Friday, May 24, 2013

ASILIMIA 31 YA WATANZANIA NI WALEVI

Asilimia 26.8 hadi asilimia 31.9 ya Watanzania wanatumia pombe na asilimia 27.4 kati ya hao ambao ni wanaume na wengine asilimia 13.4 ambao ni wanawake, ni walevi wa kupindukia. Bunge lilielezwa jana.


Takwimu hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambaye alisema kuwa viwango hivyo vimetokana na utafiti uliofanywa kati ya Februari hadi Oktoba mwaka jana 2012.

Kwa mujibu wa naibu waziri, utafiti huo ulifanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alikuwa akijibu swali la Abdallah Haji Ali (Kiwani–CUF) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu utumiaji wa pombe ambao umethibitika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.
Pia alipendekeza pombe ipigwe marufuku kabisa hapa nchini kwa kuzingatia madhara yake.

Naibu waziri alisema tafiti zimeonyesha kuwa watu milioni mbili wanafariki dunia kila mwaka duniani kutokana na madhara ya matumizi ya pombe na asilimia nne ya matatizo ya kiafya yanatokana na matumizi ya pombe.
“Hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na ustawi wa jamii inayochangiwa na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na Ukimwi,” alisema Dk Rashid.

Naibu Waziri alisema kutokana na kuongezeka kwa athari zitokanazo na matumizi ya pombe hasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Serikali inatekeleza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukizwa unaoelekeza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali.
Kuhusu mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo, alisema tayari Serikali imeanza utaratibu wa kuziwezesha hospitali za rufaa za mikoa, kuanza kutoa huduma kwa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

JWTZ WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI WAKE KUJIHUSISHA NA MAKAHABA DRC

Dar es Salaam. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa zilizotapakaa kwenye mitandao kuwa askari wa jeshi hilo waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda amani,wameanza kujihusisha na makahaba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa www.congodrcnews.com wanajeshi wa Tanzania wameanza kujihusisha na ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana na mwanamke mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza shida zake ambazo ilielezwa alizifanya bila kinga yoyote,askari huyo alikataa kumlipa ujira wake,hali iliyoleta tafrani na mwanamke huyo kupiga kelele.
“JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo mtupu wenye nia ya kulipaka matope JWTZ na Tanzania kwa ujumla. “Picha iliyotolewa kwenye tovuti hiyo ya www.congodrcnews.com ni ya wanajeshi wa Tanzania walipokuwa katika Operesheni ya huko Comoro mwaka 2008.

MUME WA MTU ANASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI


INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia  katika  dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.


Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini. 



Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 24, 2013

DSC 0113 919d1
DSC 0108 36939
DSC 0111 4ea7b

MCHUNGAJI WA 'TAG' KILIMANJARO ATIWA MBARONI KWA KULAZIMISHA PENZI LA KONDOO WAKE BILA KINGA.

KESI ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG), Jean Felix Bamana, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumatatu wiki hii ilianza kurindima katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Kilimanjaro huku upande wa walalamikaji ukiiambia korti, ‘mchungaji alitaka penzi bila kinga’.
Mchungaji huyo alitiwa mbaroni

Machi 13, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar akiwa na wanafunzi wawili, watoto wa familia moja, Artha Swai (17) na Angel Swai (19) ambao alidaiwa kuwatorosha kutoka mjini hapa.

Katika kesi ya msingi, mchungaji huyo alidaiwa kuwadanganya watoto hao kwamba alikuwa akiwafanyia mpango wa kwenda kusoma nje ya nchi lakini badala yake aliwaweka hotelini na kumtaka kimapenzi mmoja wao

MCHUNGAJI AFUMANIWA NA KUTEMBEZWA UCHI HADI KANISANI.


Mtumishi mmoja wa Mungu amejikuta akipata aibu ya mwaka si tu mbele za Mungu bali hata kwa mkewe pamoja na mashuhuda wengine baada ya mkewe kumfumania ‘live’ kitandani akifanya mapenzi na mwana kwaya wa kanisa lake huko Kisumu nchini Kenya.Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Kenyan-Post zinasema msichana huyo mweye miaka 23 amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na pasta huyo kabla hawajabambwa.
Kisa hiki ni kama movie ambazo tumezoea kuziona zenye story line ambayo unaweza kutabiri mwisho wake. Kwa mujibu wa mtandao huo, ile ‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo alikuwa anatarajia kusafiri kwenda nyumbani kwao kusalimia wazazi wake hivyo mumewe alimsindikiza mpaka kituo cha basi, lakini alionekana kuwa mtu mwenye haraka na kumwambia mkewe kuwa siku hiyo ana mkutano muhimu hivyo anapaswa kuwahi. Baada ya kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa haraka na kuondoka,

