAJI MKUU AWA MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLIKANA ZANZIBAR


Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.
Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati Mzee Abeid Amani Karume.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 30, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.


Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

Sunday, December 29, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 29, 2013 YA MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

MENEJA WA WEMA SEPETU AHUSISHWA KWENYE UJUMBE WA JACKIE CLIEF ALIOUTUMA MASAA MACHACHE KABLA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA

Yaelekea mwanadada Jackie alikuwa amejipanga kisawa sawa na alijitoa muhanga na kujua lolote lingeweza kumpata kutokana na kazi aliyo kuwa akifanya ya kubeba sembe. 
Jackie alijipanga na  kuamua kumuachia rafiki yake kipenzi Martin Kadinda maagizo na wosia wake just incase ikatokea akafariki. Jackie aliweza kuandika ujumbe huo kwenye status yake ya BBM kama inavyo onekana hapa chini.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

Saturday, December 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 28, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

LUMBESA LA VIPODOZI FEKI LAKAMATWA IRINGA


 Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana. (Picha na Denis Mlowe)

Friday, December 27, 2013

MAGAZETI LEO IJUMAA DESEMBA 27, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

HII HAPA NDIO SIRI YA PINDA KUNUSURIKA

*Katibu Umoja wa Wanawake aadhirika kikaoni
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Ijumaa iliyopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliponea chupuchupu kung’olewa uenyekiti wa kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.

Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.

Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.

Thursday, December 26, 2013

RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO ALHAMISI

15:45 Hull City Vs Manchester United
18:00 Aston Villa Vs Crystal Palace
18:00 Cardiff City Vs Southampton
18:00 Chelsea Vs Swansea City
18:00 Everton Vs Sunderland
18:00 Newcastle United Vs Stoke City
18:00 Norwich City Vs Fulham
18:00 Tottenham Hotspur Vs West Bromwich Albion
18:00 West Ham United Vs Arsenal
20:30 Manchester City Vs Liverpool

Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

PAPA FRANCIS ATETEA WANYONGE WA VITA

Papa Francis akipungia mkono waumini Vatikani
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.
Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.
Alisema:
"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.
Wacha tuendelee kumuomba Mungu awaepushe wapendwa watu wa Syria na maafa zaidi, na kuziwezesha pande zilizohusika na vita kumaliza ghasia na kuruhusu msaada ufike kwa wale wanaouhitaji"
Papa Francis piya alitoa wito kwa mapigano kusitishwa Sudan Kusini na aliwaomba viongozi wa kimataifa kushughulikia zaidi yanayotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo alisema mara nyingi haitiwi maanani.
Akizungumza juu ya mamia ya wakimbizi kutoka Eritrea waliozama karibu na kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa mwezi Oktoba, alieleza wasiwasi wake kuhusu wale wanaohatarisha kila kitu ili kutafuta maisha bora.
Piya alizungumzia swala la ukatili majumbani, akitetea wanawake wanaopigwa.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

DIAMOND AMTAMBULISHA TENA WEMA, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA....!!!


sdd 
Tukio hilo lilitokea jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Nasikia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
994992_654719497904805_1370630389_n

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 26, 2013, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

Wednesday, December 25, 2013

HILI NDILO BARAZA LA MAWAZIRI LINALOTAKIWA


Rais Kikwete. 
********
Baada ya kizaazaa cha wiki iliyopita ambapo mawaziri wanne walipoteza kazi zao kutokana na kuwajibishwa kwa vitendo vya ukatili na mauaji vilivyotokea wakati watendaji katika wizara zao walipokuwa wakiendesha ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ nchi nzima, kinachosubiriwa na wananchi hivi sasa ni Rais Jakaya Kikwete kuunda Baraza jipya la Mawaziri.
Kutokana na udhaifu mkubwa katika utendaji ambao kwa muda mrefu umeonyeshwa na mawaziri wengi katika Baraza la Mawaziri, hatudhani kama kuna mwananchi hata mmoja  anayemtarajia Rais Kikwete kujaza tu nafasi za mawaziri aliowafukuza wiki iliyopita.
Nderemo na vifijo vilivyotokana na furaha ya wananchi katika kila kona ya nchi baada ya mawaziri hao kuondolewa katika nyadhifa zao ni ishara tosha kwamba hawamtarajii Rais Kikwete kuishia hapo, isipokuwa kuwaondoa mawaziri wengine wengi ambao tayari wamethibitika na hata kutajwa na chama chao cha CCM kuwa ni ‘mawaziri mizigo’.

KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KWA WADAU WOTE WA JAMBO TZ

Tunapenda kuwatakia kheri ya Chistmas na Mwaka mpya wapenzi wasomaji wa blog hii na page yetu ya facebook.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili  tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

HII NDIO KADI YA CHRISTMASS TOKA KWA MHE. EDWARD NGOYAI LOWASSA KWENDA KWA WATANZANIA WOTE

Tafadhari Like ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA X-MASS DESEMBA 25, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.



 

.

Tuesday, December 24, 2013

SOMA TAARIFA KUHUSU BEI MPYA ZA UMEME ZITAKAZOANZA KUTUMIKA TAREHE 1 JANUARI 2014

tanesco
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.
Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.
Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.


Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 
Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

HII HAPA TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS


Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

WANAMUZIKI WA KUNDI LA PUSSY RIOT WAACHIWA HURU

Wanamuziki wote wa kundi la muziki wa Punk la Pussy Riot la nchini Russia wameachiliwa huru kutoka gerezani chini ya sheria ya msamaha.
Nadezhda Tolokonnikova aliachiwa huru kutoka hospitali moja ya gereza lililopo Siberia, wakati mwenzake Maria Alyokhina aliachiliwa huru Jumatatu huko Nizhny Novgorod.
Wote wameuita msamaha huo kuwa ni sawa na sarakasi za serikali za kujisafisha kabla ya kufanyika kwa michezo ya olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika Russia Februari mwakani.
Wanawake hao wanamuziki walifungwa Agosti 2012 baada ya kuimba nyimbo inayokejeli katika kanisa kuu jijini Moscow.
Kitendo chao kilitafsiriwa kama kumkufuru mungu na wananchi wengi wa Russia lakini kutiwa kwao hatiani kwa kosa la utukutu ukichochewa na chuki dhidi ya dini ulishutumiwa na vikundi vya kutetea haki za binadamu, wanaharakati wanaompinga Rais Vladmir Putin na mataifa ya nje.
Watu wengi wanaotumikia vifungo wanauona msamaha huo kama jaribio la Rais Putin la kusafisha taswira yake katika nchi za magharibi na kuiboresha rekodi yake ya haki za binadamu kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki huko Sochi Februari 2014.
Siku mbili baada ya sheria hiyo ya msamaha kuanza kutumika, Rais Putin alimsamehe Mikhail Khodorkovsky, ambaye siku za nyuma alikuwa ni mtu anayeongoza kwa utajiri nchini Russia na mkosoaji binafsi wa sera za serikali, hatua ambayo pia ilitafsiriwa kama kuyaridhisha mataifa ya magharibi.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 24, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA

Sunday, December 22, 2013

MWIGULU NCHEMBA AMWONYA SPIKA WA BUNGE


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumu.
Mkuya katika maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu kwa mtu mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17.
Katika mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MWENYEKITI WA YANGA YUSUPH MANJI BAADA YA KUFUNGWA NA SIMBA JANA


Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.

DUUUUUH...!!! WASANII WETU MIZINGUO TU, ANGALIA MAKOSA KWENYE MOVIE MPYA YA RAY


kwenye scene hii anaonekana camera man kwa mbali ukiangalia kwenye viio vya nyumba io ni baada tu ya wazee wao kurudi kutoka Zanzibar 
....

MAN UNITED YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI ENGALND, LIVERPOOL NAO KAMA SIMBA SC, YAUA 3-1 SUAREZ APIGA BAO MBILI

article-2527121-1A3CB4FD00000578-469_634x428_876c6.jpg
Adnan Januzaj akishangilia baada ya kuifungia Manchester United dhidi ya West Ham
Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi ya nne mfululizo, baada ya jana kuilaza West Ham mabao 3-1 Uwanja wa Old Trafford.
Danny Welbeck alifunga bao la kwanza nyumbani tangu Oktoba 2012 dakika ya 26 na Adnan Januzaj akafunga la pili dakika ya 36 kabla ya Ashley Young kumaliza kazi kwa bao la dakika ya 72 na Carlton Cole akaifungia West Ham bao la kufutia machozi dakika ya 81.

KWA UPANDE WA LIVERPOOL article-2527114-1A3C51FE00000578-586_634x433_3b6f0.jpg
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Cardiff Uwanja wa Anfield jana.
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendeleza makali yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 3-1 dhidi ya Cardiff jioni hii Uwanja wa Anfield.
Nyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 25 na 45, wakati bao lingine la Liverpool lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 42 wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Jordon Mutch.
Ushindi kama huo imepata Simba SC nchini Tanzania jana wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC na Mrundi Amisi Tambwe akifunga mabao mawili moja Awadh Juma.
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu click neno Jambo Tz kisha like page

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 22, 2013

..

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...