Huku nyuma mke wa pasta kwa bahati mbaya (upande wa pasta) na bahati nzuri (upande wake) aligundua kuwa amesahau zawadi aliyokuwa amemnunulia mama yake mzazi ambaye ndio anaenda kumsalimia hivyo ikabidi airudie nyumbani kisha asafiri na basi litakalokuwa linafuata.
Alipofika nyumbani anapoishi na mumewe alishangaa kukuta mlango haujafungwa kwa nje na huku anakumbuka walipoondoka waliufunga hivyo akahisi huenda wamevamiwa mchana kweupe, alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani ndipo alipoomba msaada wa majirani wakavunja kitasa na kuingia ndani.
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa kile alichokikuta ndani baada ya kumkuta msichana anayemfahamu kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani la mumewe wakiwa uchi wa mnyama katika kitanda chake na mumewe.
Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia kitandani na kuzitupa nje kupitia dirishani nguo zao wote lakini kwa bahati mbaya msichana aliyemfumania alifanikiwa kukimbia na kumuacha pasta mwenyewe.
Huwa wanasema hasira ni hasara na maamuzi ya hasira hugeuka majuto baadae, baada ya mmbaya wake kukimbia aliamua kumvuta mumewe (pasta) akiwa uchi wa mnyama na kumtembeza mbele ya umati wa watu mpaka katika kanisa analotoa huduma pasta huyo kwa lengo la kufichua mabaya yake.
Bahati nzuri alijitokeza mwanaume mmoja aliempatia shati lake ili ajisitiri.

POLISI ALIEKAMATWA NA GUNIA ZA BANGI ATOKOMEA KIZANI NA WALE WALIOKAMATWA NA FUVU NAO VILE VILE


Na Eliya Mbonea, Arusha
ASKARI Polisi Koplo Edward, anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya (bangi) gunia 18 ametoroka chini ya ulinzi wa askari polisi saba na kutokomea kusikojulikana. Mtuhumiwa huyo, alikuwa dereva wa gari aina ya Toyota Landcruiser namba PT. 2025 la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana, kwamba askari huyo akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi saba, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya ukaguzi.
Alisema wakiwa nyumbani kwa mtuhumiwa, waliingia ndani kuendelea na upekuzi, lakini katika mazingira ya kutatanisha aliwatoroka na kukimbia bila kufanikiwa kumkamata.
Alisema kutokana na hali hiyo, polisi mkoani Arusha limemkamata Inspekta wa Polisi Izaack Manoni aliyekuwa anasimamia upekuzi huo.

“Inspekta Manoni yupo chini ya ulinzi na hatua za kinidhamu dhidi yake zitachukuliwa,” alisema ACP Sabas na kuongeza:“Mtuhumiwa Edward, anayetafutwa kwa sasa alishafukuzwa kazi, akipatikana atafikishwa mahakama ya kiraia kusomewa mashitaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya,” alisema.

KATIKA VURUGU ZA GESI MTWARA, ASKARI WATUHUMIWA KUMBAKA HADI KUMUUA KWA KUMPIGA RISASI YA TUMBO MAMA MJAMZITO WA MIEZI 7....!!


Hali ya usalama katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa imezidi kuwa mbaya baada ya askari polisi kudaiwa kufanya unyama kwa kuwabaka wanawake na kumpiga risasi mjamzito

Mbali na unyama huo polisi pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba tatu za wananchi katika mtaa wa Magomeni na vibanda vya maduka kadhaa na kupora vitu vilivyomo ndani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa anasema hali ni shwari na kwamba wananchi watoke nje kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi amethibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, zinazoaminika kuwa za risasi na hivyo kufanya idadi ya maiti zilizopokelewa hospitalini hapo kufikia mbili na majeruhi 18: “Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba, amepigwa risasi tumboni...” “...pia tumepokea mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chuno, amevunjwa miguu yote kwa risasi.”

RAIS KIKWETE ATANGAZA VITA KUHUSU VURUGU ZA MTWARA.....AMESEMA SERIKALI YAKE ITAWASULUBU WACHOCHEZI WA VURUGU


WAKATI hali ikizidi kuwa tetea Mkaoni Mtwara kufutia Mapigano yaliyoanza jana Mkoani humo Rais Kikwete amevunja ukimwa wake na kutoa amri wahusika wakuu wa tukio hilo kusakwa mara moja.
Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.
Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo...“Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”
Kwa upande wake Waziri Muhongo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara yake alisema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasina Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:
“Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki lijalo.”
“Tumezungumza mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama hawajaelewa, nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana Mtwara katika mradi huo."

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...